Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,797
- 71,214
Maana halisi ya CCM kumuita Magufuli "Rais wa wanyonge" ni kumpamba kuwa eti ni wa wafanyakazi, wakulima,wavuvi na wafugaji.
Mbunge Bwege amezungumza bungeni kuwa makundi hayo yote yameguswa na dhiki zilizoletwa na CCM hasa awamu hii ya tano na hawatatoa kura tena kwa malaghai jee hali iko hivyo kwa eneo lako means JF?
Huku kwetu makundi yote yameguswa mfano;
Wafanyakazi, hakuna increments toka 2015 ambayo iko kisheria wala nyongeza za mishahara wakati bei za mahitaji zinapanda.
Wakulima, hao ndio usiseme kabisa kwani mazao ya biashara kama Korosho, pamba, tumbaku nk serikali imeyaua kwa ubishi na ujinga.
Wavuvi, wamewekewa sheria za ajabu mpaka hiyo shughuli wanaiacha. Kuna nyavu zinaingizwa nchi na kulipiwa kodi lakini mvuvi akinunua avulie ndio inakula kwake na jela inaweza isimkose.
Wafanyabiashara, nao wameyumbishwa kufikia kuamua biashara kuzifunga na wale wenye mitaji mikubwa kuhamishia nje ya nchi.
Sasa kama maana JF na huko unako ishi mambo ni haya haya hizo kura za "wanyonge" watazipatia wapi?
Tegemeo la Wakurugenzi (returning officers) nalo mahakama imemwagia mchanga kitumbua hicho, CCM na Mzee baba wataponea wapi?
Ila ili mbuyu kuuangusha inapaswa kunoa mashoka vizuri