Hivi EWURA ni shirika la umma ama la binafsi!

asha ngedere

Member
Nov 6, 2009
92
11
Jamani ndugu zangu, mimi napenda kuuliza kama EWURA, yaani mamalaka ya kudhibiti matumizi ya maji na nishati, ni shirika la binafsi au liko chini ya serikali. hii ni kwa sababu ya taarifa fulani ambazo niliwahi kuzisikia kwamba wanaoliongoza wanajineemesha kwa safari nyingi za nje. samahani kama nitakuwa nimepitwa na wakati, lakini kuuliza ndiko kujua, ati!
 
Liko chini ya serikali.na kuhusu safari za nje nadhani wamepewa ruhusa na serikali yenyewe kwa sababu hiyo bajeti ya pesa za kwenda nje si ilipitishwa na Bunge tukufu? na wizara husika nayo imebariki.
 
Basi kama ndivyo hii nchi inaendelea kufilisika, maana nasikia hizo bajeti zao, ni kufuru tupu.
 
EWURA wana 1% kwa kila bili ya maji, bili ya TANESCO na kila lita moja ya mafuta inayouzwa NCHI nzima. Na hii asilimia moja inalipwa na mtumiaji sio hizi kampuni. Niambie mapesa haya yote watayatumiaje.
Tungekuwa na mpango kama huo kwenye ELIMU, MATIBABU, UMASIKINI, maisha bora kwa kila MTZ yangewezekana
 
Misuse of resources,na hicho cha maana wanachotufanyia wa TZ ni kipi? bora pesa hizi wangepewa walimu waboreshe elimu.
 
Back
Top Bottom