Hivi GADAFFI amefanya kosa gani? Kwa Wa-Libya,Afrika na Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi GADAFFI amefanya kosa gani? Kwa Wa-Libya,Afrika na Dunia

Discussion in 'International Forum' started by Mathias Byabato, Aug 25, 2011.

1. Mathias Byabato

Mathias Byabato Verified User

#1
Aug 25, 2011
Joined: Nov 24, 2010
Messages: 905
Likes Received: 55
Trophy Points: 45
Naomba wenye kujua siasa za Libya,wanijuze hutyu jama hivi leo CNN,BBC nk wanamuita Dikteta amefanya makosa yapi hadi amepigwe kiasi hiki.
naomba majibu kama matatu ambayo yanafanya asitahili anachopata hivi sasa.

2. Mess

Mess JF-Expert Member

#2
Aug 25, 2011
Joined: Mar 2, 2009
Messages: 667
Likes Received: 4
Trophy Points: 35
Ila usimwambie mtu nikikuambia. Wazungu wanataka mafuta yake, ni sawa kwa jirani kuna wezi wanaiba harafu wewe unapiga story na watoto wako ndani mnacheka, hivyo ndiyo tulivyo sisi waafrica. Maana waasi ni watu wa kukodiwa hakuna waasi Libya. ni vile mwizi anakuibia then anaita watu akidai wewe ndo mwizi.

3. Mess

Mess JF-Expert Member

#3
Aug 25, 2011
Joined: Mar 2, 2009
Messages: 667
Likes Received: 4
Trophy Points: 35
ukiijua story ya Libya vizuri utalia kwa uchungu, kama ni waasi mtoto wa gadafi asingeweza kutoka nje na akazungumza na waandishi wa habari wa kigeni ambao wapo kwenye mji ambao wenyewe wanaandika habari kuwa umechukuliwa na waasi. mungu awalaaani wazunu .......

4. Baba_Enock

Baba_Enock JF-Expert Member

#4
Aug 25, 2011
Joined: Aug 21, 2008
Messages: 6,802
Likes Received: 164
Trophy Points: 160
1.. Amekaa madarakani kwa zaidi ya miaka 40 bila kuwa na usumbufu wowote (hakuna wabunge, madiwani, wala mkuu majeshi)!
2.. Amekuwa na chokochoko za kuitaka Africa kuwa nchi moja na hivyo kuwakosesha Wa-Marekani na marafiki zake mashamba ya bibi!
3.. Amekuwa akieneza kwa kasi sana uislamu kusini mwa jangwa la sahara
4.. Amelimbikiza pesa na mali nyingi sana barani Ulaya!

5. Mess

Mess JF-Expert Member

#5
Aug 25, 2011
Joined: Mar 2, 2009
Messages: 667
Likes Received: 4
Trophy Points: 35
Ukitaka kumpiga mtu lazima utafutize sababu, mzee mgabe amekaa muda gani madarakani? wako wengi ambao wamekaa muda mrefu lakini hawajawavamia. Mlipewa sababu za kizungu Iraq mkaona kuwa mmedanganywa kaka wakati wazungu wameshachukua na wanaendelea kuchukua mafuta kule. kuna msemo unasema no free lunch in America

6. ntagunga

ntagunga JF-Expert Member

#6
Aug 25, 2011
Joined: Aug 13, 2011
Messages: 507
Likes Received: 68
Trophy Points: 45
Kosa la Gaddafi, ni
1. kung'ang'ania madaraka baada ya raia wa Libya kuuchoka uongozi wake.

2. Kuwaita waliompinga ni mende na kunguni, na kutoa wito kwa majeshi yake kuwaangamiza.

3. kushindwa kuheshimu sauti na maoni ya wananchi wa liblya ya kuwa na uchaguzi utakaotoa fursa kwa walibya kuchagua viongozi wawapendao.

KAMA ANGEKUWA KIONGOZI WA WATU, ANGEANDAA MCHAKATO WA KUFANYA UCHAGUZI HURU, AMBAPO KAMA ANGEHITAJI KUENDELEA KUONGOZA LIBYA, BASI KURA ZA WANANCHI WAKE ZINGEAMUA. KI

KITENDO CHA YEYE KUKATAA MAPENDEKEZO YA WATU WAKE, KUONESHA NIA YA KUMWACHIA MADARAKA MWANAE NA KUWAITA WATU WANAOTAKA MABADILIKO NI MENDE NA KUNGUNI KUNATOSHA KUMWITA YEYE NI DIKTETA means ANT DEMOCRATIC.

HATA HIVYO SIKUBALIANI NA NCHI ZA KIGENI KUTUMA MAJESHI YAO, WANGEWAACHA WALIBYA WENYEWE WAFIKIE MABADILIKO WANAYOYAHITAJI BILA KUSAIDIWA NA WAGENI HARAMU. SIKU ZOTE MAENDELEO NI INTERNAL PROCESSES NA SIO EXTERNAL PROCESSES. WALIBYA WANA HATARI YA KUTOMUDU KUIONGOZA LIBYA BAADA YA GADDAF KWA KUWA WAMEMOUNDOA KWA MSAADA WA WAGENI, WAVAMIZI.

7. ntagunga

ntagunga JF-Expert Member

#7
Aug 25, 2011
Joined: Aug 13, 2011
Messages: 507
Likes Received: 68
Trophy Points: 45
Kosa la Gaddafi, ni
1. kung'ang'ania madaraka baada ya raia wa Libya kuuchoka uongozi wake.

2. Kuwaita waliompinga ni mende na kunguni, na kutoa wito kwa majeshi yake kuwaangamiza.

3. kushindwa kuheshimu sauti na maoni ya wananchi wa liblya ya kuwa na uchaguzi utakaotoa fursa kwa walibya kuchagua viongozi wawapendao.

KAMA ANGEKUWA KIONGOZI WA WATU, ANGEANDAA MCHAKATO WA KUFANYA UCHAGUZI HURU, AMBAPO KAMA ANGEHITAJI KUENDELEA KUONGOZA LIBYA, BASI KURA ZA WANANCHI WAKE ZINGEAMUA. KI

KITENDO CHA YEYE KUKATAA MAPENDEKEZO YA WATU WAKE, KUONESHA NIA YA KUMWACHIA MADARAKA MWANAE NA KUWAITA WATU WANAOTAKA MABADILIKO NI MENDE NA KUNGUNI KUNATOSHA KUMWITA YEYE NI DIKTETA means ANT DEMOCRATIC.

HATA HIVYO SIKUBALIANI NA NCHI ZA KIGENI KUTUMA MAJESHI YAO, WANGEWAACHA WALIBYA WENYEWE WAFIKIE MABADILIKO WANAYOYAHITAJI BILA KUSAIDIWA NA WAGENI HARAMU. SIKU ZOTE MAENDELEO NI INTERNAL PROCESSES NA SIO EXTERNAL PROCESSES. WALIBYA WANA HATARI YA KUTOMUDU KUIONGOZA LIBYA BAADA YA GADDAF KWA KUWA WAMEMOUNDOA KWA MSAADA WA WAGENI, WAVAMIZI.

8. Askari Kanzu

Askari Kanzu JF-Expert Member

#8
Aug 25, 2011
Joined: Jan 7, 2011
Messages: 4,526
Likes Received: 35
Trophy Points: 145
Ntagunga umenena (wanasemaga nipe tano!).

Ubishi wa Gaddafi usio na mpango umemponza. Watu wengi humu jamvini wanafikiria kama unampinga Gaddafi basi wewe ni kibaraka wa wakoloni. Hilo sio swala, viongozi wabishi ka Gaddafi ni watu wa kuteketezwa tu. Hiyo ndio dawa yao! Mie nshaona kuna jamaa humu hisia na hasira zimewazidi mpaka hekima imepotea. Kisa eti Gaddafi na utawala wake wa kidikteta umeangushwa. Duhu!

9. K

Kidzude JF-Expert Member

#9
Aug 25, 2011
Joined: Jul 14, 2011
Messages: 2,728
Likes Received: 333
Trophy Points: 180
mwenzako akinyolewa .....

10. Somoche

Somoche JF-Expert Member

#10
Aug 25, 2011
Joined: Oct 6, 2010
Messages: 3,825
Likes Received: 924
Trophy Points: 280
1. Makosa yake makuu ni kutaka kuunda African Monetary Fund
2. kuweka Pan -African Communication Satellite bure kwa Afrika na hivyo Waafrika wakaacha kulipa dola mil 500 kwa Ulaya na Marekani kwa kutumia satellite zao.
3. Kuwa na kiherehere cha kusema Afrika iwe moja na Jeshi moja
4. Kuzuia Mabeberu kujichukulia Mafuta ya Libya kama wanavyochukua dhahabu na Vitu vingne ikiwemo wanyama Kule Tanzania.
5.Kiherehere cha Kuanzisha African Bank na kutoa dola bil 90 kama mtaji
6. Kukataa kuwapigia Magoti wazungu kuhusu suala a Matumizi ya Dola anataka Afrika iwe na currency Moja
7.Kupinga Sudan Kusini kujitenga na hivyo kusababisha wazungu wakose mafuta Mengine ya bwerere

Yako Mengi ngoja kwanza nimpigie Simu Saif Islam Nimwellekeze la kufanya kwenye hii vita..nicheki tena baadae

11. p

punainen-red JF-Expert Member

#11
Aug 25, 2011
Joined: Nov 18, 2010
Messages: 1,735
Likes Received: 11
Trophy Points: 0

Nitajibu swali lako kuhusu Mugabe: Amekaa madarakani miaka 31... Na hata wangeanza na Mugabe ungekuja na swali hilihili kuwa Ghadafi amekaa mda gani na bila shaka ungepamba kuwa wamemwogopa ghadafi. Tulieni tu mnyolewe na mjanja mwenye nguvu, hata nyie mngejaaliwa na Mungu nguvu za hivo mngekuwa mnawakong'oli tu wale msiowapenda!!

12. Richard

Richard JF-Expert Member

#12
Aug 25, 2011
Joined: Oct 23, 2006
Messages: 8,253
Likes Received: 4,275
Trophy Points: 280
Nimewahi kuongea hapo nyuma sababu mbalimbali za wazungu na wale wenye kuelewa demokrasia kwa kiasi cha juu kuivuruga nchi hiyo.

Muamar Gaddafi ameondolewa na raia wa Libya waliochoka na maisha waliyokuwa wakiishi ya umaskini, huku yeye na wale wote wanomzunguka wakiishi kama wako mbinguni.

Nchi hiyo inahodhi mafuta machafu ambayo hayajasafishwa bado kuwa mafuta ya aina mbalimbali kama petroli, doesel na mengine. Mafuta hayo yana thamani ya dola bilioni 40.

Libya ni nchi pekee Africa yenye kiasi hicho cha mafuta na ni nchi ambayo imelala karibu kabisa na lango kuu la kuingia bara la Ulaya.

Kama Tanzania ilivyofanya Azimio la Arusha mwaka 67, Libya nayo chini ya Gaddafi, ikataifisha visima vyote vya mafuta na sekta yote ya nishati na vikawa chini ya serikali ya Gaddafi, hiyo ilikuwa kwenye miaka ya sabini na makampuni yote ya mafuta ya kigeni ikiwemo BP ya Uingereza(ikumbukwe BP wana visima kwenye eneo la kilomita za mraba 54,000 au maili za mraba 21,000), na ENI ya Italy yalikuwepo kabla ya mapinduzi yaliyofanywa na Gaddafi lakini yalikuwa yakizungumza na mfalme Idris, hivyo wote wakatimuliwa.

Wakishiriana na Gaddafi nchi za UK, Italy, France na US waliweza kuchimba mafuta na UK walikuwa wakijishughulisha na ujenzi wa miundo mbinu yote ambayo umewahi kuiona pale Libya .

Walikuwa wakifanya watakavyo na hali hii haikuwafurahisha watu wa hali ya chini maana ni ukoo wa kifalme na watu wengine wa karibu ndio walokuwa wakifaidi.

Nchi zote za magharibi wamekuwa kwa miaka yote wakipanga namna ya kurudi Libya na ilikuwa ni nchi ya mwisho baada ya Egypt, Tunisia, Moroco, ingawa nchi za Bahrain, Syria na Algeria bado zimo kwenye ramani ya "targerts".

Kwa hiyo sababu kubwa ni kwamba nchi za magahribi zinahitaji access ya mafuta kwa urahisi zaidi bila vikwazo vya mikataba yenye masharti magumu. Pia gharama za mafuta zimekuwa kubwa mno na wananchi wamekuwa wakihoji serikali zao na uzalishaji wa mafuta umekuwa ukidorora kufikia kiasi cha mapipa 60,000 kwa siku badala ya milioni 1.6 kwa siku.

Nchi zote kubwa za Ulaya zinataka mafuta hayo na takwimu zinaonesha mpaka sasa kuna visima ambavyo havijachimbwa bado vyenye gharama ya dola bilioni 46.4

Halafu ukiangalia sana Gaddafi hakuchaguliwa kwa kura za wananchi, bali aliingia kwa nguvu za kijeshi.

13. Mathias Byabato

Mathias Byabato Verified User

#13
Aug 25, 2011
Joined: Nov 24, 2010
Messages: 905
Likes Received: 55
Trophy Points: 45
mbona hakuna rais yeyote wa agrika anayekemea hali hii

14. VUVUZELA

VUVUZELA JF-Expert Member

#14
Aug 25, 2011
Joined: Jun 19, 2010
Messages: 3,106
Likes Received: 11
Trophy Points: 135
Hapo ndio watu mkae mkijua nchi kama China, Venezuela, Russia ana Iran ni wanafiki wakubwa. Rafiki yao Ghadafi anakula kichapo hadi anaaibishwa wao wamekaa pembeni. Uwezo wanao so kwa nini wasimsimamishe NATO?
China wanachojali ni kuganga njaa zao. Juzi walikuwa marafiki wa Ghadafi kesho mtasikia Beijin wamesign trade deals na Rebels.
Heri huyo mmarekani anayejulikana ana msimamo gani kuliko China, Russia na Iran ambao sio marafiki wa kweli

15. Askari Kanzu

Askari Kanzu JF-Expert Member

#15
Aug 25, 2011
Joined: Jan 7, 2011
Messages: 4,526
Likes Received: 35
Trophy Points: 145
...wewe anza kutia maji!

Wahenga walisema.

16. H

Hofstede JF-Expert Member

#16
Aug 25, 2011
Joined: Jul 15, 2007
Messages: 3,584
Likes Received: 32
Trophy Points: 0
Mkuu hizi habari zako umezipatia kwenye vijiwe vya kahawa nini?,
Facts:
1. Kabla ya vurugu kuanza 80% of Libya's oil was exported to Europe
2. Waasi ni wananchi wa Libya + deffected soldiers and govt officials
3. Gaddafi anatumia askari wa kukodi (mercenaries)

17. HT

HT JF-Expert Member

#17
Aug 25, 2011
Joined: Jul 29, 2011
Messages: 1,899
Likes Received: 3
Trophy Points: 0
wote mnaosema Gaddafi ameondolewa na wananchi wa Libya aidha ni waongo au hamjui mnachosema.

18. Richard

Richard JF-Expert Member

#18
Aug 25, 2011
Joined: Oct 23, 2006
Messages: 8,253
Likes Received: 4,275
Trophy Points: 280
Mkuu sasa wewe unadhani ameondolewa na nani?

Maana tunajaribu kuelimishana.

Kusema au kumwambia mwenzio muongo halafu wewe mwenyewe hutoi maoni yako kunaonesha upungufu wa uelewa ulio nao.

19. N

Nonda JF-Expert Member

#19
Aug 25, 2011
Joined: Nov 30, 2010
Messages: 13,223
Likes Received: 1,958
Trophy Points: 280
Gaddafi hakufanya kosa ila alifanya ushujaa na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yake.
Sasa kama kuwa mzawa na mzalendo kwa nchi na wananchi wa nchi yake ni kosa basi hilo ndilo alilolifanya.

Gaddafi amekataa kwa miaka 42 kuiweka rehani Libya. Amewaweka vultures at bay, hakuruhusu majambazi, wizi,wanafiki wa West kujinufaisha na maliasili na rasilimali za Libya.

Gaddafi amekataa kununuliwa na "economic hitman" na hivyo kuwa kikwazo kwa wazungu na wamarekani wanaongozwa kwa remote control na International bankers kukomba utajiri wa Libya.

Gaddafi pia alikuwa amejitayarisha kuanzisha mfumo wa fedha na mabenki ya Afrika na hivyo World bank na IMF vingekosa wateja wake wa Afrika ambazo matokeo yake ni nchi za kiafrika kuibiwa na kufukarishwa.

Kwa hiyo kumuondoa Gaddafi, kutaleta serikali kibaraka, itaua au kuihasi AU na itawezesha US na West kujikombea wakitakacho Libya na kuendelea kujitwalia wanavyovitaka katika nchi nyengine za Afrika.

Kwa ufupi ni mchezo mchafu wa West na US na hakuna hata harufu ya utashi wa demokrasia au kulinda raia.

Tembelea hapa Lizzie Cocker talks to Canadian woman living in Tripoli, Libya - YouTube

20. jmushi1

jmushi1 JF-Expert Member

#20
Aug 25, 2011
Joined: Nov 2, 2007
Messages: 17,568
Likes Received: 1,935
Trophy Points: 280
In the ruins of Gadhafi's lair, rebels find album filled with photos of his 'darling' Condoleezza Rice[/h]David R Arnott writes
The ransacking of Moammar Gadhafi's compound is turning up some bizarre loot. Following on from the Libyan leader's eccentric fashion accessories and his daughter's golden mermaid couch, the latest discovery is a photo album filled with page after page of pictures of Condoleezza Rice.
[​IMG] Ammar Abd Rabbo / Abaca
Rebels examine a photo album of former U.S. Secretary of State Condoleezza Rice, which was found in Moammar Gadhafi's Bab al-Aziziya compound in Tripoli, Libya, on August 24.

The former U.S. Secretary of State paid a visit to Tripoli in 2008 during a brief interlude that saw Gadhafi begin to be welcomed back into the international fold. As Jason Ukman of the Washington Post wrote on Wednesday, "it was only three short years ago that Rice shared a late-night dinner with Gaddafi to break the Ramadan fast, three short years ago that the United States and Libya were celebrating what was to be a new chapter in their relations."
In a 2007 interview with al-Jazeera television, Gadhafi spoke of Rice in glowing terms. "I support my darling black African woman," he said. "I admire and am very proud of the way she leans back and gives orders to the Arab leaders ... Leezza, Leezza, Leezza. ... I love her very much. I admire her and I'm proud of her because she's a black woman of African origin."
[​IMG] Mahmud Turkia / AFP-Getty Images, file
Moammar Gadhafi poses with Condoleezza Rice prior to a meeting in Tripoli on September 5, 2008. Rice's was the first such visit in more than half a century, marking a new chapter in Washington's reconciliation with the former enemy state.

AP photographer Sergey Ponomarev was with the rebels as they flicked through the album in the Bab al-Aziziya complex on Wednesday. "There were lots of rebels celebrating their victory," Ponomarev said. "It was still unsafe - loyalists were shelling the compound from time to time - but rebels were celebrating the seizure of the Gadhafi compound. They believe the victory is in their hands. Some of them even brought their children to the scene."
[​IMG] Sergey Ponomarev / AP
Rebel fighters look through a photo album they found inside Moammar Gadhafi's compound on August 24

Loading...