Hivi Gazeti la Mwananchi nalo limeshakuwa Gazeti la Udaku?

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,492
92,911
Odemba amtesa Kim Kardashian
Send to a friend
Saturday, 19 May 2012 12:25
0digg

000001anitaaaa.jpg

NANI alijua kuwa hata wanawake wazuri kama Kim Kardashian nao huwa wanateswa na wivu, basi amini usiamini Miriam Odemba alimnyima raha mlimbwende huyo baada ya kuwa bega kwa bega na 'boy frend' wake, Kanye West.

Inadaiwa kuwa Kim alianzisha patashika nyuma ya jukwaa wakati mpenzi wake huyo akizindua nguo zake mpya huko Ufaransa.

Kim na Kanye walikuwa Paris kwa shughuli hiyo na Odemba yuko huko Ufaransa kwa kazi yake ya kuonyesha mavazi.

Inasemekana Odemba aliwahi kukutana na Kanye West na kujuana mwaka jana wakati rapa huyo akizindua nguo za kwanza huko Ufaransa.

Sasa wikiendi hii Kanye West alipokwenda tena Odemba baada ya kumuona rafiki yake, alimchangamkia na kujumuika naye kucheza muziki kitendo ambacho hakikumfurahisha Kim.

Wakati Kanye akicheza na Odemba, Kim alikuwa amekaa na Swizz Beatz na mkewe Alicia Keys, unaambiwa Kim alikuwa hapepesi macho kwa wivu.

Hata hivyo Kim anadaiwa kuwa alishindwa kuendelea kuvumilia kuona mwanamke mrembo akiendelea kucheza na mpenzi wake na kuhatarisha penzi lao changa. Moja kwa moja alimvuta Kanye huku maneno yakimtoka.

Mastaa wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na
D’Banj, P.Diddy, common, Big Sean, Cassie na Waka Flocka Flame.

My take: Sikubaliani kwa Gazeti makini kama mwananchi mhariri wake kuruhusu huu uandishi wa style ya kina Shigongo, hapa ni kweli kuna habari ya kuripoti lakini habari yenyewe ya kuripoti tulipaswa kuelezwa kwa ufasaha huyu Odemba anaendeleaje na mambo yake ya maonesho ya mavazi na siyo swala la kucheza muziki na mume wa Kim.
 
ulitaka waaandike siasa kuanzia mwanzo hadi mwisho?
lazima waandike burudani pia so kila mtu anapenda kusoma siasa.
acha hizo magaeti mengi yana safu kama hizi
 
Mkuu acha uvivu wakufikiri,hii habari ipo kwenye kijarida kinachopatikana ndani ya hilo gazeti,kinahusu udambwi dambwi.....
 
Tujitahidi tuelewe aina za uandishi jamani,Mwananchi kila jumamosi ndani kuna kijarida kinachohusu burudani nadhani hiyo habari ni sehemu yake muafaka!
 
Acha kukurupuka ww unajifanya makini huna lolote,ukipata habari mbio kuileta kabla ya kuichunguza,lile ni Gazeti la Habari mchanganyiko sio Siasa pekee!
 
Mwananchi waepuke kishawishi cha kugeuka gazeti la udaku. Habari hii ni ya kidaku zaidi!!!
 
Mkuu acha uvivu wakufikiri,hii habari ipo kwenye kijarida kinachopatikana ndani ya hilo gazeti,kinahusu udambwi dambwi.....
Mkuu nafikiri mtoa mada ana negatve self inclination kwa Gazeti la Mwananchi kwa ujumla.
Habari yenyewe haina mshiko na hajatujuza imeandikwa ukurasa gani.
Kwa wengi wetu bado Gazeti la Mwananchi ni gazeti makini kuliko karibu magazeti yote ya kiswahili.
 
Unashangaa nini wakati Tanzania ni nchi ya wadaku watupu kuanzia wakubwa hadi wadogo? Hiyo picha itakuondolea mshangao wako.
IMAG0191.jpg
 
Back
Top Bottom