Hivi hatuna njia nyingine za kuingiza mapato ya serikali zaidi ya VINYWAJI NA SIGARA

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,889
1,346
Serikali zote zimekua zikiongeza ushuru kwenye vitu viwili mara kwa mara. Bajeti zote utaziona zikiwa zimelenga vinywaji vyote kwa ujumla wake na sigara safari hii wameenda mbali zaidi kumkaba mfanyakazi wa uma na wamemuondolea hata ule msamaha mdogo wa kodi aliokua akiupata endapo ataagiza kitu kima usafiri .

Tukumbuke kwamba vitu hivi ni nadra sana kwa wafanyakazi mishahara yetu haitoshi hata mahitaji muhimu tu ya kawaida achiilia mbali hizo habari nyingine .

Mi naona serikali yetu haina jipya zaidi ya mambo yale yale ya waliopita na mbaya zaidi hawa
wanaharibu zaidi. Bajeti ambazo tunawekeza kwenye matumizi na wala si kwenye uwekezaji hizi hazitufai hata kidogo.
 
Inashangaza, walevi na wavuta fegi ndiyo wanaotegemewa na taifa katika uendeshaji wa shughuli za serikali na maendeleo!
 
Siku wapiga laga na wazee wa gari moshi wakipiga kunji, Taifa litaingia ktk janga kubwa. putting all eggs in one basket ndo mwendo wetu waTZ. Migodi inatema kila kukicha and they get away with it, wa laga na moshi wanasulubiwa kila uchao!
 
Hii serikali ya magamba tumeichoka,kila bajeti hakuna jipya,migodi ya madini inaachwa badala ya kukamuliwa kodi serikali inategemea pombe na sigara.Dawa ya haya yote ni kuikataa serikali ya CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
 
Tuanzishe chama cha wanywaji na wavutaji halafu tuitishe mgomo nchi nzima. Kwa mwezi mmoja wanywe mawaziri na wabunge ili serikali iache tabia ya kuendesha nchi kwa kuwatumia wanywaji
 
bula sisi nchi haiendi (walevi, wanywaji na wavutaji)
 
Gizlenen-Sigara-Gercegi-Nedir.jpg
 
Ewe Mtanzania mwenzangu ongeza speed ya kunywa uchangie pato la taifa!
4.jpg
 

OMBI; Serikali ya kikwete ihalalishe hii kitu kuinua uchumi wa ndani na kuwawezesha mama zetu!
 
Tutajie kabisa tarehe ya kuanza mgomo tulianzishe au wadau mnasemaje?:A S crown-2:
Tuanzishe chama cha wanywaji na wavutaji halafu tuitishe mgomo nchi nzima. Kwa mwezi mmoja wanywe mawaziri na wabunge ili serikali iache tabia ya kuendesha nchi kwa kuwatumia wanywaji
 
lakini bado serikali haijatutajia gharama inazotumia kutibu magonjwa yanayotokana na madhara ya sigara na pombe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom