Hivi haiwezekani kuwa na CCM imara, Upinzani imara na Serikali makini kwa wakati mmoja?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,423
147,100
Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
 
Inawezekana.

Tatizo ni CCM.

Hawaamini katika upinzani.

Kwa CCM upinzani ni kama jinai.

We mtu kama polepole anafikia hatua ya kusema hata Mungu hakutaka upinzani ndiyo mana akamfukuza shetani.

Mwengine anakwambia atahakikisha anaufuta upinzani kufikia 2020.

Achilia mbali hii sheria mpya inayompa uungu mtu msajili wa vyama lengo kubwa ikiwa ni kuvibana vyama vya upinzani.

Kwa hali hiyo tunaachaje kuiona CCM ni tatizo.
 
Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
Hapo ndipo nchi itapiga maendeleo makubwa....

Tatizo la nchi hii lipo kwa Jiwe, kwa sababu yeye binafsi ndiye anauchukia upinzani kwa kiwango kikubwa kabisa

Kwa dunia ya sasa ni lazima kuwe na mfumo wa kidemokrasia wa hali ya juu sana

Kwa njia hii anayotupeleka Jiwe, hakika anatupeleka shimoni, ambako Taifa hili litazikwa!
 
Shida ni wanasiasa wetu wapo kimaslahi zaidi na si wakweli leo ataamini hili kesho lile.....kila mmoja anaangalia atanufaika vipi na hawayaishi maneno yao.....nachama tawala wanatake advantage hapo tu
 
Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
INGEWEZEKANA PIA INAWEZEKANA.
Suluhisho ni katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi.
Lakini kwa mwenendo tulionao sasa hayo ni NDOTO ZA MCHANA
RASIMU ILE YA WARIOBA ILIKUWA INAJIBU KILA SWALI TATA LA NCHI YETU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.
Muulize JPM na watangulizi wake huko CCM. Binafsi sioni kwa nini lisiwezekane kama concept ya CHAMADOLA na SAUTI MOJA zitawekwa kando kama ustarabu unavyo hitaji. Lakini mambo yenyewe yakiwa kama yale ya Korogwe Vijijini kwa zaidi ya masaa 5 vyama zaidi ya Vitano "vinashindwa" kurudisha formu za wagombea wao na tume ya uchaguzi inapiga tiki basi wee acha tu.
 
kuna genge fulani linalofanya kazi bila oversight yoyote, walipaswa kuwa walinzi wa katiba na demokrasia yetu na walipswa kuhakikisha nchi hii ina siasa safi, lakini kutokana na incompetence zao wamejigeuza walinzi/walezi wa chama tawala.
 
Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
Hii inawezekana, lakini kwa sasa haiwezekani kwasababu

"Wenye Ujuzi hawana Confidence, na wajinga wanayo confidence na wameshikilia Rungu."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ni wanasiasa wetu wapo kimaslahi zaidi na si wakweli leo ataamini hili kesho lile.....kila mmoja anaangalia atanufaika vipi na hawayaishi maneno yao.....nachama tawala wanatake advantage hapo tu
Kweli kabisa mpaka labda tufike kiwango fulani kiuchumi mwa mtu mmoja mmoja. Vyama ni kama family business
 
Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!

Nasikia kuna mjadala wa amani huko TBC1, imekuwaje hujaripoti hilo kongamano?
 
Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
Ndiyo, kwa Tanzania hii bado saaaana. Ndani ya ngumi hii hamna kitu kama hicho, sahau kabisa. Ccm ya leo ni mpya kweli kweli, centralized unquestionable governance ndio sera ya awamu. Unatakiwa kuimba ,"Jina lako litukuzwe na mapenzi yako yatimizwe" ndio utaishi kuiona kesho yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
Hapo Ndipo nchi za Afrika zingeondoka kwenye '3rd word countries' Si kwamba hakuna wenye uelewa huo but 1st world walisha 'tuprogramme.' Subiri uwe mtumwa tena, jamaa wanarudi na sababu ni kushindwa kujiendesha kistaarabu matokeo yake mnatesa na kuua binadamu wenzenu na kusumbua dunia.
 
Huu utatu wa kisiasa kwanini unashindikana?

Yaani tuwe na Chama Cha Mapinduzi imara kabisa. Kisha tuna Upinzani imara kabisa na tukawa na Serikali makini kabisa isiyosubiri mashinikizo ya kisiasa kuendesha shughuli zake.

Hili haliwezekani kweli hadi tukeshe tukibomoana kila iitwapo leo?

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
Inawezekana kabisa ila polepole polepole na genge lake hawataki kabisa jambo hilo. kwa ujumla ingekuwa hivyo ndio tungeendelea kama Taifa. Jamaa hao niliowataja hawana nia njema na nchi. Wametujaza chuki tu sisi kwa sisi, tunajiona ni maadui na ndicho wanachopenda Bashiru na Polex2, na jiwe mlaaniwa
 
Hilo ndilo lilikuwa lengo tulipokubali mfumo wa vyama vingi. Lakini kadri siku zinavyopita ndivyo wanasiasa wetu wanavyozidi kupwaya katika nafasi zao. Badala ya kutumia ushawishi wa kisiasa kupata ufuasi wanatumia ulaghai, hila, mabavu, kuvunja katiba na hata kuuana kudhoofisha upended wa pili. Wanaodhani hiyo ni siasa hawajui siasa.
 
Tatizo ni Viongozi wanaotokana na CCM kutokuwa na ufahamu mzuri hivyo kuamini katika kupata madaraka kwa njia yoyote ile hata kama ni kuangamiza wakosoaji wao.

Matumizi ya wasiojulikana na vyombo vingine vya dola kuhakikisha CCM wanatawala bila ya ushawishi wa hoja kwa watu haviwezi kuisha kwa kuwa vinawapa turufu ya kuendelea kutawala.

Siku CCM wakiamini kuwa hata vyama vingine vinaundwa ma watanzania wenye uwezo mkubwa kuwazidi hata wao na wana haki ya kuwa viongozi wa taifa hili, tutakuwa tumepiga hatua kubwa ya kimaenddeleo! Na kwa aina ya viongozi tulio nao mpaka tuzichape ndiyo tuheshimiane!
 
Back
Top Bottom