Hivi hawa Azam TV, Startimes, Zuku na DSTV huwa wanalipa kiasi gani cha fedha kwa filamu moja ya kibongo?

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Jul 2, 2019
895
1,363
Yoyote anayefahamu Azam TV, Startimes, Zuku na DSTV huwa wanalipa kiasi gani cha fedha kwa filamu moja ya kibongo anifahamishe..
 
Nilisikia kwa mdau kutoka kwenye group moja akisema

Huwa wanalipa kati ya TZS 400,000 hadi 1,000,000 kulingana na aina ya movie...
 
Sina uhakika kamili ila najibu kama ambavyo nimekuwa nikiambiwa na watu wamewahi kupekeka filamu.

DSTV - Hawa nasikia ndiyo wanaolipa zaidi kulivyo ving'amuzi vingine. Niliambiwa ni kati ya 1M to 2M kwa movie ila ubora ni kitu kinachozingatiwa sana kwao. Huwa wanachukua movie na kuipitia kisha wanakupa majibu kama itaonyeshwa au lah.Muda wa filamu kukaguliwa huweza kufika hata miezi miwili.

Azam - Nasikia wanalipa kati ya 500k to 700k, lakini pia ukitaka mkataba wa kulipwa kulingana na inavyoonyeshwa basi utalipwa 200k kwa kila itakapooneshwa.

Startimes - Sina hata tetesi kuwa wanalipa sh. Ngapi, kitu pekee ninachokifahamu ni kuwa wao startimes wanazipa kipaumbeleo filamu zilizochezwa kuonyesha mazingira ya asili.

ZUKU - Sina taarifa zozote.

Hizi ni taarifa za kusikia, nakushauri uzidi kukusanya taarifa ili kupata majibu sahihi zaidi.
 
nimetengeneza kwa milion nilipwe laki 5 duh
Soko ni pana boss, wao (mfano Azam tv) wananunua haki ya kuonesha kwenye tv yao tu, bado unakuwa na nafasi ya kuiuza filamu hiyohiyo kwenye tv nyingine na hata kusambaza mitaani so usitegemee wakurudishie mtaji wote uliotumia.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom