Hivi GADAFFI amefanya kosa gani? Kwa Wa-Libya,Afrika na Dunia

Leta statstics za umaskini wa walibya ukilinganisha na watanzania. Huduma za kiafya shule nk.

Kidzude usitumie taarifa za mitaani, hakuna nchi isiyokuwa na masikini duniani mpaka sasa.

udini unakusumbua wewe. Mbona alishawaomba msamaha na mkamsamehe. je Bush nsi kichaa alimtoa Saddaam.

Mkuu unasisitiza aliomba msamaha, alitumia utaratibu gani kutuomba msamaha watanzania na sie tulitumia utaratibu gani kumsamehe. Na kama aliomba msamaha mbona hatulipi fidia tuliopoteza ndugu kwenye vita vya kagera kama alivyokubali kuwalipa fidia waliofiwa na ndugu baada ya kuilipua ndege ya PANAM? Binafsi siwezi kumsamehe chizi kama Gaddafi ila nimewasamehe Walibya kwasababu walimsaidia Idd Amin bila kupenda.

Miafrika mirahisi sana kuigawanya.Unadhani ingekuwa Europe wangekubali?

1. Makosa yake makuu ni kutaka kuunda African Monetary Fund

2. kuweka Pan -African Communication Satellite bure kwa Afrika na hivyo Waafrika wakaacha kulipa dola mil 500 kwa Ulaya na Marekani kwa kutumia satellite zao.

3. Kuwa na kiherehere cha kusema Afrika iwe moja na Jeshi moja

4. Kuzuia Mabeberu kujichukulia Mafuta ya Libya kama wanavyochukua dhahabu na Vitu vingne ikiwemo wanyama Kule Tanzania.

5.Kiherehere cha Kuanzisha African Bank na kutoa dola bil 90 kama mtaji

6. Kukataa kuwapigia Magoti wazungu kuhusu suala a Matumizi ya Dola anataka Afrika iwe na currency Moja

7.Kupinga Sudan Kusini kujitenga na hivyo kusababisha wazungu wakose mafuta Mengine ya bwerere

Yako Mengi ngoja kwanza nimpigie Simu Saif Islam Nimwellekeze la kufanya kwenye hii vita..nicheki tena baadae

ndugu yangu we acha tu! Kwani siye tulio na demokrasia mbona kila siku tunalia njaa? Ila Libya karibia 100% ya mahitaji ya kibinadamu ilikuwa ni FREE.kweli binadamu hana shukrani tusubiri tuone.....

Ntagunga umenena (wanasemaga nipe tano!).

Ubishi wa Gaddafi usio na mpango umemponza. Watu wengi humu jamvini wanafikiria kama unampinga Gaddafi basi wewe ni kibaraka wa wakoloni. Hilo sio swala, viongozi wabishi ka Gaddafi ni watu wa kuteketezwa tu. Hiyo ndio dawa yao! Mie nshaona kuna jamaa humu hisia na hasira zimewazidi mpaka hekima imepotea. Kisa eti Gaddafi na utawala wake wa kidikteta umeangushwa. Duhu!
'''Sikubaliani na mawazo yako asilimia 90,kwani unadhani ukoloni mambo leo kama wanavyoendelea kuufanya hawa wazungu huko Libya utaleta democrasia ya kweli pale Libya'''simply ni kwamba haiwezekani,,,,as democracy kamwe haiwezi letwa na NATO kwa njia wanayotumia sasa'''Kinachofanyika ni ujambazi na uporaji wa mali za Wa'Libya kwa kutumia mabavu.

kati ya yote kosa kubwa sana alilofanya ni nchi yake kuwa na mali nyingi hasa mafuta,wakati huohuo anatumia mali hizo yeye na Wa Libya bila kutoa mwanya kwa NATO kufaidi mali hizo hata kidogo.

....kati ya yote kosa kubwa sana alilofanya Gaddaf ni nchi yake kuwa na mali nyingi hasa mafuta,wakati huohuo anatumia mali hizo yeye na Wa Libya bila kutoa mwanya kwa NATO kufaidi mali hizo hata kidogo.

Naomba wenye kujua siasa za Libya,wanijuze hutyu jama hivi leo CNN,BBC nk wanamuita Dikteta amefanya makosa yapi hadi amepigwe kiasi hiki.

naomba majibu kama matatu ambayo yanafanya asitahili anachopata hivi sasa.

Wakati anazindua msikiti uganda aliutukana sana ukristo na kumtukana sana Yesu.haya ni mapigo kwa kumlaani Mungu.

Kidzude usitumie taarifa za mitaani, hakuna nchi isiyokuwa na masikini duniani mpaka sasa.

Kibona sijatoa taarifa yyoyote. Nimekwambia nipe statistics ya umaskini wa walibya na watanzania . Ratio ya daktari na wananchi, shule, huduma za maji si umaskini wa mtu mmoja mmoja hiyo siyo rating ya kimataifa. Ni kweli hata maskini wa marekani ana uwezo wa kumuliki gari je TZ.

Nimewahi kuongea hapo nyuma sababu mbalimbali za wazungu na wale wenye kuelewa demokrasia kwa kiasi cha juu kuivuruga nchi hiyo.

Muamar Gaddafi ameondolewa na raia wa Libya waliochoka na maisha waliyokuwa wakiishi ya umaskini, huku yeye na wale wote wanomzunguka wakiishi kama wako mbinguni.

Nchi hiyo inahodhi mafuta machafu ambayo hayajasafishwa bado kuwa mafuta ya aina mbalimbali kama petroli, doesel na mengine. Mafuta hayo yana thamani ya dola bilioni 40.

Libya ni nchi pekee Africa yenye kiasi hicho cha mafuta na ni nchi ambayo imelala karibu kabisa na lango kuu la kuingia bara la Ulaya.

Kama Tanzania ilivyofanya Azimio la Arusha mwaka 67, Libya nayo chini ya Gaddafi, ikataifisha visima vyote vya mafuta na sekta yote ya nishati na vikawa chini ya serikali ya Gaddafi, hiyo ilikuwa kwenye miaka ya sabini na makampuni yote ya mafuta ya kigeni ikiwemo BP ya Uingereza(ikumbukwe BP wana visima kwenye eneo la kilomita za mraba 54,000 au maili za mraba 21,000), na ENI ya Italy yalikuwepo kabla ya mapinduzi yaliyofanywa na Gaddafi lakini yalikuwa yakizungumza na mfalme Idris, hivyo wote wakatimuliwa.

Wakishiriana na Gaddafi nchi za UK, Italy, France na US waliweza kuchimba mafuta na UK walikuwa wakijishughulisha na ujenzi wa miundo mbinu yote ambayo umewahi kuiona pale Libya .

Walikuwa wakifanya watakavyo na hali hii haikuwafurahisha watu wa hali ya chini maana ni ukoo wa kifalme na watu wengine wa karibu ndio walokuwa wakifaidi.

Nchi zote za magharibi wamekuwa kwa miaka yote wakipanga namna ya kurudi Libya na ilikuwa ni nchi ya mwisho baada ya Egypt, Tunisia, Moroco, ingawa nchi za Bahrain, Syria na Algeria bado zimo kwenye ramani ya "targerts".

Kwa hiyo sababu kubwa ni kwamba nchi za magahribi zinahitaji access ya mafuta kwa urahisi zaidi bila vikwazo vya mikataba yenye masharti magumu. Pia gharama za mafuta zimekuwa kubwa mno na wananchi wamekuwa wakihoji serikali zao na uzalishaji wa mafuta umekuwa ukidorora kufikia kiasi cha mapipa 60,000 kwa siku badala ya milioni 1.6 kwa siku.

Nchi zote kubwa za Ulaya zinataka mafuta hayo na takwimu zinaonesha mpaka sasa kuna visima ambavyo havijachimbwa bado vyenye gharama ya dola bilioni 46.4

Halafu ukiangalia sana Gaddafi hakuchaguliwa kwa kura za wananchi, bali aliingia kwa nguvu za kijeshi.

kuchaguliwa kwa kura ni kitu kimoja na kuongoza nchi vizuri ni kitu kingine COMRADE CASTRO hakuchaguliwa kwa kura na HITLER alichaguliwa kura nyingi tu.kwa hio sio suala uliingiaje madarakani bali unafanya nini kwa watu wako ukishaingia madarakani.kwa suala libya ghadafi kaitoa libya kwenye umasikini mkubwa kwenda kwenye switzerland ya afrika.

Afrika ina utajiri mkubwa wa rasirimali kiasi hakuna nchi ya afrika inaweza kulinda rasilimali zake peke yake.ndo maana watu wanashangaa kugawa bure madini kwa wazungu.ukiwakatalia yanakukuta yaliyowakuta wote waliokataa kuibiwa mf.lumumba drc,kabila drc.kwame nkuruma ghana,kwa tunaishukuru ccm kwa kuliona hilo,mkitaka kuwaneemesha wananchi wenu km ghadafi yatawapata makubwa i luv ccm.

Afrika ina utajiri mkubwa wa rasirimali kiasi hakuna nchi ya afrika inaweza kulinda rasilimali zake peke yake.ndo maana watu wanashangaa kugawa bure madini kwa wazungu.ukiwakatalia yanakukuta yaliyowakuta wote waliokataa kuibiwa mf.lumumba drc,kabila drc.kwame nkuruma ghana,kwa tunaishukuru ccm kwa kuliona hilo,mkitaka kuwaneemesha wananchi wenu km ghadafi yatawapata makubwa i luv ccm.

Wewe lazima una ngozi ya chui na kondoo. Umenikitisha sana kwa kauli yako. TUPO PAMOJA THANK U.

Luxury, horror lurk in Gadhafi family compound - CNN.com

huyu ni muafrika mmoja tu, kuna wangapi ambao hatujui Gaddafi kawafanya nini?

Anayeweza kuelezea uovu wa Gadafi bila hata kuhangaika na vyombo vya nje ni Huyu Kiongozi wa REBELS ambaye muda wote alikuwa ni mushauri wa karibu wa gadafi na aliyepelekea haya yote kufanyika huku akiyaona hata bila ya kumpinga either kuresign au kukimbia nchi. Nadhani hata wale waliokuwa viongozi chini ya Gadafi wanalo lakujibu?.

Kampala
A Ugandan trapped in Tripoli has said rebels consolidating their hold on the Libyan capital are targeting, and killing, black Africans they suspect to have fought as mercenaries for Col. Muammar Gaddafi. "These black people came here to take up employment at oil fields, diplomatic missions and as domestic servants [but] the rebels are now killing them indiscriminately," the source told this newspaper yesterday by telephone from Tripoli.

"When they arrest any black person they suspect to be a fighter (mercenary), they force them to wear an army uniform and then mutilate them using swords and machetes."

Somalis, Eritreans, Ethiopians, Senegalese, Chadians and Nigerian nationals are the most affected, according to our source and human right groups. These revelations came as Col. Gaddafi, through regime spokesman Moussa Ibrahim, contacted the Associated Press by telephone, announcing that the Libyan leader, who is in hiding, is ready for talks with the insurgents he had mocked as "rats"!

The fighters, who have already overrun the presidential palace and are heading to capture Col. Gaddafi's Sirte home town, dismissed the suggestion as delusional. They said there is no basis for dialogue and the runaway dictator should surrender himself to face trial.

Yesterday's reports of increased xenophobic attacks energised AU lobbyists to intensify demands that only an all-inclusive transitional arrangement - but one that excludes Col. Gaddafi as agreed in Malabo, Equatorial Guinea on June 29 - would deliver true democratic dispensation to anxious Libyans, without widening tribal fissures and endangering its pivotal role on the continent.

The country's oil riches made it possible for Col. Gaddafi's crumbling regime to subsidise living for citizens and the stipends, combined with other lucrative opportunities, attracted African economic refugees, with some aiming to transit to Europe. But as the conflict intensified over its six-month course, reports, repeatedly denied by government officials, showed Col. Gaddafi drafted fighters from some friendly countries when it became clear NATO-supported rebels were determined to wrest power from him.

Mkuu nadhani unakumbuka uongo tuliozusha kuhusu Idd Amin mpaka leo watu wakisikia jina hilo wanaogopa. Jamaa anaitwa nduli na majina mengi kutokana na propaganda, lakini ukweli ni kwamba hakuwa mbaya kuliko Obote. Tumesikia kuwa TNC wanaongopa so inawezekana hii ni propaganda dhidi ya Gaddafi, inawezekana pia ni kweli na inawezekana pia kuwa si kweli. kwanini wasiseme kabla ya hapo?

Back
Top Bottom