Hivi hawa mawaziri kwenye cabinet wako huru kutoa mawazo yao?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,888
2,000
Leo hii Waziri Charles Mwijage kakutana na wamiliki wa Malori yanayosafirisha mizigo kutoka bandarini na kupeleka nje ya nchi na sehemu mbalimbli za ndani ya nchi.

Katika kikao hicho waziri kapokea malalamiko /mawazo kutoka kwa wamiliki hao juu ya kupungua kwa mizigo bandarini na hivyo kuwafanya wafanyabiashara hao wa malori kuwa katika wakati mgumu kutokana na hali hiyo ya kupungua kwa mizigo bandarini.

Sababu zilizotajwa na wafanyabiashara hao ambazo zinapelekea kupungua kwa mizigo bandarini ni pamoja na swala la VAT na sababu nyingine alizotamka waziri ni swala la single customs territory na muda mrefu wa kutoa mizigo bandarini hadi kufikia kipindi cha wiki mbili tofauti na bandari zingine kama Beira ambapo hutumia muda wa siku moja kwa mealezo ya waziri.

Hata hivyo,kilichonishangaza ni Waziri Mwijage kuwataka wamiliki wa malori kuwasilisha malamiko/maoni yao hayo kwa waziri fedha.

Sasa nachojiuliza yeye kama Waziri wa Viwanda na Biashara, kwanini asipokee malalamiko hayo na kuyawasilisha kwa waziri mwenzake au ayawasilishe kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri badala ya kuwataka wamiliki hao wa malori kuwasiliana na waziri wa fedha?

Je,jambo hili si la kupeleka kwenye cabinet?

Wadau,au mimi ndio sielewi?

Baadhi ya matamshi yake utayapata kupitia hii link

>http://bit.ly/2dJPFXf
 

nra2303

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
2,779
2,000
Hii inshu ya VAT kwy service za mizigo ya transist linahitaji busara na sio la kulazimisha manake tozo ya kodi ipo kisheria! Waziri alitakiwa kusema ataongea na waziri wa fedha then atarudisha majibu,yeye kaamua kukaapembeni!
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,888
2,000
Hii inshu ya VAT kwy service za mizigo ya transist linahitaji busara na sio la kulazimisha manake tozo ya kodi ipo kisheria! Waziri alitakiwa kusema ataongea na waziri wa fedha then atarudisha majibu,yeye kaamua kukaapembeni!
Cha kujiuliza ni kwanini anaona tabu kulipokea na kuliwasilisha kunakohusika?
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
Watu wanaokuja na sera za kupanda miti, kufukuzana na akina Dr Mwaka and constant new ideas bound to cause 'public nuisance' from ministerial devised agenda unataka kuniambia awana uhuru wa mawazo kweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom