Hivi EWURA iko kuwasaidia wavuja jasho na walalahoi au kujinufaisha wakubwa?

  • Thread starter Kungetafiti Kaniki
  • Start date

K

Kungetafiti Kaniki

New Member
Joined
Dec 4, 2012
Messages
1
Points
0
K

Kungetafiti Kaniki

New Member
Joined Dec 4, 2012
1 0
Watanganyika wenzangu hebu nisaidieni kujua kazi ya EWURA, maana naona inawanyonya watanganyika wenzangu kwa maana katika maazimio yao ni kuwatetea walaji wanyonge na kusimamia masilahi ya watanganyika wenye kipato kidogo kama ilivyoainishwa kwenye mipango mikakati yao.

Lakini, ukiangalia kiundani zaidi unaona kabisa kuwa inawanyonya watanganyika wavuja jasho badala ya kuwasaidia. Hii nasema kwa sababu, inakusanya kamission kutoka kwenye maji ambayo mtanganyika mvuja jasho hayapati kabisa lakini bili ya maji anapata na kukomaliwa kuilipa bila huduma, pili kwenye umeme wanapata commission ambapo kila siku bei inapanda na hakuna jitihada zinazofanywa na EWURA kusimamia hiyo bei, ya mwisho ya kukamuliwa kwa wavuja jasho ni kwenye mafuta ambapo kila wenye rungu(Matajiri) wakiamua kupandisha wanapandisha. Mbaya zaidi hiyo EWURA kila siku inatanagaza bei ya mafuta kwenye magazeti ambayo gazeti moja tu inakula si chini ya million mbili kwa tangazo moja tu na mnyonge hawezi kulinunua hilo gazeti. Hivi inamaana kuwa iliundwa kwa kutangaza au kusimamia watanganyika wanyonge?

zamani wakati wa tume ya bei ilipokuwepo, bei ilikuwa inapanda baada miaka mingi, lakini EWURA inapandisha hata baada ya siku mbili na kuitangaza kwenye magazeti kwa kutumia pesa za wanyonge ambao hata kununua hiyo gazeti ni shida. Hii inasaidia nini wenzangu. Hebu tuwe wazalendo kwa kutetea wanyonge.

EWURA inasimamia Umeme, Maji, Mafuta, Gasi. Nchi yetu iko kwenye soko huria, kusimamia bei ni vigumu ndo maana tume ya bei ilivunjwa. Ndo maana EWURA inaamuliwa na matajiri ambao wakiamua kupandisha bei wanapandisha bila kipingamizi chochote.

Kwa kuwa nchi iko kwenye mchakato wa kutafuta gasi basi EWURA ibaki tu na Gasi ambayo itakuwa kwa matajiri tu.

Tuungane kuwatetea na kulinda masilahi ya wanyonge na kuendeleza nchi yetu.

Hebu fikiria kila mtanganyika, kwenye maji, umeme, mafuta, gasi analipa kwa EWURA ambayo kwa maoni yangu hamsaidii mtanganyika maskini ila inamnyonya kwa kiwango kikubwa.

Hebu chukulia mfano, Mtanganyikaa huyu, kwenye umeme atalipa (Ushuru yaani TRA, Tanesco, Service line, EWURA, n.k) Maji atalipa (Ushuru yaani TRA, Dawasco kama DSM, Service line EWURA N.K) Mafuta kadhalika. Hebu fikiria huyu EWURA anapata kiasi gani kwa mwezi kwa ajili ya manufaa yake tu.

Nahitimisha kwa kusema kama kuna mtu anajua vizuri kazi ya EWURA mbele ya wanyonge basi anieleweshe ili nisikirie vibaya, lakini kama ni kweli wanamnyonya mnyonge basi naomba tuungane kutetea wanyonge wapate nafuu ya maisha maana Umeme, maji, mafuta ni vitu muhimu kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu (mtanganyika)


Asanteni

Kungetafiki Kaniki
 

Forum statistics

Threads 1,285,256
Members 494,502
Posts 30,855,589
Top