Hivi Hawa Ghasia hajui hili nalo lipo Mahakamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Hawa Ghasia hajui hili nalo lipo Mahakamani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Jul 31, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Yupo TBC 1 jambo Tanzania anazungumzia mgogoro wa walimu. Hawa Ghasi waziri mwenye dhamana ya TAMISEMi leo wanazungumzia jambo mgogoro ambao wakati fulani ulipohusu madaktari wao wenyewe ukiacha JK walidai hawapaswi kuzungumzia jambo kama hilo liliopo mahakamani.Hivi hili la walimu limewagusa sana mkadharau Mahakama!?
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huyo mama tangia akiwa utumishi alikuwa na gasia kweli, hili neno "suala lililopo mahakamani"viongozi wetu wanalitumia vibaya,wengine kuzuiliwa kuliongelea ila wao ruksa.Yana mwisho(Kitabu cha Kuli)
   
 3. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tangu serikali iwafukuze madaktari wakati swala lao lipo mahakamani, mahakama zetu zimejidhihirisha kuwa si muhimili kamili kwa kutoishauri serikali kusitisha uwamuzi huo. Serikali imekuwa ikiingilia sana maswala ya Mahakama na maranyingine kupingana na maamuzi ya mahakama. Tunakumbuka swala la mgombea binafsi jinsi Waziri Mkuu (Mh. Pinda) alivyoliingilia na kutoa uamuzi wa serikali ofauti na Mahakama.

  Tunakumbuka Rais kuongelea swala la Madaktari na kutoa miongozo mablimbali wakati lilikuwa mahakamani, hata hili la walimu hivi sasa IKULU ilitoa tamko kupinga mgomo wa mahakama badala ya Mahakama kitengo cha kazi. Kwa matukio kama haya, wananchi tumekuwa na wasiwasi hata maamuzi ya kisiasa yanayoigusa serikali huwa IKULU ina dectate maamuzi. Mf. swala la kuvuliwa Ubunge Bwa. Lema ambapo sheria aziwani na maamuzi na kusikika tetesi kuwa IKULU imeingilia.

  Pia swala la Mbunge wa Segerea Mh.Makongoro Mahanga, inajulikana wazi hujuma alizofanya lakini POLISI na MAHAKAMA vyote vimesikiliza maelekezo kutoka IKULU. Kwa mambo kama haya, yanapelekea sisi wananchi kutoaiamini tena mihimili yetu na kupelekea kujichukulia maamuzi ambayo tunaona yatatetea haki zetu. Ni vizuri mihimili yote mitatu kuwa na mipaka yake kiutendaji.
   
 4. Tanzania Mpya

  Tanzania Mpya JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 248
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Ktk TBC1 Waziri Ghasia amesema walimu ni kati ta kada zinazolipwa vizuri.
   
 5. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hili limjamaa lina bige ya kinga dhidi ya mahakama.
   
 6. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mahakama inatumika vibaya, inaingiliwa ipo kimya haina nguvu kabisa labda ni kutokana na mfumo wa uteuzi wa majaji hawa wa "voda rusha"
   
Loading...