Hivi hakuna teknolojia ya kuyavuna maji yasilete madhara kwa jamii?

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,023
1,315
2f5a230d31f7971a3eebc34918646f55.jpg
 
Nchi ya Singapore wanavuna maji ya mvua na maji taka kurudisha kwenye mfumo wa uzalishaji na usambazaji maji. Hii inasaidia kupunguza mafuriko na kusaidia kwenye utunzaji wa vyanzo vya maji. Mvua ikinyesha maji yanaingia kwenye mifereji ya mvua na kwenda kwenye mitambo yao ya usafishaji na kuwekwa dawa kisha kurudishwa viwandani na mashambani kwa matumizi mengine. Maji ya vyoo huingia kwenye mitambo mingine na kutengenezewa maji ya chupa na viwandani pia
 
Huko ni duniani
 
Tenolojia ta uvunaji maji hipo kama,nchi ikiamia kuwekeza lakin kwa serikali hii siyo kipaumbele
Pia wataalamu wa masuala hayo wanazalishwa kila mwaka kwaenye vyuo vya hapahapa tz.
Naushauri gov't iwatumie wataalamu hawa wasaifue maduala haya kwrnye maeneo yenye mvua chache kama same dc, lindi, na baadhi ya maeneo yenyeshida ya maji kama morogoro, dom, singida na kwingineko lakini sijuhi kama siku hizi wanapangiwa cha kufanya au kushauriwa
 
Kuvuna maji sidhani kama ni swala la teknolojia bali ni gharama tu za kujenga mabwawa na mitaro ya kuyaelekeza hayo maji kwenda kwenye mabwawa husika halafu yaje kutumika katika kipindi cha kiangazi kwa matumizi mbalimbali.
 
Mkuu kuna mafuriko mengine hayazuiliki. Huko duniani napo huwa kuna mafuriko ya kufa mtu,pamoja na kwamba wanamifumo mizuri ya maji taka
Tenolojia ta uvunaji maji hipo kama,nchi ikiamia kuwekeza lakin kwa serikali hii siyo kipaumbele
Pia wataalamu wa masuala hayo wanazalishwa kila mwaka kwaenye vyuo vya hapahapa tz.
Naushauri gov't iwatumie wataalamu hawa wasaifue maduala haya kwrnye maeneo yenye mvua chache kama same dc, lindi, na baadhi ya maeneo yenyeshida ya maji kama morogoro, dom, singida na kwingineko lakini sijuhi kama siku hizi wanapangiwa cha kufanya au kushauriwa
 
Mafuriko kwetu chanzo chake kikubwa ni uharibifu wa mazingira (kulima kwenye miinuko, na pembeni ya mto) Mvua inaponyesha, maji yanatiririka yakiwa na udongo ambao unazoa miti na taka nyingine. Maji pekee bila udongo yakipita juu ya daraja hayalibomoi. Lakini kama kuna miti, mawe na taka nyingine zinajikita kwenye daraja na mwisho kuling'oa. Kama serikali ikiamua kwa dhati, ikishirikisha wananchi, mabwawa yanaweza kuchimbwa na kukusanya maji ya mvua. Kama uharibifu wa mazingira utadhibitiwa, mafuriko yatadhibitiwa na wananchi kupata maji ya kunyeshea siku za baadaye
 
TUWAULIZE WALE WANAFUNZI WA DIT,MUST NA CHUO CHA MAJI LABDA

Hapa ntasimama kama mwanafunzj Wa DIT na Chuo cha maji,........Teknolojia IPO tu, ila ujenzi Wa hzo miundo mbinu gharama zake si za mchezo....

Haya maji yanaweza kutumika kwa kilimo cha umwagiliaji pale mvua ikikata hasa wakati Wa ukame katika eneo husika
 
Nashukuru kwa kujitokeza wewe mwanafunzi ila nikwambie tu kwa upande wa gharama si kubwa na wala hazitushindi pengine uniambie tu udhati wa kulichukulia hili swala kitaalamu lisiingiliwe na siasa pia na wataalamu wetu kuifanya hiyo kazi kiweledi. Mfano hebu niambie gharama ya kununua Gx Vx au Gx Tx mpyaa ni sh ngapi, halafu linganisha na hizo gharama
 
Mkuu kuna mafuriko mengine hayazuiliki. Huko duniani napo huwa kuna mafuriko ya kufa mtu,pamoja na kwamba wanamifumo mizuri ya maji taka
Ila hapa Dar ni mvua tu ya masaa machache inaleta kero ambapo kungekuwa na drainage system ya kueleweka wala tusingeona haya madhara.
 
Back
Top Bottom