Hivi hakuna wanasheria wa kufungua kesi ya zuio la uchaguzi wa marudio Jimboni kwa Tundu Lissu?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,418
2,000
Siwezi kuita watanzania wengine mabedui kwa sababu tu sikubaliani nao kiitikadi. Ila kwenye katiba kifungu cha 71 ambacho Ndungai alitumia kifungu kidogo cha kwanza sehemu za (c) na (g) kufuta ubunge wa Lissu, kifungu kidogo chake cha pili kinaweka wazi kuwa Bunge litakuwa na utaratibu wa mbunge kujitetea asivuliwe ubunge wake. Leo nilijaribu kupitia sheria kadhaa za Tanzania kuangalia kama kuna sheria inayotamka utaratibu huo sikuiona. Ila katiba ilitegemea kuwa mtu anayevuliwa ubunge ana haki ya kujitetea mahakamani kisheria. Nasari alijitetea mahakamani lakini utetezi wake ukashindwa kukidhi sheria mbele ya mahakama.
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,741
2,000
Hahaha mpingaji ni mbunge aliyevuliwa ubunge, ambaye wanadai hajulikani yuko wapi. Atakapo rudi nchini, jimbo linakua na mbunge tayari, sasa inakuwa sarakasi, hawezi kumpinga aliyeteuliwa na kupitishwa na tume ya uchaguzi, katiba inasema hao ndio wa juu kimamlaka kumtangaza wanayemtaka. Kwanza atakuwa na kesi nyingi sana hata huo ubunge hatoweza kuuhudumia, wacha apewe mwingine. Atapita bila kupingwa, na ndiyo style ya chaguzi za awamu hii.
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,725
2,000
Makonda hana akili. Anabebwa tu.

Pasi kubebwa, hawezi simama kwa miguu yake mwenyewe!
Sasa hivi amerukia kupanga safu ya wachezaji wa Taifa stars.
Nimemsikia akitoa amri kwa wachezaji wa stars wanaotaka kustaafu kucheza kuwa hataki kusikia hilo.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
9,894
2,000
Siwezi kuita watanzania wengine mabedui kwa sababu tu sikubaliani nao kiitikadi. Ila kwenye katiba kifungu cha 71 ambacho Ndungai alitumia kifungu kidogo cha kwanza sehemu ya (c) ma (g) kufuta ubuinge wa Lissu, kifungu kidogo cha pili kiliweka kuwa Bunge litakuwa na utrataibu wa mbunge kujitetea asivuliwe ubunge wake. Leo nilijaribu kupitia sheria kadhaa za Tanzania kuangalia kama kuna sheria inayotamka utaratibu huo sikuina. Ila katiba ilitegemea kuwa mtu anayevuliwa ubunge ana haki ya kujitetea mahakamani kisheria. Nasari alijitetea mahakani lakini utetezi wake ukashindwa kikidhi sheraia mbele ya mahakama.
Na hakuna chochote katika katiba hiyo kinachowazungumzia wananchi kuhusu mbunge wao?
Hawana nafasi kabisa ya kutetea uamzi wao juu ya mbunge waliyemchagua, halafu hata hawashirikishwi wakati anapoundiwa mizwengwe ya kuondolewa katika uwakilishi wao?

"Siwezi kuita watanzania wengine mabedui kwa sababu tu sikubaliani nao kiitikadi."
Maamzi yanayofanywa kama hayo yaliyofanyika kwa kumwengua Lissu kutoka katika ubunge, siwezi kuuita "kutokubaliana kiitikadi."
Uamzi huu sio wa kiitikadi. Ni uamzi wa 'chuki', na mTanzania anayeonyesha chuki kwa waTanzanaia wenzake, hata hilo jina la 'bedui' ni la kumpa heshima isiyostahili.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
9,894
2,000
Zuio la kimahakama ni muhimu kwa hawa mabedui.
Wakati mwingine hata mtu unaweza kutamani na kuomba muujiza utokee!

Mathalan, hivi itakuwaje/ingekuwaje kwa umoja wao wapiga kura wa jimbo wakasimama kwa umoja wao, umoja wao wa ubinaadam zaidi kuliko maslahi ya vyama vya siasa. Wakasimama na kupaaza sauti moja kwamba Jimboni kwao hapafanyiki uchaguzi wa marudio; na kwamba mbunge pekee wanayemtambua ni huyo aliyelazimishwa, bila utashi wake kutokuwepo na kuwawakilisha wakati wote huu.
Na kwa vile mbunge wao amekwishatangaza kwamba anarudi karibuni, hawaoni sababu ya mbunge huyo kuenguliwa katika uwakilishi.

Huu ndio kama muujiza ambao ungependeza wananchi wakauonyesha kama mfano kwa kukataa kuendeshwa kama mkokoteni na viongozi hawa wasiokuwa na sifa za uongozi.

Hili lingependeza sana, na lingekuwa mfano mzuri wa kuigwa na kuanza kuwatia akili hawa wanaojiona maamzi yao ndio kila kitu, bila ya kujali maslahi ya watu wanaohusika moja kwa moja. ambao ndio wanao athiriwa na maamzi yao mabaya.
 
Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,425
2,000
Hahaha mpingaji ni mbunge aliyevuliwa ubunge, ambaye wanadai hajulikani yuko wapi. Atakapo rudi nchini, jimbo linakua na mbunge tayari, sasa inakuwa sarakasi, hawezi kumpinga aliyeteuliwa na kupitishwa na tume ya uchaguzi, katiba inasema hao ndio wa juu kimamlaka kumtangaza wanayemtaka. Kwanza atakuwa na kesi nyingi sana hata huo ubunge hatoweza kuuhudumia, wacha apewe mwingine. Atapita bila kupingwa, na ndiyo style ya chaguzi za awamu hii.
Umekosea mkuu...uchaguzi ambao aupingwi mahakamani ni wa Rais tu basi
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
10,741
2,000
Kwani ile TLS yao haiwezi?

Manake wakiwaga na kale kauchaguzi kao huwa wanapiga sana kelele humu hao makamanda....

Wanaye shangazi yao yule....kuna yule Kibatala sijui....na wengineo wasomi wasomi.

Wote hao hawawezi kufungia hilo shauri?
Mimi navyojua TLS haipo kwa ajili ya Chadema wala haipo kutetea maslahi ya Chadema au kikundi Fulani cha jamii. TLS ni kwa ajili ya Watanganyika wote bila kujali itikadi. Maana yake Chadema kutumia mawakili ambao ni wanachama wa TLS haina maana Chadema wanaitumia TLS.
 
Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,116
2,000
Kwani ile TLS yao haiwezi?

Manake wakiwaga na kale kauchaguzi kao huwa wanapiga sana kelele humu hao makamanda....

Wanaye shangazi yao yule....kuna yule Kibatala sijui....na wengineo wasomi wasomi.

Wote hao hawawezi kufungia hilo shauri?
Siku hizi hata lugha zako zimefanana na yule nduli/shetani wa Chattle!
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,504
2,000
Ingependeza sana lakini nani hapo jimboni mwenye ujasiri wa kulianzisha hilo?
Wakati mwingine hata mtu unaweza kutamani na kuomba muujiza utokee!

Mathalan, hivi itakuwaje/ingekuwaje kwa umoja wao wapiga kura wa jimbo wakasimama kwa umoja wao, umoja wao wa ubinaadam zaidi kuliko maslahi ya vyama vya siasa. Wakasimama na kupaaza sauti moja kwamba Jimboni kwao hapafanyiki uchaguzi wa marudio; na kwamba mbunge pekee wanayemtambua ni huyo aliyelazimishwa, bila utashi wake kutokuwepo na kuwawakilisha wakati wote huu.
Na kwa vile mbunge wao amekwishatangaza kwamba anarudi karibuni, hawaoni sababu ya mbunge huyo kuenguliwa katika uwakilishi.

Huu ndio kama muujiza ambao ungependeza wananchi wakauonyesha kama mfano kwa kukataa kuendeshwa kama mkokoteni na viongozi hawa wasiokuwa na sifa za uongozi.

Hili lingependeza sana, na lingekuwa mfano mzuri wa kuigwa na kuanza kuwatia akili hawa wanaojiona maamzi yao ndio kila kitu, bila ya kujali maslahi ya watu wanaohusika moja kwa moja. ambao ndio wanao athiriwa na maamzi yao mabaya.
 
Emery Paper

JF-Expert Member
Jun 1, 2019
1,415
2,000
TLS ni CHADEMA, point blank, period dot com.
Umetumia vigezo gani mkuu kufikia hilo hitimisho ? Wakili hana chama bali ana wateja. Na sifa ya wakili ni kuhakikisha/kutetea haki itendeke.TLS kuwa na wanachama wawili au watatu wanaotumiwa sana katika kesi za Chadema hakuifanyi TLS kuwa Chadema.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,944
2,000
Zuio la kimahakama ni muhimu kwa hawa mabedui.
Kwa kigezo kipi?
Acha mihemko,unajua sheria kuliko Fatuma karume,kibatala?hujiulizi kwa nini wapo kimya?
Lissu akihojiwa na Bbc amekiri kwamba hakumtaarifu spika maendeleo ya afya yake wala sehemu alipo
Spika katika taarifa yake ameonesha vifungu vya kanuni vilivyomtimua lissu
Kufungua kesi itakua ni kupoteza muda na pesa,hawatashinda
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,922
2,000
Chadema si impitishe tena agombee!

Wana Singida Mashariki wamekuwa kama Yatima acheni wapate mwakilishi sasa na Mh. Tundu aendelee na mchakato wa kupigania Afya yake
 
nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,195
2,000
Sio awamu hii aisee. Tuna siraha zipo tu hazitumiki. Tutazitumia kuzuia hayo maandamano sijui mnaita mapingano
Wakati mwingine hata mtu unaweza kutamani na kuomba muujiza utokee!

Mathalan, hivi itakuwaje/ingekuwaje kwa umoja wao wapiga kura wa jimbo wakasimama kwa umoja wao, umoja wao wa ubinaadam zaidi kuliko maslahi ya vyama vya siasa. Wakasimama na kupaaza sauti moja kwamba Jimboni kwao hapafanyiki uchaguzi wa marudio; na kwamba mbunge pekee wanayemtambua ni huyo aliyelazimishwa, bila utashi wake kutokuwepo na kuwawakilisha wakati wote huu.
Na kwa vile mbunge wao amekwishatangaza kwamba anarudi karibuni, hawaoni sababu ya mbunge huyo kuenguliwa katika uwakilishi.

Huu ndio kama muujiza ambao ungependeza wananchi wakauonyesha kama mfano kwa kukataa kuendeshwa kama mkokoteni na viongozi hawa wasiokuwa na sifa za uongozi.

Hili lingependeza sana, na lingekuwa mfano mzuri wa kuigwa na kuanza kuwatia akili hawa wanaojiona maamzi yao ndio kila kitu, bila ya kujali maslahi ya watu wanaohusika moja kwa moja. ambao ndio wanao athiriwa na maamzi yao mabaya.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,944
2,000
Uchaguzi utazuiwa hadi kesi ya msingi iishe!
Usiwe na wasi wasi kwa hilo!
Hujui sheria wewe
Walutakiwa wawahi kabla tume haijatangaza tarehe
Kwa sasa wakiomba zuio,tume itaomba mlalamikaji aweke cash depositi walau 50% ya gharama za kuandaa uchaguzi au jaji anaweza kupunguza.wakiambiwa waweke bilioni mezani watakimbia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom