Hivi hakuna namna bora ya kusherehekea Uhuru bila kuonesha silaha za kivita?

Mkuu: nchi zote zilizowahi kuwa na eastern ideology ndio zao hizo - NK, Russia, China, etc. tena hawa hufungulia mavifaru na makombora kuyaacha yazurure mitaani kwa wiki nzima kabla kiongozi mkuu muadhama hajahutubia taifa ajenda kuu ikiwa kuitukana US na western countries!

Ajenda ya pili ni kuwatisha wananchi wasilete fyoko fyoko ili watawaliwe vizuri bila kuhoji! Na sisi tunapita mule mule sema hatujawa na jeuri ya kutukana US na western bado japo 2015 - 2020 baadhi ya vitimbakwira walijaribu ila walionekana wehu tu wasio na vision au lolote la maana wakaishia kupuuzwa ndani na hata nje.
Nakuunga mkono kwenye agenda ya pili mkuu
 
Hahahaha eti mara kibao? Said raia ambaye hata mafunzo ya jeshi hajapita, not even basic

Anyway unaweza kutaja idadi ya operesheni ulizoshoriki nao, mahali, idadi ya askari, logistics,transport modes, details of op, results, casualties. And with evidence pls
Wewe kama nani unanihoji hivyo?
 
Kuna jambo huwa linanitatiza sana kwenye hizi sherehe za kiserikali, uhuru au muungano.

Yaani imekuwa ni kama formula kwamba uhuru lazima tuoneshe masilaha ya kivita na makomandoo wapite pale wakirukaruka.

Mi nahisi, kuna kitu hakipo sawa kuhusu hili suala. Yaani ni kwanini sherehe za uhuru wa taifa inapambwa na mambo ya kijeshi?

Mimi nahisi labda viongozi wetu wamekariri na tena wamepotea vibaya sana.

Ingekuwa sisi ni nchi kama North Korea, Iran, Russia, China ingekuwa ni sawa kuonesha silaha zetu za kivita kwa sababu hizi nchi hizi silaha wanazitengeneza, kwahiyo siku ya uhuru wanaitumia kuonesha technolojia zao.

Ila kwa nchi kama Tanzania, hatutengenezi silaha tunanunua nje. Kwa maana yake ni kwamba silaha ambazo tunazo na wenzetu wanazo.. Kwahiyo moja kwa moja sioni point ya kujigamba na haya masilaha ya kivita ambayo ni imported.

Ningetegemea kuona tunasherehekea hizi sherehe na kuzitumia kama namna ya kuitangaza Tanzania, yaani tuoneshe vitu ambavyo ni Made in Tanzania.

Mfano jana tumeona mavifaru lakini ukiamka leo asubuhi hakuna value yoyote ya hayo mavifaru kwa Watanzania.

Ila imagine kama tungetangaza technolojia ya kitanzania, leo ingekuwa ina add value kwa watu.
Mkuu naona huelewi serikali ni kitu gani na hakuna namna ya kukusaidia- wewe endelea kuwaona hao kama wajinga na kuwa mshauri wao- ila hiyo ndiyo maana ya serikali
 
Nonsense kuonyesha silaha usizotengeneza, zote umenunua na tozo zetu, tena kutoka mataifa ya kikoloni. Wanatuchora sana
Unaamini hivyo- basi kama ni kweli muache mkeo kwa sababu ya hizo kucha , nywele za bandia na ngozi ya kujichubua
 
Kweli mkuu hili suala ni hoja ya mjadala! Hata hivyo nazani imetokana zaidi na wafrika wengi kuishi kwa mazoea kuliko ubunifu unaoendana mahtaji ya wakati!
Kwanza jeshi letu halikuchangia chochote ktk mapambano ya kudai uhuru, hatukuwa na jeshi lolote wakati ule lilikuwepo jeshi la mkoloni tu! Waliodai Uhuru wetu kwa mkoloni walikuwa wakulima, wafanyabiashara na wanasiasa, Hivyo matendo ya makundi hayo ndio ya kukumbukwa siku ya Uhuru!
Vinginevyo watasababisha watu tuache kwenda kuhudhuria au kufuatilia sherehe hizo luningani maana maonyesho yake hayana uhalisia na kilichofanyika wakati wa kudai uhuru na wala hayatowi mafundisho kwa vijana wetu!
 
Back
Top Bottom