Hivi eti aliyetungua ndege ya akina Habyarimana hajulikani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi eti aliyetungua ndege ya akina Habyarimana hajulikani?

Discussion in 'International Forum' started by Magezi, Nov 19, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kila mara najiuliza hivi ni kweli ndege iliyowaua akina Habyarimana na rais wa burundi wakati ule ilitunguliwa kweli na RPF au ni uzushi tu. Na kama RPF waliitungua ndege hiyo je wamechukuliwa hatua gani??
   
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maraisi wa Rwanda. Burundi na Uganda waliokuwa waondoke na ndege moja lakini mipango ilipangwa kuwaondoa hawa jamaa kwani walikuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa M7 kutimiza mipango yako.

  Hivi unajua kwamba hata Samora machel wa msumbiji ndege yake ilitunguliwa kwa makusudi kabisa ya kumwondoa hapa duniani?.
   
 3. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Habyarimana alijitungua mwenyewe bila kujua. Pale DSM alimwamuru Rais wa Burundi apande falcon ya Rwanda ili wawe na mazungumzo hadi Kigali, kisha ndege ya Burundi ikatangulia kwenda ili iwasubiri Kigali. Habyalimana alipiga simu Kigali na kuamuru ndege hiyo ikifika itunguliwe bila kutoa maelezo. Bahati njema ya ndege hiyo ilibadili mpango angani kwa mari ya Mkuu wa Majeshi wa burundi aliyemwamuru rubani aende Bujumbura na kumshusha kisha arudi Kigali kumchukua rais Ntayamirwa. Hii ina maana ndege ya kwanza kuingia Kigali ilikuwa iliyowabeba marais, na walinzi wa Kibelgiji walitekeleza amri waliyopewa bila kusita.

  Imekaaje hii?
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  It does not make sense. Lakini kumbuka interahamwe na mipango iliyokuwa imeandaliwa kuua"inyenzi." Sasa ghafla zinatangazwa habari kutoka Dar kuwa Habyarimana amekubali kushirikiana na RPF.Wale wanajeshi waliopewa mafunzo ya kuwaua Watusi wangefanyaje? Walimwona rais wao amewasaliti.
   
 5. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Yeah, ni kweli wale interahamwe wa msimamo mkali waliona kuwa Habyalimana amewasaliti, na mpaka leo ninaamini kuwa hata bila kutunguliwa kwa ndege, walikuwa wanaenda kumwua huko nyumbani.

  Lakini, yeye pia alikuwa alikuwa na mpango wa kuwamaliza watusi waliokuwa wanamnyima pumzi katika shuttle diplomacy ya Arusha. Siku hiyo aliona chance maana Mkuu wake wa majeshi wa Burundi (Mtusi) na maafisa wake waliokuwa na damu ya Kitusi aliwapakia ndani ya ndege ya Burundi na kuwaamuru watangulie Kigali, huku maafisa wa Kihutu wa Burundi na Rwanda wakipakiwa ndani ya Falcon yake. Lengo lilikuwa ni kutungua ndege ya Burundi inapotua Kigali ili kuwamaliza Watusi wa pande zote mbili. Mkuu wa majeshi wa Burundi akiwa amelewa bia za tanzania ndiye aliokoa jahazi kwa kuamuru ndege iende kwanza Bujumbura na ndipo irudi Kigali.
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ina maana alimuru wamuue mkuu wa majeshi? soma tena paragraph yako nimesoma mara tatu nashindwa kuelewa. alitaka ndege ipi itunguliwe? iliyokuwa nani ndani? ambayo ingekuwa inatokea wapi muda huo? itatunguliwa ikiwa wapi? Kuna kitu cha maana kwenye paragraph yako lakini nakosa link
   
 7. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mbogela
  Soma mchango wangu uliopita hivi punde utaelewa. Nifupishe tena kwa kusema, ubaguzi ndio uliommaliza Habyalimana, maana aliwabagua watusi na kuwapakia kwenye ndege ya rais wa Burundi huku Wahutu akiwapakia katika ndege yake (Falcon). Kisha akaamuru ya Burundi itangulie Kigali kumsubiri rais wa Burundi. Ilipoondoka Dar akapiga simu kuamiru kikosi maalum pale kigali kitungue ndege hiyo ya kwanza kuingia bila kutoa sababu. Ikiwa angani, ndege hiyo iliamuriwa na Mkuu wa majeshi wa Burundi (Mtusi) iende Bujumbura kwanza na baadaye irudi Kigali kumchukua Rais. Maana yake hapa ni kuwa Falcon ilikuwa ya kwanza kuingia Kigali, na kikosi maalum kikatekeleza amri bika kuuliza. Ndege ya Burundi iliporudi kuja kumchukua rais Ntayamirwa ilikuta uwanja unawaka moto, ikarudi tena Bujumbura.

  Kama movie vile!
   
 8. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Je watunguaji wameshafikishwa kwenye mkono wa sheria Arusha?
   
 9. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Watunguaji wengi walikuwa ni wabelgiji (Kikosi Maalum-uwanjani kanombe), na baadhi yao waliuawa na Interahamwe baada ya ndege kutunguliwa bila kujua kuwa waliamuliwa na Habyalimana mwenyewe. Ukifika Kigali utaona hata mahali walipouawa hao maaskari wa Kibelgiji.
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Paul Kagame anajua sana ni nani alimwua Habyarimana, Imar Kombe alikuwa anajua kabisa nani aliyemwua Habyarimana. Aliyetungua ndege si wa maana sana, wa muhimu ni yule aliyotoa amri ya kutungua hiyo ndege ambaye mpaka sasa bado yupo na anaishi.

  Lakini Habyarimana sasa ni historia, lakini Interahamwe watarudi tena mika 10 au 15 ijayo, kuna ndugu zao wengi walifyekwa na Kagame na sasa wanaishi kama wakimbizi huko Congo. Sasa hivi wanatunga sheria tu, wanaweza kurudi kwa nguvu kama walivyokuja RPF.
   
 11. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Usemalo ni kweli ndugu yangu. Vicious circle haijakamilika bado. Interahamwe wako nje ya system. Watarudi na hapo Inyenzi watakuwa nje. Ubaguzi ni kansa ya hatari sana.

  Lakini suala la muuaji wa Habyalimana, hilo nasita kukubaliana nawe. That was accidental suicide. It does not matter who pulled the trigger, but who ordered the trigger to be pulled. It is at least reasonable to believe Habyalimana ordered it. Who else?
   
 12. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Si kweli Rais Ntaryamila wa Burundi alishauriwa asiondoke na Ndege yake kwa sababu za kiusalama kwa wakati huo wa jioni, ndipo alipopewa lift na Habyalimana. Wakati wakiondoka Dar makubaliano yalikuwa ashushwe kwanza Rais wa Burundi mjini Bujumbura ndo Habyalimana aende Kigali.
  Wakiwa njiani wao walibadili utaratibu ambao ndo kwanza ulikuwa umewekwa wakiwa Dar.
   
 13. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Kama ni hivyo kwa nini ndege ya Burundi ilitua Bujumbura, kisha ikarudi Kigali? Ilifuata nini ikiwa ilikuwa na matatizo ya kiusalama au kama kulikuwa na sababu za kiusalama? na kwa nini baadhi ya maafisa wa Rwanda walishushwa kwenye falcon na kupandishwa ndani ya ndege ya Burundi?

  Kuna mengi tumegee!
   
 14. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ah!! Na ile ndege ya Rais wa Rwanda pale Airwing JWTZ inafanya nini si ndio ilikuwa imeharibika ndio maana wakapanda ndege moja? Kwani ndege ile ni ya Rais wa Rwanda ilileta Itilafu ndio maana wakapanda ndege ya Burundi ndio ilitunguliwa kwani haya maelezo yako hayajakaa vyema nenda pale Airwing waombe uione ndege ya Rais wa Rwanda kisha andika tena. ok um esikia wewe Baija Bolob.i
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  haya maelezo hayaeleweki hebu rudia rudia kuweka mambo sawa labda tutakuelewa
   
 16. E

  Ex-Fisadi Member

  #16
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubaguzi ni mbaya. Mauwaji ya Rwanda bado yanaendelea, Kagame anaua Wahutu kama nzige, utawala wa Habyarimana uliua Watutsi kama mende. Wote wanauana ili Kagame ni mshenzi zaidi maana anjua propaganda kuliko wahutu. Kagame alimuua habyarimana na ametoa amri kwa jeshi lake kuwamaliza Wahutu wote waliosoma. Ebu fikiria hili, kuna Ofisa wa Ubalozi wa Rwanda aliyekuwepo hapa Dar es salaam tangu mwaka 1992 hadi Kagame anakamata nchi. Lakini bwana huyu sasa anatfutwa eti alihusika na mauaji ya halaiki. Mwaka 1996, aliitwa arudi nyumbanii akakataa akatorokea katika mitaa ya Dar es salam maana alijua akienda Kigali utakuwa ndio mwisho wake. lakini propaganda za RPF ni kuwa yeye ni sehemu ya nzige ambao kwa kukataa kurudi Kigali anajua alichokifanya na wanamtafuta kwa udi na uvumba kama mhusika wa mauaji ya kimbari!! Kagame muuaji lakini dunia haijui!!!! ana mkakati wa kumaliza Wahutu.
   
 17. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Yeah, Kagame kwa sasa ni shujaa na kipenzi cha wengi. Hata mimi namkubali kwa positive dictatorship yake. Ana nguvu kuliko anayoiongoza. Anastahili hata kuiongoza Bongo yetu kwa mafanikio makubwa. Kwa suala la Hutu/Tusi hapo ndipo anachemsha. Amezungukwa na Ultra discriminators watupu. Akiwasikiliza anawamaliza wahutu. Asipowasikiliza, wahutu wanammaliza.
   
 18. E

  Ex-Fisadi Member

  #18
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa propaganda anafaa kuongoza Tanzania lakini mikono yake imejaa damu ya Wahutu hafai hata kidogo. Kwa tanzania Mafisadi wangemkoma kama wahutu wanavyomkoma.
   
 19. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135

  Hiyo Itakuwa Genocide Ya kutisha Kuliko Ile ya '94
  Ee Mungu Okoa Rwanda
   
 20. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Na Vipi Kuhusu Melchior Ndadaye??

  [​IMG]
   
Loading...