Hivi Ester Matiko ana chuki gani na Chato/Geita?

Makusudically

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
2,201
1,232
Ninasikitishwa mno na Malalamiko ya Mh.Mbunge huyu, Je sisi watu wa Chato siyo Watanzania? Hatuna thamani? Madai ya kuwa ni "Misuse of resources" haoni kuwa ni matusi? Kwa wananchi wa Chato ni Misuse of resources? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.

======

Akichangia, mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko alisema kuweka taa za barabarani katika mji wa Chato ni matumizi mabaya ya fedha za umma. "Tumeona traffic light (taa za barabarani) Chato. Kuna miji ina msongamano wa magari ninyi mnaenda kujenga Chato?" alihoji Matiko.

Alisema Chato haina msongamano wa magari na kuna picha aliona punda wakivuka katika taa hizo japo hana uhakika kama ilikuwa Chato lakini akasema hayo ni matumizi mabaya ya fedha.Mbali na suala hilo, alisema hata ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege Chato haukustahili bali uwanja wa aina hiyo ungejengwa Dodoma.

Matiko alisema kama uwanja huo ungejengwa Dodoma, hata ndege kubwa inayombeba Rais wa Marekani, Donald Trump ingeweza kutua badala ya Rais Magufuli kulazimika kwenda Dar es Salaam kumpokea endapo atafanya ziara nchini.

Alisema badala ya Serikali kutumia Sh39 bilioni kujenga uwanja huo, ni vyema fedha hizo zingejenga hospitali kubwa Chato au kujenga chuo kikuu eneo hilo. Kwa mujibu wa Matiko, Chato kungeweza kujengwa uwanja mdogo ambao utawezesha kutua ndege kama Bombadier na uwanja mkubwa ujengwe Dodoma.
 
Hana chuki, anauliza Bajeti ya Ujenzi wa uwanja ilipangwa na Nani? Wao Kama Bunge walipitisha bilioni 2, lakini mpaka Leo imetumika bilioni 36,
Ni Nani aliyepitisha hizo Pesa?

Jibuni swali Acheni kupotosha ukweli,
Kiongozi hata kama zikipitishwa Trilion 1,000 shida iko wapi kama Uwanja huo ni kwa manufaa ya Watanzania wote, kana faida ni kwa kikundi cha watu au mtu mmoja hapo litakuwa kosa baya na kubwa sana. Tuache Ushabiki, Uwanja wa KIA mbona fedha yake haikupitishwa na Bunge na bado hakuna anayelalamika? Tuache Ubaguzi wa Ukanda.
 
Sikia Mkuu, yaani hapa kinachotakiwa ni kufuata Bajeti, Mwaka huu tunataka kujenga Daraja Fulani na Barabara Fulani Bunge linapitisha PESA, sasa kinachohojiwa, ni Nani aliyepitisha PESA kujenga uwanja huu?

Unajua hatufanyi kitu chochote hasa kinachohusu Pesa bila kupitishwa Bungeni, Bajeti.

Mkuu hapo ndipo shida ilipo
 
kama taa za barabarani wanavuka punda huo uwanja si ndio mtafugia mbuzi kabisa? haya ni matumizi mabaya ya kodi za watanzania
Mawazo ya jinsi hii yanafaa yatolewe na Mi-Chadema tu siyo mtu mwenye busara kama wewe.
 
Ninasikitishwa mno na Malalamiko ya Mh.Mbunge huyu, Je sisi watu wa Chato siyo Watanzania? Hatuna thamani? Madai ya kuwa ni "miss use of resources" haoni kuwa ni matusi? Kwa wabanchi wa Chato ni miss use of resources? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.
Hana chuki Mh mbunge,anataka majibu,hata vikijengwa viwanja,mia vya ndege,hapo chato,
Kama taratibu za sheria,uchumi,zimefuatwa hakuna shida
 
Swali ni , Je! Hizo fedha zimeidhinishwa kwa bajeti iliyoko?? Msiwe na hasira mtu akiwauliza swali jamani. Kwani kikao cha bajeti kazi yake ni kwenda kuambiwa mlizotumia au mnazoomba kwenda kutumia. Ijulikane zitapatikanaje na mtumie kiasi gani. Hizo 2 billion kwanini mkaziomba?? Mngepeleka bungeni hayo maombi kwani ingelikuwa dhambi??
 
Kiongozi hata kama zikipitishwa Trilion 1,000 shida iko wapi kama Uwanja huo ni kwa manufaa ya Watanzania wote, kana faida ni kwa kikundi cha watu au mtu mmoja hapo litakuwa kosa baya na kubwa sana. Tuache Ushabiki, Uwanja wa KIA mbona fedha yake haikupitishwa na Bunge na bado hakuna anayelalamika? Tuache Ubaguzi wa Ukanda.

Unaweza kuthibitisha kuwa fedha za kujenga KIA hazikupitishwa na bunge?
 
Hana chuki, anauliza Bajeti ya Ujenzi wa uwanja ilipangwa na Nani? Wao Kama Bunge walipitisha bilioni 2, lakini mpaka Leo imetumika bilioni 36,
Ni Nani aliyepitisha hizo Pesa?

Jibuni swali Acheni kupotosha ukweli,
hizo ni zile kakusanya kwa matapeli haziwekwi kwenye bajeti
 
Hana chuki, anauliza Bajeti ya Ujenzi wa uwanja ilipangwa na Nani? Wao Kama Bunge walipitisha bilioni 2, lakini mpaka Leo imetumika bilioni 36,
Ni Nani aliyepitisha hizo Pesa?

Jibuni swali Acheni kupotosha ukweli,
duuuuu kumbe ndo hivyo?
 
Ninasikitishwa mno na Malalamiko ya Mh.Mbunge huyu, Je sisi watu wa Chato siyo Watanzania? Hatuna thamani? Madai ya kuwa ni "miss use of resources" haoni kuwa ni matusi? Kwa wabanchi wa Chato ni miss use of resources? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.
Ukweli ni ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa huko ni misuse of resources, hajakosea kitu.
 
Sikia Mkuu, yaani hapa kinachotakiwa ni kufuata Bajeti, Mwaka huu tunataka kujenga Daraja Fulani na Barabara Fulani Bunge linapitisha PESA, sasa kinachohojiwa, ni Nani aliyepitisha PESA kujenga uwanja huu?

Unajua hatufanyi kitu chochote hasa kinachohusu Pesa bila kupitishwa Bungeni, Bajeti.

Mkuu hapo ndipo shida ilipo
Kwa hiyo all of a sudden ishu ni budget na sio location tena???
 
Back
Top Bottom