Hivi hakuna wanasheria wa kufungua kesi ya zuio la uchaguzi wa marudio Jimboni kwa Tundu Lissu?

Jamani haya ni mambo ya kisheria!
Sasa bila tangazo la NEC unafungua shtaka gani?
Hutakiwi kulipa chochote unapo enda Mahakamani kulinda ubunge wako!
Hapo unazuia uchaguzi mpaka kesi ya msingi iishe
Utalazimika kuweka deposit ili ukishindwa kesi itumike kugharamia kesi
Watu walikua wanaweka mapingamizi tu kupoteza muda
 
Ni lazima uwe na standing mbele ya Mahakama. Binafsi naamini ukimuondoa Lissu mwenyewe mtu mwingine kwenye hii "locus standi" Ni CHADEMA. Itashangaza kama hawatafungua kesi. Lengo hata like kuchelewesha hadi muda ufike ambao unazuia kufanyika uchaguzi ndogo. HINT: Sababu ya kumvua ubunge Lissu na kutangaza uchaguzi ndogo haraka hivi.
Mkuu siku hizi mahakama za Tanzania huwa hazichelewi,na serikali haijawahi kushindwa mahakamani tokea Magufuli aingie,'sijui kwa nini!'
 
Kwani ile TLS yao haiwezi?

Manake wakiwaga na kale kauchaguzi kao huwa wanapiga sana kelele humu hao makamanda....

Wanaye shangazi yao yule....kuna yule Kibatala sijui....na wengineo wasomi wasomi.

Wote hao hawawezi kufungia hilo shauri?
Nyani
 
Hapo unazuia uchaguzi mpaka kesi ya msingi iishe
Utalazimika kuweka deposit ili ukishindwa kesi itumike kugharamia kesi
Watu walikua wanaweka mapingamizi tu kupoteza muda
Nadhani unachanganya mambo,hii sio kesi ya uchaguzi
Ni kesi ya Mh Lissu ya kupinga kutenguliwa ubunge wake
Hakuna hata senti unayo takiwa uiweke kama deposit
Mbunge wa Arumeru Nasari alipo enda Mahakama kuu kuomba kusimamisha uchaguzi usifanyike Jimboni kwake hadi kesi yake ya msingi iishe alilipa bei gani?
Mbona Mahakama Kuu Dodoma ilisimamisha uchaguzi hadi kesi yake ilipo isha na akashindwa kesi na hakulipa chochote?
Anyway,haya ni mambo ya kisheria!

NB:Week hii case ya Lissu inafunguliwa
 
Back
Top Bottom