Hivi haiwezekani kuwa na CCM imara, Upinzani imara na Serikali makini kwa wakati mmoja?

Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!

Kufikia kiwango hicho cha maendeleo/ustaarabu siyo rahisi. Bado sana.
 
Tatizo ni ujuaji mwiiingi wa wanasiasa wetu. Wanadhani kuwa imara lazima umdhoofishe mwingine ndiyo maana wanachafuana lakini wakiungana chama kimoja wanaanza kusafishana.
Chadema walisema lowasa ni fisadi,alipoingia kwao wakasema sioyeye...ccm wakasema niyeye tens anajinyea tens anakaribia kuaga...aliporudi kwao sasa hafi tena na wamemkaribisha kwa nguvu na shamrashamra haswaaa.
Hizi ni siasa za kipwagu pwaguzi chama cha siasa kinataka kuwa kama vikundi vya miziki ya bongo fleva.
 
Back
Top Bottom