Hivi hakuna watu makini ndani ya CCM wakujadiliwa nafasi ya Urais hapa JF?

Mwamba Usemao Kweli

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
744
186
Inasikitisha sana kuona ndani ya jf hakuna watanzania makini wa kujadiliwa katika tasnia ya uongozi wa juu wa nchi yetu kwa mustakabali wa taifa letu.


Bali tumekuwa tukiletewa baadhi ya wana ccm waliojidhihirisha kwa matendo, tabia na hulka zao kuwa ni mafisadi na wezi wa rasilimali za taifa letu kuwa wanafaa kwa nafasi ya urais mwaka 2015. Si hivyo tu bali kwa njia moja au nyengine watu hawa tunaoletewa hapa janvini wamechangia kudhoofisha kwa makusudi juhudi za watanzania waliowengi kujikwamua kutoka katika lindi la umaskini kwa maslahi binafsi.

Kumbukeni kashfa zifuatazo ambazo leo wahusika wanajitanabahisha ndani ya CCM kuwa iko tayari kuwapa uraisi: -

1. EPA.
2. Meremeta.
3. Mwananchi gold.
4. Ununuzi wa rada kwa bei mara 3 ya bei halisi.
5. Ununuzi wa ndege ya raisi kwa bei mara 3 ya bei halisi.
6. Deep green.
7. Ujensi wa benki kuu kwa garama kubwa zaidi duniani kuliko benki kuu yoyote.
8. Kubinafsisha na kuuza viwanda na makampuni ya umma kwa bei ya kutupa.
9. Richmond & Dowans.
10. Umiliki wa migodi ya madini na mikataba ya hovyo isiyoleta tija kiuchumi TZ.
11. Umiliki mbovu wa viwanja vya michezo na sehemu za wazi na kupelekea ujenzi holela mijini na ukosefu wa mipango miji bora.
12. Uuzwaji wa nyumba za umma kwa manufaa ya wachache
13. Kupandisha bei za umeme na uunganishaji wake kiholela kwa manufaa ya wachache
14. Kupandisha garama za ujenzi wa minudombinu ya barabara kwa asilimia 300 kwa manufaa ya wachache.
15. Kubinafsisha reli kwa kampuni ya India (RITES) ilioshindwa kutoa huduma bora.
16. ATC kuuzwa na kuididimiza kiuchumi na ki-huduma
17. Kushindwa kukusanya kodi toka kwa wawekezaji kuboresha maisha ya watanzania.

Kashafa hizi zimechangia sana kuzorotesha uchumi wa taifa letu na kupelekea kukuza umaskini kwa fedha zake kupotea bila kuchangia upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa watanzania.

Nawasihi sana wana jf tujitahidi sana katika dhama hizi ambapo taifa letu limekumbwa na wimbi la wana siasa tumbo kuepuka kuendelea kuwakandamiza watanzania wenzetu kwa kutumia mitandao kama JF kuwalisha uongo na uzandiki wa kuwapigia debe na kuwauza kwa sifa za kupika kwa namna yeyote ile wanasiasa walioshindwa na ambao kwao wamebaki kutumia fedha kujitangaza na kufanya kampeni makanisani na kwenye harambee za kuchangia maendeleo ya taifa letu kuwa wao ndio wanaokubalika na wanafaa kutuongoza.

Ni vema mkafahamu kuwa ni sisi wachache ndani ya taifa letu kwa uewelewa wetu ndo tunaweza kulikomboa taifa letu kutoka katika mikono ya walafi wachache waliozorotesha kwa makusudi huduma za umma katika kupata: -

1. Maji safi si mijini tu hadi vijijini.
2. Elimu bora na bure bila kulipia kote nchini.
3. Afya na matibabu bora bila kulipia.
4. Ajira kwa vijana wetu.
5. Pembejeo kwa wakati bila kutumia gharama kubwa.
6. Ununuzi wa mazao kwa wakati na kwa bei bora kutoka kwa mkulima bila kumdhulumu.
7. Haki mahakamani, polisi na sehemu nyenginezo za umma.
8. Haki katika matumizi ya ardhi vijijini na maeneo yenye rasilimali za madini.

Ni vema tuwakatae watu hawa ambao wamekuwa chimbuko la kuangamiza utaifa wetu na rasilimali za taifa letu. Tuwakatae kwa sauti moja kuwa hawatufai na tuwaogope kama ukoma.

Nawaombeni sana wanaJF mtuletee watanzania wengine tuwajadili wenye mvuto na walio tayari kuwatumikia watanzania wasio na kashfa za ufisadi wenye uadilifu na walio tayari bila kuchoka kuwaondolea watanzania umaskini uliopindukia huko mijini na vijijini.

Nawasilisha kwenu JF kwa manufaa ya taifa letu. Tujaribu kujadili majina kama hapa chini: -

1. Dr. Mwakyembe
2. Dr. Magufuli
3. Balozi Kagasheki
4. Prof. Muhongo
5. Nahodha

Na si kutuletea majina ya watu kama vile: -

1. Lowasa
2. Chenge
3. Ngeleja

Hawa walishashindwa katika nafasi za utendaji za uwaziri na uwaziri mkuu bado mnataka eti wawe rais na mnakaa kabisa na kujadili hapa jukwaani huku mate yakiwatoka kuwa eti washikiki ndani ya CCM. Eti hawana upinzani.

ACHENI HIZO.
 
Naunga mkono hoja ila ktk Orodha yako itakuwa afya kwetu Ukiwachinjia baharini Shamsi Nahodha na Hamisi Kagasheki hawa ni kwamba ni hawajitambui..wa kuagizwa tu
 
Wacha wafu wazike wafu wenzao.
Hamna kitu hapo wote hata kama si mafisadi hakuna rais material hapo
 
T atizo si watu tatizo ni mfumo wa uongozi wa nchi yetu; hata ukimweka MwakyeMbe awe Rais bila kubadilisha mfumo ni kazi bure; lazima atakwama tu wakati anatimiza majukumu yake na ndiyo maana unaona watu wanaharibu haribu uongiz1 wizarani lakini wamegoma kuwajibika - tusiwalaumu wao hapana bali ni mfumo unawaruhusu. Cha maana watanzania ni kubadili kabisa huu mfumo uliopo sasa tukitaka kulinusuru taifa letu.
 
Mada nzuri sana mtoa mada ila ilibdi upanue wigo yaani tujadili watu na sio wa chama Fulani peke yake. Hivyo namuongeza Dr. Slaa, Tundu Lissu na John Mnyika. Tukishawajadili waandaliwe mdahahalo tuone nani ana uelewa wa mambo ya kitaifa na kimataifa
 
Mada nzuri sana mtoa mada ila ilibdi upanue wigo yaani tujadili watu na sio wa chama Fulani peke yake. Hivyo namuongeza Dr. Slaa, Tundu Lissu na John Mnyika. Tukishawajadili waandaliwe mdahahalo tuone nani ana uelewa wa mambo ya kitaifa na kimataifa
wewe ukitaka kuwatoa nduki CCM, taja mdahalo.
 
Japo umeanza vizuri lakini umemaliza vibaya sana , kwa sisi watu wa KUSINI kutuwekea jina la SOSPETER MUHONGO ni sawa na kutuwekea chumvi kwenye Donda kuubwa sana ! Kingine ni kwamba hawa vijana wengi wanaoleta porojo za Mafisadi humu Jf wanatumika ! Wako kazini , wanaishi hivyo , kwa kila uzushi unaouona humu wanalipwa ! Haya Mapovu wanayotoa si bure ! Shortly ni kwamba Njaa ndiyo inayodhalilisha chama chako ! Hata hivyo ndani ya CCM kumpata Msafi ni kazi ngumu mno ! Ni heri hata kuhubiri injili kwenye kundi la walevi kuliko kumsaka msafi ccm !
 
Huyu jamii wa umasaini anaumiza vichwa vya watu. Ana sifa mojaa kubwaaa ambayo viongoz wengine wanashindwa. ALIJIUZURU hii inampa maujiko jamaa. Ufisadiii wahusika wapo hakutaka kuwataja tu.
 
Kama unamuona mtu hafai basi waachie watanzania ndio waamuzi na kama unamuona fulani anafaa waachie watanzania pia!!kama hafai anakuumizaje kichwa!!mtoa mada kama unawashwa kujikuna ruksa!!
 
Siamini kama umeliacha jina la dr saliam ahmed salim huyo tu ndio anafaa ndani ya ccm kashfa zote ulizozitaja hapo juu hahusiki hata moja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom