Hivi Gesi yetu imeishia wapi?

mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,273
1,225
Wakuu, nilikua nataka kujua hivi hii gesi yetu na mambo ya uchumi wa gesi yameishia wapi?, naona Wakuu wa awamo ya tano hawaongelei kabisa gesi na ukiangalia harakati iliyopo ya kimakakati ya kiuchumi inaashiria hamna gesi katika mikakati hiyo..

Tunajua gesi ingesaidia Sana katika ujenzi wa miundombinu yetu kwa kasi na kuunganisha nchi yetu na kufanya shughuli za uzalishaji kua nafuu na fanisi zaidi huku mitaji ya ndani na nje ikizunguka kwa urahisi zaidi, na mengineo mengi kama uboreshaji elimu na mishahara ya walimu Wetu, vyombo vya usalama, na kuwekeza katika makazi mijini na kuwekeza nje kiasi kingine ill kuepukana na mzunguko mkubwa wa fedha kuliko uzalishaji wa ndani. Haya yalikua matumaini sasa ukweli iko wapi?

ingependa kupata taarifa yeyote ya jambo hili kwa wale wanaojua au wafuatiliaji wa hili jambo pamoja na kuwatarifu wengine wenye kutaka ufahamu kama Mimi. Tujuzane kwa upeo na uelewo mzuri.
Asante.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,342
2,000
Bado inafanyiwa utafiti kule China. Si unajua kuwa gesi zingine zaweza kulipukia majikoni mwetu? Vuta subra majibu yakirudi tutaanza kuipakua pale Bagamoyo kurudi Ntwala wenyeji waionje.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,370
2,000
Wakuu, nilikua nataka kujua hivi hii gesi yetu na mambo ya uchumi wa gesi yameishia wapi?, naona Wakuu wa awamo ya tano hawaongelei kabisa gesi na ukiangalia harakati iliyopo ya kimakakati ya kiuchumi inaashiria hamna gesi katika mikakati hiyo..

Tunajua gesi ingesaidia Sana katika ujenzi wa miundombinu yetu kwa kasi na kuunganisha nchi yetu na kufanya shughuli za uzalishaji kua nafuu na fanisi zaidi huku mitaji ya ndani na nje ikizunguka kwa urahisi zaidi, na mengineo mengi kama uboreshaji elimu na mishahara ya walimu Wetu, vyombo vya usalama, na kuwekeza katika makazi mijini na kuwekeza nje kiasi kingine ill kuepukana na mzunguko mkubwa wa fedha kuliko uzalishaji wa ndani. Haya yalikua matumaini sasa ukweli iko wapi?

ingependa kupata taarifa yeyote ya jambo hili kwa wale wanaojua au wafuatiliaji wa hili jambo pamoja na kuwatarifu wengine wenye kutaka ufahamu kama Mimi. Tujuzane kwa upeo na uelewo mzuri.
Asante.
Mkuu hii nchi ni ngumu sana na masikitiko yangu ni kuwa watu tunahoji mambo ya msingi uwa tunaishia kujibiwa kisiasa.....

Swala la gesi linatia kinyaa sana mikataba ilipitishwa kwa hati ya dharura hapo tu ndio nilikata tamaa na kujua tumepigwa.......

TPDC wapo wanabariki ukwapuaji kinachowapata ni kubadirisha mkurugenzi wake wakati mkurugenzi mpya hawezi kubadirisha mikataba iliyosainiwa na mtangulizi wake........

Masikini nchi ilivyo masikini wachina wamejenga bomba kwa garama Mara mbili .

Inauma sana sometimes kufatilia mambo ya Tanzania unaweza kuwa mweu.......
 
mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,273
1,225
Mkuu hii nchi ni ngumu sana na masikitiko yangu ni kuwa watu tunahoji mambo ya msingi uwa tunaishia kujibiwa kisiasa.....

Sala la gesi linatia kinyaa sana mikataba ilipitishwa kwa hati ya dharura hapo tu ndio nilikata tamaa na kujua tumepigwa.......

Masikini nchi ilivyo masikini wachina wamejenga bomba kwa garama Mara mbili .

Inauma sana sometimes kufatilia mambo ya Tanzania unaweza kuwa mweu.......
Tatizo watz bora liende...kujua mambo ni kujiumiza kweli
 
pyongyang

Senior Member
Aug 31, 2016
112
225
Mkuu huu uchumi wa gesi asilia upo complex kidogo, kwakuwa sehemu kubwa ya utafutaji na uzalishaji tunategemea kampuni za kigeni ambazo nazo zinataratibu zake hasa katika kuamua nilini waanze uzarishaji, hii kitu huenda inafanya hata viongozi wetu washidwe kuweka bayana nilini tutaanza kunufaika na hii resource ingawa lazima tukiri kwa kiasi fulani tumeanza kunufaika na rasilimali hii kwani kiasi kikubwa cha umeme kinazalishwa na gesi

Serikali iiwezeshe TPDC iweze kusambaza mabomba ya gesi katika nyumba za watu kwa kuanza na mikoa iliyojirani na rasilimali hii, angalau watu waone moja kwa moja manufaa ya hii raslimali.
 
Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
16,596

Tunaeleza mambo makubwa kama ni rahisi mno. Engineering behind the gas extraction is very complex...investment on processing the gas for commercial markets is so collosal....and behind it, there should be well intended preparations. Tuna maneno mengi kuliko matendo...waelezee maana wengine labda wanafikiria hiyo ni gas ya kupikia inapatikana kwa kituo cha Lake Oil
 
Prince Kunta

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
16,364
2,000
Kuna maneno yao huwa wanayatumia sana wakieleze gesi kama haya:
●mchakato
●Kuchakata
●kinyerezi one
Utasikia serikali ipo mbioni kuanzisha kituo cha "kuchakata" gesi asilia
 
mchumia tumbo

JF-Expert Member
Jun 19, 2012
1,442
1,500
Hivi ile gesi ya Mtwara inafika dar kweli?Maana nasikia dangote tu haijapata anatumia mafuta tu
 
Top Bottom