Hivi haiwezekani interview ikafanywa kwa Kiswahili?

ranjan

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
338
288
Nimekuja kugundua watu wengi hawana ajira si kwamba hawana uwezo au akili, lakini Ni Kiingereza ndiyo kiliwakwamisha kupata kazi.

Unakuta Mtu ni graduate kabisa lakini Hana uwezo wa kunieleza kwa kiingereza ,lakini Ni mzuri practicaly.

Mfano mzuri, hivi kazi Kama bank teller hiyo ata form four anaweza fanya au form six. Au kufungulisha watu account bank, zipo nyingi, lakini watu wanakosa kutokana na lugha.

Me nadhani serikali iliangalie hili, ikiwezekana lungha ya kiingereza itimike kufundishia masomo yote katika.shule za msingi na awali ili watu wajijengee msingi mzuri wa lugha. Ni hayo tu.
 
Inawezekana, ila interviewer ndo anaeamua na hiyo pia inadepend na position husika unayotakiwa. Ila si mara nyingi.

Kikawaida mi navyoingia interview room namsikilizia kwanza interviewer ataanzaje akianza kwa kiingereza, lazima umalizie kiingereza, akianza kwa kiswahili usijifanye unajua kiingereza unamalizia kiswahili.

Makadirio katika interview 100 nilizofanya interview 3 ndo ilikuwa kiswahili, na hizo walikuwa hawahitaji professional. So ni nadra sana.
 
Mkuu ajira nyingi inaitaji kigezo moja wapo lazima ujue kuzungumza kiingereza kwa hiyo interview inakuwa ni sehemu ya kuthibitisha je hicho kigezo unacho? Unaweza kujieleza kwa lugha hiyo.
 
Mtoa mada naona umetoa ushauri kwa serikali katika paragraph ya mwisho bt huo ushauri hakuna hata kiongozi ambaye anaweza fanyia kazi hvyo cha msingi pambana usomeshe watoto wako Zile shule za kingereza ili huko mbelen waondokane na haya majanga yakutojua kuongea kingereza hali ya kuwa una gamba lako lenye GPA za kibabe.Pia kingine ni kwamba serikali huwa wanatuzuga kusema kiswahili ndo kila kitu lakin wenyew kwenye nyaraka zao nyingi sana zinaandikwa kwa kingereza na mbaya zaidi kwenye hizi saili zao ukishindwa kuongea tu imekula kwako.
 
Back
Top Bottom