Makusudically
JF-Expert Member
- Feb 3, 2014
- 2,201
- 1,232
Ninasikitishwa mno na Malalamiko ya Mh.Mbunge huyu, Je sisi watu wa Chato siyo Watanzania? Hatuna thamani? Madai ya kuwa ni "Misuse of resources" haoni kuwa ni matusi? Kwa wananchi wa Chato ni Misuse of resources? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.
======
Akichangia, mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko alisema kuweka taa za barabarani katika mji wa Chato ni matumizi mabaya ya fedha za umma. "Tumeona traffic light (taa za barabarani) Chato. Kuna miji ina msongamano wa magari ninyi mnaenda kujenga Chato?" alihoji Matiko.
Alisema Chato haina msongamano wa magari na kuna picha aliona punda wakivuka katika taa hizo japo hana uhakika kama ilikuwa Chato lakini akasema hayo ni matumizi mabaya ya fedha.Mbali na suala hilo, alisema hata ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege Chato haukustahili bali uwanja wa aina hiyo ungejengwa Dodoma.
Matiko alisema kama uwanja huo ungejengwa Dodoma, hata ndege kubwa inayombeba Rais wa Marekani, Donald Trump ingeweza kutua badala ya Rais Magufuli kulazimika kwenda Dar es Salaam kumpokea endapo atafanya ziara nchini.
Alisema badala ya Serikali kutumia Sh39 bilioni kujenga uwanja huo, ni vyema fedha hizo zingejenga hospitali kubwa Chato au kujenga chuo kikuu eneo hilo. Kwa mujibu wa Matiko, Chato kungeweza kujengwa uwanja mdogo ambao utawezesha kutua ndege kama Bombadier na uwanja mkubwa ujengwe Dodoma.