Hivi hakuna njia nyingine ya kupunguza Vitambi/Mafuta mwilini?

Wataalam
Nimekuwa nikijiuliza hivi imeshindikana kweli kufanya surgery ya kuondoa mafuta toka kwenye tumbo? mi naona jinsi yalivyojirundika sehemu moja tumboni kama mnavyotuaminisha kupitia michoro yenu nk ni kazi rahisi zaidi kama imewezekana kuzalisha mwanamke kwa kisu? badala ya sijui kukata utumbo nk???au kuna kitu sijui hapa wataalam?
Nimehangaika sana kupunguza kitambi changu lakini sasa nimekata tamaa baada ya kubugia madawa mbalimbali ya kienyeji,herbal,food suplements , diet,kuacha kula wanga,mafuta ,sukari na nyama nyekundu......Yote haya nimefanya lakini wapi......yaani kuna madawa nikinywa naharisha mafuta mpaka nasikia kizunguzungu...lakini kitambi kinabaki pale pale hata sijui yale mafuta huwa yanapungua kutokeaga wapi.....hii ni pamoja na kufanya mazoezi mepesi.......nilichoshindwa kuacha ni pombe kali - Vodka.....lakini nimejitahidi sana kuacha mavyakula ya ajabu ajabu hasa usiku...lakini wapi.......??...Ttizo kila mtaalam wa mitishamba anakwambia dawa yake ni kiboko lakini wapi! ...nina mwaka wa tano sasa nahangaika na hili tumbo linanyima sana raha wakuu.....
Napokea ushauri wa kitaalam wa aina zote
Asanteni
Acha kunywa Pombe huo ndo ushauri wangu mna mnywaji pombe humfanya awe na kitambi
 
Wengi wenye vitambi Ni walafi mno.
Asilimia kubwa Ni wapenzi wa kula viporo.

Kiporo hakijawahi muacha mtu salama.

Chunguza hata watoto wadogo wa vijijini wanafakamia viporo,
Wanavitambi utadhani watu wazima.
Vijijiji watu Wana shida za unyafuzi
 
Plunking ndo nn mkuu, naomba Elimu🤝
Anamaanisha Plank, aina ya zoezi, ila zoezi hili haliwezi kuondoa kitambi, hauwezi kupunguza mafuta kwa kufanya spot reduction kama niliivyoeleza hii ni myth. Sio zoezi baya kujenga misuli ya core kwa ujumla ila pia ni advanced kidogo.

 
Tatizo kubwa la sisi watz ni kurahisisha Mambo haswa mtu atakuambia kupunguza kitambi mbona ni simpo Sana fanya skwashi itapunguza kitambi chako ..mwingine kunywa maji ya Moto...lakini hivyo vyote ni uwongo mkubwa kabisa .haiwezekani ukafanya mazoezi ya kupunguza sehemu moja ya mwili alafu sehemu nyingine zibaki Kama zilivyo huu ni uwongo wa Karne ...hoja ni rahisi tu kitambi huwa kinapungua pale ambapo mwili wote upungua ... Maana yake kwamba unapopunguza uzito wa mwili na sehemu ya tumbo inapungua so ukitaka kupunguza kitambi inabidi utengeneze programu ya kupunguza body weight...lakini ukisema dawa za dokta ndodi au docta mwaka sijui docta kajamba Nani utadhulumiwa...na Kuna watu wengi wamekufa kwa kupotoshwa na Dr njaa...njia ya pili Niya mazoezi ya kujenga misuli ya mwili . Ambapo utatakiwa unyanyue vitu vizito ambapo itasaidia kujenga misuli ya sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo tumboni.....kwa experience yangu mtu ambaye amefanikiwa kupunguza tumbo ni witness aliyekuwa msanii wa hip hop...
 
Hizo njia zote ulizotaja wewe unazifanya kama Temporary, yani unataka Temporary solution inashindwa kufanya kazi unabakia na permanent problem


Badili mfumo wako wa maisha ,
Anza na diet (acha kula vyakula vya wanga kabisa)
Kula protein , healthy fat, matunda yani vitamins ..na n.k

Usishinde njaa kula ushobe lakini usile wanga wala carbonated drinks soda , na beer ukinywa unafanya sukari ya mwili inayotokana na wanga kuchelewa kunyonywa ..

yani ni matataizo ya insulin kuwa nyingi inapelekea sukari kuzalishwa kwa wingi na sukari unaongezeka uzito maana itakuwa vigumu ku burn calories/kuchoma mafuta ya mwilini kwako ..

Fanya mazoezi ya viungo mwli mzima atlist 40dk na mara3 /week ruka kamba kimbia , push ups squats


Ukianza hiyo life style umemaliza tatizo jipange sasa usisubiri hadi uumwe kisukari ndio ujali afya yako
Samahan mkuu.. hivi mtu akiacha vyakula vya wanga ale nini sasa?

Nataman nipate mlo mbadala wa wanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo njia zote ulizotaja wewe unazifanya kama Temporary, yani unataka Temporary solution inashindwa kufanya kazi unabakia na permanent problem


Badili mfumo wako wa maisha ,
Anza na diet (acha kula vyakula vya wanga kabisa)
Kula protein , healthy fat, matunda yani vitamins ..na n.k

Usishinde njaa kula ushobe lakini usile wanga wala carbonated drinks soda , na beer ukinywa unafanya sukari ya mwili inayotokana na wanga kuchelewa kunyonywa ..

yani ni matataizo ya insulin kuwa nyingi inapelekea sukari kuzalishwa kwa wingi na sukari unaongezeka uzito maana itakuwa vigumu ku burn calories/kuchoma mafuta ya mwilini kwako ..

Fanya mazoezi ya viungo mwli mzima atlist 40dk na mara3 /week ruka kamba kimbia , push ups squats


Ukianza hiyo life style umemaliza tatizo jipange sasa usisubiri hadi uumwe kisukari ndio ujali afya yako
Na mimi nataka ni nenepe kwa haraka najiona mwembamba .nitumie vyakula vya haina gani kwa wingi
 
Tumia mertfomin hutojutia!, Mm nilianza kwa 250 gram once per day nkila chakula Cha mchana nikiri kwamba from 125 now 80 Ila niliandikiwa na daktar.
Kwa Sasa nilishaacha hizo dawa tangu nkiwa na kg 112
 
Wataalam

Nimekuwa nikijiuliza hivi imeshindikana kweli kufanya surgery ya kuondoa mafuta toka kwenye tumbo? Mi naona jinsi yalivyojirundika sehemu moja tumboni kama mnavyotuaminisha kupitia michoro yenu nk ni kazi rahisi zaidi kama imewezekana kuzalisha mwanamke kwa kisu? Badala ya sijui kukata utumbo nk???au kuna kitu sijui hapa wataalam?

Nimehangaika sana kupunguza kitambi changu lakini sasa nimekata tamaa baada ya kubugia madawa mbalimbali ya kienyeji, herbal, food suplements, diet, kuacha kula wanga, mafuta, sukari na nyama nyekundu......Yote haya nimefanya lakini wapi......yaani kuna madawa nikinywa naharisha mafuta mpaka nasikia kizunguzungu...lakini kitambi kinabaki pale pale hata sijui yale mafuta huwa yanapungua kutokeaga wapi.....

Hii ni pamoja na kufanya mazoezi mepesi.......nilichoshindwa kuacha ni pombe kali - Vodka.....lakini nimejitahidi sana kuacha mavyakula ya ajabu ajabu hasa usiku...lakini wapi.......??...

Ttizo kila mtaalam wa mitishamba anakwambia dawa yake ni kiboko lakini wapi! ...nina mwaka wa tano sasa nahangaika na hili tumbo linanyima sana raha wakuu.....

Napokea ushauri wa kitaalam wa aina zote

Asanteni
Naomba kujua hayo madawa ya kuarisha Mafuta nianze nayo.
 
Back
Top Bottom