Hivi gazeti la THISDAY haliuziki bila kumuandika Manji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi gazeti la THISDAY haliuziki bila kumuandika Manji?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by uporoto01, Nov 14, 2008.

 1. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimekua nasoma gazeti la Thisday mara kwa mara na haipiti siku mbili bila kuona habari za Manji na mara nyingi ni za kumkandamiza.Mi binafsi simpendi Manji lakini naona hii ni zaidi ya 'Obsession'.Naomba kutoka kwa wenye kujua zaidi kuna kitu gani baina ya Mengi na Manji? Navyo ona mimi hapa ni zaidi ya 'Personal' labda kwakua MAnji ni muhuni na Mengi ana watoto wa kike kuna kitu kilitokea? Mnaweza kuona hata kwenye hii ya 'import support' inahusu watu wengi lakini ukisoma Thisday unaweza dhani ni Manji pekee anahusika.
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Safi Thisday!!! ukitaka kuua nyoka anza na kichwa chake then mkia utaukata baadaye!!! Manji ndo beneficiary mkuu wa CIS!!!!! na alikuwa anazuga kulipa kwa kuwa anakingiwa kifua na bigshots!!!!

  Hakuna cha ugomvi wala nini, huo ndiyo uhuru wa vyombo vya habari tunaoutaka wa kuandika bila woga. Editors wake wako makini na media ni kama kioo kinamulika na kutoa hali halisi. Na kwa hilo la Manji ni global na linaathiri uchumi kwa namna moja au nyingine.

  Hakuna ubaya hapo. Grand corruption na mambo mengine kama hayoo ya CIS ndo tunataka tupate habari zake na si vihabari vya mtu kulalia muhogo na kuamkia mhogo. Thanks and big up Thisday Editors and my beloved Kulikoni!!!
   
 3. Arsenal

  Arsenal Senior Member

  #3
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Manji ana hela za epa na import support ambazo alizitumia kumshinda Mengi kwenye kila opportunity ya kibiashara na pia hela ambazo wabunge na viongozi wako wakubwa anawashikia na apo ndo Mengi hakubali which makes sense! why yeye? ana ujinga flani angalia ata kwenye michezo why Yanga and not Simba????? basi wangegawana ye na rostam yanga na simba...upo?
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hili gazeti na la KULIKONI yalianzishwa rasmi kwa ajili ya kumchafua mfadhili mkuu wa YANGA ambaye ndo Manji....lakini kumbuka ugomvi naoana ulianzia pale Mengi alipokataliwa na wana Jangwani kuwa msuluhishi akaja Manji akapokewa kwa vifijo na vigelegele mpaka leo akina mzee Mzimba wanatengeneza matumbo pale mitaa ya Twiga na Jangwani. Yawezekana kabisa bifu ndipo lilipo anzia hawa wadosi wawili.
   
 5. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uzuri yanayoandikwa kumhusu Manji yana ukweli, otherwise ThisDay & Kulikoni yangekuwa yashafungwa siku nyingi.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280


  F80 pamoja na yote hayo haka kajamaa Manji kana kiburi kwa sababu ya vijisenti hivyohivyo vya CIS na EPA na frauds nyingi kibao ukiweka ile ya ........inayosemekana agenda ile ilisababisha kifo cha mheshimiwa mmoja.

  Fahamu kuwa Manji amebebwa sana na serikali kwa kuwa anachangia sana chaguzi kwani mihela ya bure anayo.We mtu kama Mengi anekimbizana na mikopo ya benki anazo hela za kutupa??? Tena Mengi namsifu kwa kuwa anatoa misaada kwa jamii tena bila kubagua dini na rangi!!! Je Manji ametoa misaada mingapi kwa jamii? Pale Yanga sisemi anatoa msaada bali anataka awe mshirika mkubwa ili kufanikisha mambo yake. Zamani si unaju wanatumia mipira na ..... kuhifadhia ile haramu....Na pia anapima mwelekeo wa upepo maana anajua kipindi hiki upepo uko kwenye kuendeleza soka.

  Wanachama na wachezaji wa Yanga walimpokea Manji kwa kisihindio hii ni kwa sababu ya njaa tu si kwa kuwa wanampenda. Wanajua Manji ana midili ya hela chafu so watapata pesa. Watahangaikaje na Mengi ambaye pesa anaitafuta kwa nguvu. Sasa kumbe wangekubali Mengi awasuluhishe pengine wangesaidika zaidi.

  Si unaona hata hili la EPA, Manji alirudisha pesa maana ilibidi mbinu zifanyike ili RA asionekane kuwa anahusika na EPA hivyo Manji akaombwa abebe EPA ya Kagoda na akakubali japo pesa halisi aliyorudisha inawewezekana imetoka kwa mtu mwingine na yeye kutumika tu au pia ni changa la Macho pengine Kagoda haijarudisha kitu!!!! Mwenye data za jinsi fedha za EPA zimerejeshwa na kwa kiasi gani kwa kila kampuni alete hapa.

  Nchi inayumba na itaendelea kuyumba. Who will be our change?????
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,548
  Trophy Points: 280
  Hakuna ubishi This Day na Kulikoni ni magazeti makini na waandishi wake are wanafanya really investigative journalism. Big Up for that ila nakubaliana na anayeuliza kulikoni?.
  Hakuna asiyejua kuna bifu ya kibiashara kati ya Mengi na Manji. Mengi alijiingiza kuutatua mgogoro wa yanga na naamini alimwaga faranga, mgogoro ule ukamshinda na kutaka kumtia aibu. Manji akapenyeza rupia, kama penye uzia, mgogoro ukaisha.

  Ugomvi mkubwa wa Mengi na Manji ni ubaguzi wa rangi na vivu wa umasikini wa roho ambapo Mengi kama Mtazania mzawa tena Mbantu aliumia roho kwa nini Manji, Mtanzania mwenye asili ya kihindi alikopeshwa shilingi bilioni 9 na mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF kwa ajili ya kujenga Quality Plaza. baada ya hiyo Quality Plaza kukamilika Manji akawauzia hao hao NSSF hiyo Quality Plaza kwa gharama za Shilingi Bilioni 50!.Alipolipwa ndipo akatoa ile Bilioni 9aliyokopeshwa bila riba na yeye akabakiwa na Bilioni 41!. Good Bussiness!. Mengi kwa vile ni mfanya biashara mkubwa akapiga kelele tunaibiwa hapa!.Akapaaza sana sauti kupitia vyombo vyake vya habari.
  Tatizo la Mengi aliweka wazi chuki na ubaguzi dhidi ya jamaa zetu wahindi bila kujua wameshapenyeza rupia sehemu zote muhimu. NSSFwalijubu ilikuwa biashara safi.Mengi anapaza sauti kupitia vyombo vyake ili hatimaye iwe ni kilio cha wananchi wote. Hii ndiyo kazi inayofanwa na This Day na Kulikoni lazima yapige tarumbeta hii kwa nguvu zote, after all who pays the piper may call the tune.
  One thing is clear ni kuwa Manji is not clean,he is really dirty indeed! swali ni How clean is Mengi?.
  Pamoja na uhuru wa wana JF sidhani kama mtakubali kuwa na Thread kama hii kwa vile Mengi amejijengea heshima kubwa kwake yeye binafsi, jamii ya kitanzania na kimataifa kwa ujumla kuwa he is a really philantropist.
  I believe deep down from inner voice, something is telling me Mengi is not all that clean. Yes he is white but not all that white, some of it is a painting and it will fed with time where the true colour will be vividly be visible.
  Keep on doing the good work your doing huku tukisubiri the time for the true colour.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,733
  Trophy Points: 280
  Sioni ubaya wowote wa gazeti hilo kuandika habari za Manji kama zina umuhimu kufahamishwa kwa Watanzania hasa kama zinahusu mapambano dhidi ya mafisadi.
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama una matatizo na content, na siyo innuendo kuhusu imagined vendetta, leta hapa serious objection kuhusu content.

  THISDAY ni gazeti huru, linaweza kuamua kuji dedicate kwa mtu yeyote, likawa linaandika story zake tu gazeti zima kutoka article ya kwanza mpaka ya mwisho, hamna kitu kinachowazuia kufanya hivyo. Katika ulimwengu huu wa ushindani, as long as habari hazina unsubstantiated malicious content, kumshikia bango mtu poa tu.Kuna vitu vingine haviendi mpaka kwa kushikiwa bango.

  Sasa una nondo kuhusu accuracy ya content?
   
 10. DDT

  DDT Member

  #10
  Nov 14, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  U're very right Pasco, ila unasahau Manji na washirika wake RA&EL wanahodhi vyombo vingi kuliko Mengi, wamewashika wahariri wengi Tanzania hii, wanahodhi mpaka mawasiliano ya simu, je ni kweli wameshindwa kuandika na kudadavua kuhusu the 'black' Mengi?
  Soma bold mkuu, hapa ni JF kama una nondo za kuweka kuhusu the 'real' Mengi weka hapa zitadadavuliwa tu...where we dare to talk openly!
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Waambie DDT,

  Mbona Mengi tushamjadili sana tangu kitambo tu? Mpaka alivyokuwa anakwenda kwa kidosho wake wa Kinyarwanda pale Mindu St ? Mpaka mke wake alipokuja na mguu wa kuku na kusimamishwa na walinzi getini? Mpaka Mzee Mzima alivyoruka ukuta na kukimbilia kupanda teksi Muhimbili? Siku nyiiingi tu.

  halafu with all that open hipocrisy anakuja ku preach kuhusu ngono na ukimwi!

  Watu wanamjadili Mungu, itakuwa Mengi!
   
 12. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Au anayeuliza hivyo ni Manji mwenyewe?Who knows,anaweza kuwa anakuaja hapa kufatilia hasira za walalahoi dhidi ya ufisadi.

  Just thinking aloud,no offence intended!
   
 13. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yawezekana magazeti mengine yamekula mlungula wa Manji ili yasiandike sana kuhusu yeye???

  Halafu pundit, hii usikumbushe!!!! eti!!!

  Tobaaa!!!!

  Isiwe ugomvi wao umehamia kwa vidonsho?!!! hivi yule mama anaeendesha BONGO STAR SEARCH yuko na nani sasa??? Maana nilisikia mzee keshatemwa!!!!
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Aliwahi kufanya hivyo zamani, alikuwa anawalipa wahariri kuhakikisha kuwa habari sanasana zinazomchafua, hazitoki kwenye vyombo vya habari. lbda anaendelea kufanya hivyo
   
 15. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sioni tatizo hapa.Kwani habari zinazoandikwa ni za uongo au? After all lile ni gazeti huru.Ina maana kama mtu kila siku ana jipya asiandikwe kwa hofu ya kuwa atakua ameandikwa sana? Utakuwa sawa tu endapo habari za manji huwa zinarudiwarudiwa kama zilivyo kila siku which is not true at all.
   
 16. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Mh! Haya bwana.Mbona huyu jamaa huwa anazungumzia sana mambo ya Mungu as if ameokoka? Mbingu kuiona kazi!
   
 17. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  There are more people involved in this 'import support' scandal including many former and current Ministers and MP's so 'Thisday' can tell us their names and amounts involved while they still continue with their Manji headlines thereby informing us while they still zero in on Manji.
   
Loading...