Hivi Hawa polisi wanatumwa na nani na kwa lengo gani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Hawa polisi wanatumwa na nani na kwa lengo gani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Expedito Mduda, Jan 5, 2011.

 1. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ndugu Watanzania, kama mnakumbuka CHADEMA walitaka kuandamana siku fulani huko nyuma baada ya uchaguzi wa meya wa Arusha wakidai kuwa uchaguzi ule haukuwa halali!
  Kwa mtu mwenye kufuatilia mambo, ni kweli uchaguzi ule haukuwa halali hata kidogo.
  Polisi walifanya fujo kwa kumpiga mbunge wa Arusha mimi nasema bila kosa kwani kwenye uchaguzi wa meya polisi walipelekwa kwa ajili ya nini.
  Baada ya maelewano kati ya IGP na viongozi wa CHADEMA, maandamano yakapangwa yafanyike tarehe 5, Januari. Leo hii.
  Mpaka jana asubuhi maandamano hayo yalikuwa halali. Jioni IGP kama kawaida inavyoonekana kuwa ndio mtindo wa siku hizi akasema maandamano hayo yasifanyike ila mkutano ufanyike kwa kisingizio kuwa habari za kiintelijensia inaonesha kuwa katika maandamano hayo kungekuwa na fujo!
  CHADEMA wameshikilia msimamo wao kuwa kuandamana ni haki yao kitu ambacho ni kweli maandamanoni haki.
  Wakati wa maandamano, tumeona polisi wakibomoa vioo vya magari wakati huo wafuasi wa CHADEMA wakiwa watulivu bila kufanya lolote.
  Polisi wamewashika viongozi wa CHADEMA na kuwaweka ndani.
  Mimi napenda kujua kama Raisi Kikwete kama binadamu, je anaona uonevu huu? Yeye yupo madarakani tumempa ridhaa ya kuongoza nchi hii ya amani na amani iliyosotewa na waasisi wa taifa letu hili. Yeye Kikwete anajisikiaje kuona amani ya nchi yetu inapopotelea mikononi mwake?
  Eti nyie maaskofu na mashehe mambo haya mnayaona? Hivi tuseme baada ya kifo cha baba wa taifa hakuna tena mtu yoyote mwenye uchungu na nchi yetu hii aiokoe? Ninyi mnahubiri dini na kila siku mnaona mambo yanavyoenda mrama. Je, mnataka mpaka damu imwagike ndipo mtoe maneno yenu? Mimi nawashangaa sana maaskofu ma mashehe maana sikutegemea kwamba mnawenza kubaki bubu kiasi hicho mpaka amani yetu inaanza kupotea kwa kuonekana kabisa.
  Nyie viongozi wa siasa, tafadhali sana achani kufanya amani yetu itoweke eti kwa sababu ya uroho wa madaraka na kufanyia kazi matumbo yetu. Tunaomba mtukome kabisa muiache nchi yetu amani itawale. Achane demokrasia ifuate mkondo wake. Kwanza kinachofanyika ni wizi mtupu. Kila kukicha mnatubebesha matatizo ya mara UMEME, DOWANS, MEREMETA, n.k.
  Tunaomba wote mnaofikiri nchi hii ni ya mama zenu muondoe mawazo hayo, nchi hii ni yetu wote na tunaomba tuheshimiane. Nyie mnatembea kwenye mashangingi sisi wananchi tunateseka. Hivi jamani ubinadamu mmeuweka pembeni? kitendo tu cha polisi kuvunja vioo vya gari la watu ambao kwa kweli hawakuwa hata na silaha yoyote inaonesha Tanzania inageuka kuwa nchi yenye watu wanaoishi kwa kugugumia tu!
  Hivi tujiulize, kwa nini hao polisi wasingeruhusu hayo maandamano na wenyewe wawalinde waandamanji ili wasifanye fujo. Ndugu zangu, hasa rais Kikwete tunakuomba sana uwe mbele kutetea amani hii. Ujue amani hii haikuja tu kama muujiza bali kuna watu waliifanya ikawa. Hivi wewe huoni haya mambo? Unajua mimi binafsi nashindwa kuelewa vizuri kama hiki kinachokuja moyoni mwangu kwako hakiji. Uonevu siyo mzuri.
  MIMI NAOMBA DEMOKRASIA TUIACHE IFUATE MKONDO WAKE!
   
 2. V

  Vipaji Senior Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NDUGU YANGU KUMBUKA RAISI WA CCM HANA SAUTI KWA UJUMLA NASEMA TANGANYIKA HAINA RAIS POLISI WALIOPO NI WA NCHI YA MAFISADI. WAZO LAKO NI ZURI LAKINI POLISI WENGI HAWAJUI HATA KUSOMA MITANDAO KAMA HII. HALAFU KWA AJILI YA MAZOEA WANAFANYA KAZI ZA MABWENYENYE :redfaces:
   
Loading...