Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Leo hii Waziri Charles Mwijage kakutana na wamiliki wa Malori yanayosafirisha mizigo kutoka bandarini na kupeleka nje ya nchi na sehemu mbalimbli za ndani ya nchi.
Katika kikao hicho waziri kapokea malalamiko /mawazo kutoka kwa wamiliki hao juu ya kupungua kwa mizigo bandarini na hivyo kuwafanya wafanyabiashara hao wa malori kuwa katika wakati mgumu kutokana na hali hiyo ya kupungua kwa mizigo bandarini.
Sababu zilizotajwa na wafanyabiashara hao ambazo zinapelekea kupungua kwa mizigo bandarini ni pamoja na swala la VAT na sababu nyingine alizotamka waziri ni swala la single customs territory na muda mrefu wa kutoa mizigo bandarini hadi kufikia kipindi cha wiki mbili tofauti na bandari zingine kama Beira ambapo hutumia muda wa siku moja kwa mealezo ya waziri.
Hata hivyo,kilichonishangaza ni Waziri Mwijage kuwataka wamiliki wa malori kuwasilisha malamiko/maoni yao hayo kwa waziri fedha.
Sasa nachojiuliza yeye kama Waziri wa Viwanda na Biashara, kwanini asipokee malalamiko hayo na kuyawasilisha kwa waziri mwenzake au ayawasilishe kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri badala ya kuwataka wamiliki hao wa malori kuwasiliana na waziri wa fedha?
Je,jambo hili si la kupeleka kwenye cabinet?
Wadau,au mimi ndio sielewi?
Baadhi ya matamshi yake utayapata kupitia hii link
>http://bit.ly/2dJPFXf