Hivi hakuna namna bora ya kusherehekea Uhuru bila kuonesha silaha za kivita?

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,600
Kuna jambo huwa linanitatiza sana kwenye hizi sherehe za kiserikali, uhuru au muungano.

Yaani imekuwa ni kama formula kwamba uhuru lazima tuoneshe masilaha ya kivita na makomandoo wapite pale wakirukaruka.

Mi nahisi, kuna kitu hakipo sawa kuhusu hili suala. Yaani ni kwanini sherehe za uhuru wa taifa inapambwa na mambo ya kijeshi?

Mimi nahisi labda viongozi wetu wamekariri na tena wamepotea vibaya sana.

Ingekuwa sisi ni nchi kama North Korea, Iran, Russia, China ingekuwa ni sawa kuonesha silaha zetu za kivita kwa sababu hizi nchi hizi silaha wanazitengeneza, kwahiyo siku ya uhuru wanaitumia kuonesha technolojia zao.

Ila kwa nchi kama Tanzania, hatutengenezi silaha tunanunua nje. Kwa maana yake ni kwamba silaha ambazo tunazo na wenzetu wanazo.. Kwahiyo moja kwa moja sioni point ya kujigamba na haya masilaha ya kivita ambayo ni imported.

Ningetegemea kuona tunasherehekea hizi sherehe na kuzitumia kama namna ya kuitangaza Tanzania, yaani tuoneshe vitu ambavyo ni Made in Tanzania.

Mfano jana tumeona mavifaru lakini ukiamka leo asubuhi hakuna value yoyote ya hayo mavifaru kwa Watanzania.

Ila imagine kama tungetangaza technolojia ya kitanzania, leo ingekuwa ina add value kwa watu.
 
Mkuu: nchi zote zilizowahi kuwa na eastern ideology ndio zao hizo - NK, Russia, China, etc. tena hawa hufungulia mavifaru na makombora kuyaacha yazurure mitaani kwa wiki nzima kabla kiongozi mkuu muadhama hajahutubia taifa ajenda kuu ikiwa kuitukana US na western countries!

Ajenda ya pili ni kuwatisha wananchi wasilete fyoko fyoko ili watawaliwe vizuri bila kuhoji! Na sisi tunapita mule mule sema hatujawa na jeuri ya kutukana US na western bado japo 2015 - 2020 baadhi ya vitimbakwira walijaribu ila walionekana wehu tu wasio na vision au lolote la maana wakaishia kupuuzwa ndani na hata nje.
 
Marekani na Nguvu zote zile za kijeshi hata bunduki hawaonyeshi kwenye gwaride la kumbukumbu ya siku ya uhuru wao 🤣 🤣 Mkubwa ni mkubwa tu,na mkubwa hajaribiwi kwa kushikwa sharubu
Kabisa. Tena utashangaa hata mizinga wanapiga ile ya kizamani.

Kuonesha masilaha hakuleti tija yoyote.
 
Back
Top Bottom