Hivi hakuna madhara kwa Nchi kama Uongozi mbovu hauwajibishwi na Bunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi hakuna madhara kwa Nchi kama Uongozi mbovu hauwajibishwi na Bunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmaroroi, Jun 23, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wana JF nimekuwa nikifuatilia siasa za hapa kwetu Tanzania bila kujua uelekeo wake kwani kuna mihimili mitatau BUNGE,MAHAKAMA na RAIS.Vinategemeana katika Uongozi wa Nchi,mfano BUNGE linaweza kukataa bajeti ya Serikali kama hairidhishi na RAIS anaweza kuvunja Bunge kama haridhiki.Sasa kama BUNGE litaogopa kuchukua hatua kwa Wabunge kuogopa kupoteza nafasi zao,haina madhara kwa ustawi wa Nchi kama Uongozi hauridhishi? Nawasilisha,tuelimishane.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nchi zingine ni kawaida Bunge kuvunjwa na kufanyika uchaguzi mpya,hapa kwetu tatizo ni nini?kama kufanya hivyo kutasaidia maendeleo?
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  wanasubiri hasara kubwa zaidi kutokea ndio waseme ah, pale bwana/bibi ulizidisha, wakati huo inakuwa majutoo mjukuu. maafa yameisha tokea.
   
 4. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,076
  Likes Received: 15,730
  Trophy Points: 280

  Kwanza nimefurahi maana umenikumbusha ile kitu inayoitwa "Doctrine of Separation of power" kwa sisi hapa Tanzania zile sheria zote 3 ni sifuri kabisaa.

  wanaposema mtu mmoja asiingie katika sehemu zote yani executive, legislature na judiciary hapa kwetu ukiangaalia mwanasheria mkuu lazima aingie kote kote halafu tena waziri lazima awe mbunge na mengine mengi,

  Na kama rais ana mamlaka ya kuvunja bunge lisipotisha mswada, nani atachezea kitumbua chake? maana wanasema kwamba kama akilivunja uchaguzi utafika upya kama wakirudi wabunge walewale ina maana ule mswada wananchi wanauungana na wabunge wale na kama wakichagua wabunge wengine ina maana wananchi wanamuunga mkono rais.

  Separation of power iko USA tu hapa kwetu ni ndoto
   
 5. Muadilifu

  Muadilifu Senior Member

  #5
  Jun 24, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nyamungo,
  Asante sana kwa maelezo hayo, sikuwahi kuitazama hiyo dhana kwa mtizamo huo.
   
 6. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hiyo heading ndio jibu
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana wa Tanzania kama tunataka kusonga mbele ni vyema Sheria zetu hasa katiba irekebishwe ili iende na wakati kwani baadhi ya vifungu katika Katiba ya 1977 ni kikwazo katika wa mambo mbalimbali kutokana na kupitwa na wakati na hutumiwa na watawala kama ngao wanapokiuka maadili ya Uongozi.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na kama Bunge linashindwa kuwawajibisha viongozi wabovu, kwa nini wananchi wasifanye hivyo?
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hakuna wa kufanya hivyo kwani tuna SPIKA MZINZI na MLA RUSHWA sasa unategemea cha zaidi hapo?
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inawezekana kabisa kwa Wabunge kuweka msimamo na kupinga maazimio hata yote ya serikali. Ila kunaweza kukawa na matatizo yafuatayo (endapo hali hiyo itatokea):

  1. Bunge linaweza kuvunjwa na hivyo uchaguzi mpya kuitishwa. Hili si tatizo kubwa, japokuwa baadhi ya wabunge wanahofu kuanza tena kampeni na haina maana kuwa vyama vyao vitawateua tena kugombea Ubunge kwa ticket za chama hicho (hasa Wabunge wa chama tawala - in this case CCM)
  2. Rais anaweza kuamua (endapo atataka) kufuta uanachama wa Wabunge wanaoonekana kupingana na serikali yake. Hivyo wabunge hao automatically kupoteza nafasi zao za Ubunge. Hili linaweza kufanywa kwa urahisi sana na Rais bila kuhitaji vikao vya kichama. Majimbo yao yakiwa wazi, ni dhahiri chama chao hakitawateua tena kugombea (kwa kuwa ndicho kilichowafukuza uanachama na pia hawatakuwa wanachama wa chama hicho tawala). Hili ndilo linaloogopwa na wabunge wengi. Wanajua wakifukuzwa kwenye chama kwa kushindwa/kukataa kutetea msimamo wa chama chao, basi watathirika sana kisiasa.

  Solution: Katiba ibadilishwe na kuruhusu Mbunge kuendelea hadi mwisho wa kipindi chake cha miaka 5 hata kama chama chake kikimfukuza uanachama. Vinginevyo, Katiba ibadilishwe na kuruhusu wagombea binafsi. Lililo rahisi kutekelezwa ni la kuruhusu Mbunge kumalizia muhula wake hadi uchaguzi, isipokuwa kama atashindwa kabisa kutekeleza majukumu yake ya Kibunge, akifariki au akiamua mwenyewe kuachana na nafasi hiyo kwa hiari yake.

  Sababu za kutaka vipengele vya Katiba vibalishwe na kuruhusu hayo ni kwa kuwa Mbunge amechaguliwa na wananchi na hivyo ni kunyima haki kwa wananchi endapo Mbunge atapoteza haki ya kuwakilisha wananchi wake kwakuwa tu, chama chake hakimtaki tena. Logically, sababu za kumnyang'anya mtu Ubunge kwakuwa amepoteza uanachama hazina manufaa kwa Taifa wala kwa jamii anayoiwakilisha.
   
Loading...