Hivi hawa Polisi kwanini wanafupisha maisha ya watanzania bila sababu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi hawa Polisi kwanini wanafupisha maisha ya watanzania bila sababu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by No admission, Feb 23, 2012.

 1. No admission

  No admission JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Jamvi;

  Naomba jamani nitoe hiki kilio changu kwani moyo wangu unashindwa kabisa kuvumilia jinsi maisha ya watanzania wenzangu yanavyokatishwa bila sababu na hawa polisi. Ilikuwa Arusha, Mara, Mbeya na sasa Songea watanzania wanauwawa kisa kuandamana. Kuandamana ni haki ya kisheria wananchi lakini Polisi wamekuwa wanatumia nguvu na ubabe zaidi kuliko akili na busara. Kwa hili la Songea Mkuu wa mkoa angetoka na kuongea na wananchi wake tusingefika hapa lakini hakuona sababu ya kufanya hivyo akaamua kutumia nguvu na baada ya mauaji ndiyo anaita kikao cha kamati ya ulinzi ya mkoa. Kule Mbeya Kandoro alitumia miguvu bila mafanikio baada ya mbunge mwenye busara Mr Sugu kuja na kuwasikiliza wananchi fujo ziliisha.

  Je kwanini serikali hailaani haya mauwaji wala kuwashitaki polisi waliofanya hivyo?

  Maandamano ya Ugiriki yaliyodumu kwa zaidi ya mwezi sasa hakuna mtu aliyeuwawa lakini Tanzania ndani ya masaa machache watu wanne wameuwawa na wengi kujeruhiwa. Je siku ikifikia wananchi nao wakawa na silaha siitakuwa vita? Serikali naomba itoe kauli ya kulaani haya yaliyo tokea Songea.

  Nawakilisha
   
Loading...