Hivi Hapa KIKWETE ana maana gani. WHERE IS TAKUKURU? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Hapa KIKWETE ana maana gani. WHERE IS TAKUKURU?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Profesy, Sep 28, 2010.

 1. Profesy

  Profesy Verified User

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  source - Habari Leo

  Kikwete aahidi kutokomeza malaria kwa kuua mbu kila nyumba

  Imeandikwa na Mgaya Kingoba, Musoma;
  Tarehe: 26th September 2010

  MKOA wa Mara utaanza kampeni ya kunyunyizia dawa ya kuua mbu katika nyumba zake zote kuanzia Oktoba mosi, mwaka huu katika jitihada za serikali kupambana na ugonjwa wa malaria unaoua watu wengi nchini.

  Akizungumza katika mkutano mkubwa wa kampeni za uchaguzi mkuu juzi kwenye Uwanja wa Mukendo mjini hapa, mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema kazi kama hiyo imekwisha kamilika mkoani Kagera.


  Alisema kupulizia dawa hiyo ni moja ya jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo, baada ya kutoa pia vyandarua vya hati punguzo kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.


  "Tulianza kampeni ya kunyunyizia dawa za kuua mbu katika Mkoa wa Kagera na tumerudia mara ya pili…sasa kuanzia Oktoba mosi tunaanza Mkoa wa Mara na kila nyumba itapuliziwa dawa," alisema Rais Kikwete.


  Alisema nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015, Tanzania itatangaza kuwa imetokomeza ugonjwa huo, hasa Tanzania Bara baada ya Tanzania Zanzibar kutokomeza ugonjwa huo.


  Alieleza kuwa mipango mingine ya serikali ni kujenga kiwanda cha dawa za kuua viluwiluwi wa mbu kwa msaada wa Serikali ya Cuba ili kukabili ugonjwa huo unaoua Watanzania wengi hasa wajawazito na watoto.


  Katika masuala mengine, aliwahakikishia wananchi wa Musoma Mjini kwamba Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa itajengwa licha ya kusuasua kwa mpango huo kwa ushirikiano na Kanisa Katoliki, na mzigo huo sasa utabebwa na serikali.


  Kuhusu kiwanda cha nguo cha Mutex, aliuagiza uongozi wa Mkoa kufuatilia na kujua nini kimesababisha mwekezaji aliyepewa kiwanda hicho kushindwa kukifufua, na hivyo serikali ifanye jitihada za kukifufua.


  Aliahidi kuwa barabara za Musoma Mjini zitawekwa lami; kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama na upatikanaji wa dawa hospitalini.


  PS - ALIKUA WAPI MIAKA YOTE MITANO YALIOPITA SAA HIZI NDIO ANAAMUA KUFANYA HIVI?
   
 2. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ameshaahidi kutoa ahadi zaidi, achana naye
   
 3. Profesy

  Profesy Verified User

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yani...
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Anaongea as if ana serikali tayari. Hii si kamapeni ya kuomba kuura jamani Au
   
 5. Profesy

  Profesy Verified User

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  alafu TAKUKURU wanatutumia SMS eti tutoe report ya ufisadi. Hivi hii hapa sio wazi wazi ufisadi?:confused2:
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  JK asimsahau Malaria Sugu wa humu ndani!!

  Tehe tehe tehe!!!!!
   
 7. Profesy

  Profesy Verified User

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yes yes
   
 8. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kwa kasi zaidi na nguvu zaidi....:becky:
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mi ndio maana nampongeza sana Mkapa kutompigia kampeni huyu JK maana anajua atajiabisha kwa midubwana anayoropoka ropoka wakati sheria kaishaini mwenyewe kwa mbwembwe na mabiriani watu wakala pale ikulu kisha kucheza kiduku!!! nchi haina rais hata kidogo
   
 10. Profesy

  Profesy Verified User

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hamna Rais.
   
 11. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Rais wetu kweli hamnazo. Kichwani ni wazi tu, hamna ubongo
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Anaahidi kanakwamba hakuwepo madarakani bwana!
   
 13. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #13
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi sheria ya gharama za uchaguzi haipo tena?
   
 14. Profesy

  Profesy Verified User

  #14
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Takukuru wenyewe wamepotea kudadeki
   
 15. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tumemuzoea huyo lkn mwaka huu tunaye...Slaa 2010 mpaka 2020,yes ataweza..
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  inawezekana!
   
 17. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Ahadi ahadi ahadi............................!!!
   
 18. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa Mfano TAKUKURU Wakipewa kitu kidogo, Mtafanyaje?:confused2:
   
 19. Profesy

  Profesy Verified User

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Good question.
   
Loading...