Hivi Ester Matiko ana chuki gani na Chato/Geita?

Nadhani haujaelewa hoja kuu ya mleta mada. Yeye analalamikia mbunge kusema kujengwa uwanja wa ndege Chato ni "misuse of resources" kana kwamba walioko huko chato hawana thamani ya kuweza kupata huo uwanja. Hajalalamikia kuhojiwa kwa fungu la huo ujenzi kwenye bajeti.
Kwa hakika wewe ni moja kati ya watu wenye uelewa wa hali ya juu kabisa, mantiki ya mada hiyo kuhusu kauli ya "mis use of resources" nini maana yake halisi? Ikumbukwe kila jamii inayo haki yakutumia resources za nchi hii equally. Suala la bunge kutopitisha fedha au kuzidisha kile kilichopitishwa hakiwezi kuwa mis use, bali ni mis appropriation" kauli ya mbunge huyu mi naiona ni dharau na kuwajengea chuki watu wa eneo hili.
 
Kiongozi hata kama zikipitishwa Trilion 1,000 shida iko wapi kama Uwanja huo ni kwa manufaa ya Watanzania wote, kana faida ni kwa kikundi cha watu au mtu mmoja hapo litakuwa kosa baya na kubwa sana. Tuache Ushabiki, Uwanja wa KIA mbona fedha yake haikupitishwa na Bunge na bado hakuna anayelalamika? Tuache Ubaguzi wa Ukanda.
Tutajie KIA ilijengwa mwaka gani na madhumuni yake yalikuwa yapi. Kama hutapata majibu hayo mawili basi endelea na kulalamikia mambo ya Chato. Tueleze manufaa watakayopata waTanzania kwa kujengwa uwanja wa Chato.
 
Hata kama utalalamika hadi uzimie; UWANJA WA NDEGE LAZIMA UJENGWE CHATO,NARUDIA LAZIMA UJENGWE CHATO. KELELE ZA CHURA NA DUA LA KUKU.
 
Mpinzani uchwara hawezi kufurahia maendeleo yanayofanywa na serikali.
 
Kiongozi hata kama zikipitishwa Trilion 1,000 shida iko wapi kama Uwanja huo ni kwa manufaa ya Watanzania wote, kana faida ni kwa kikundi cha watu au mtu mmoja hapo litakuwa kosa baya na kubwa sana. Tuache Ushabiki, Uwanja wa KIA mbona fedha yake haikupitishwa na Bunge na bado hakuna anayelalamika? Tuache Ubaguzi wa Ukanda.
Mjinga kweli wewe! Chato International Airport ina manufaa gani kiuchumi kwa nchi hii?!

Kilimanjaro International Airport hujui manufaa yake kiuchumi kwa nchi hii hadi ufananishe na Chato?!
 
Sikia Mkuu, yaani hapa kinachotakiwa ni kufuata Bajeti, Mwaka huu tunataka kujenga Daraja Fulani na Barabara Fulani Bunge linapitisha PESA, sasa kinachohojiwa, ni Nani aliyepitisha PESA kujenga uwanja huu?

Unajua hatufanyi kitu chochote hasa kinachohusu Pesa bila kupitishwa Bungeni, Bajeti.

Mkuu hapo ndipo shida ilipo
Urasimu usiokuwa na tija e
wa nini ?
 
Hata kama utalalamika hadi uzimie; UWANJA WA NDEGE LAZIMA UJENGWE CHATO,NARUDIA LAZIMA UJENGWE CHATO. KELELE ZA CHURA NA DUA LA KUKU.
Hujajibu maswali yangu mawili. Mimi sitaki mipasho ya taarabu nahitaji majibu. Mwaka wa ujenzi wa uwanja wa KIA na sababu za kujengwa uwanja ule. Mipasho kwenye chit chat.
 
Ninasikitishwa mno na Malalamiko ya Mh.Mbunge huyu, Je sisi watu wa Chato siyo Watanzania? Hatuna thamani? Madai ya kuwa ni "miss use of resources" haoni kuwa ni matusi? Kwa wabanchi wa Chato ni miss use of resources? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.
Umeelewa ulichoandika ama ili mradi ujaze wingi wa mada chafu jf?
 
Ninasikitishwa mno na Malalamiko ya Mh.Mbunge huyu, Je sisi watu wa Chato siyo Watanzania? Hatuna thamani? Madai ya kuwa ni "miss use of resources" haoni kuwa ni matusi? Kwa wabanchi wa Chato ni miss use of resources? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.

KIA angalau kuna Kuna Mbuga Arusha na mlima Kilimanjaro vinatoa pato la taifa, unajengewa barabara, huduma za afya na kurudisha hata hiyo fedha, halafu hata ndege zinazotua Kilimanjaro zinalipishwa gharama za kutumia huo uwanja, je Chato kuna nini cha kufidia hayo Matumizi makubwa hivyo? Hakuna anayesema ukanda wala nini? mbona umejengwa Mwanza hakuna anayelalamika? akili zako zifikirie mbali kidogo, watu kama nyinyi hamtakiwi kabisa katika taifa hili maana mawazo yenu mnawaza ukabila tu, nina wasiwasi na wewe kama hujatokea kwenye nchi fulani hivi!

Kinaachoalalamikiwa hapa Kiuchumi utatusaidiaje? au Hizo pesa zinarudishwa na watumia uwanja je kama uwanja utajengwa na ndege za kutua ni finyu baba yako ndio atarudisha hizo pesa? Watu wanachoongelea hapa ni mambo ya kiuchumi na si vinginevyo?

Basi kama ni kila mtu anahitaji Uwanja wa Kimataifa Kuna Njombe, Simiyu, Geita, Ruvuma, wote hawa nao watadai viwanja wa kimataifa kwani wao si Watanzania?

Nimechoka na msg yako?
 
Hana chuki, anauliza Bajeti ya Ujenzi wa uwanja ilipangwa na Nani? Wao Kama Bunge walipitisha bilioni 2, lakini mpaka Leo imetumika bilioni 36,
Ni Nani aliyepitisha hizo Pesa?

Jibuni swali Acheni kupotosha ukweli,
Hili swala linachanganywa na siasa za kikanda, watu wanahojiwa waeleze ukweli wanaingiza ukanda.

Nchi ina masifuri mengi sana hii!
 
Kujengwa airport tu chato mnalaaaaaaalaaaaamiiiikaaaa,,,!!!!!!!
Hamkuona kwa lowasa Lami hadi majumbani kwao au kwa kina Msuya lami umeme hadi vijijini kwao ten a miaka hio ya 80/90
Wakuu tuangalie kotekote tuache chuki binafsi na roho za kwanini
 
Kwanini enzi hizo hamkuingia kwenye mitandao kuhoji?

Kwakua nyinyi hamkuhoji na sisi ndo tusihoji
 
Unaonaje kama hela hiyo ingetumika kuwajengea hospital kubwa, si mgepata faida kuliko kujenga uwanja? Usipelekeshwe na ushabiki fuatilia taratibu hoja zake
 
Swali ni , Je! Hizo fedha zimeidhinishwa kwa bajeti iliyoko?? Msiwe na hasira mtu akiwauliza swali jamani. Kwani kikao cha bajeti kazi yake ni kwenda kuambiwa mlizotumia au mnazoomba kwenda kutumia. Ijulikane zitapatikanaje na mtumie kiasi gani. Hizo 2 billion kwanini mkaziomba?? Mngepeleka bungeni hayo maombi kwani ingelikuwa dhambi??
Taratibu wameziweka wenyewe kuzifuata ni tatizo. Wanataka walala hoi na wanyonge ndo wafuate. Kiapo cha kinafiki wameapa kwa kumnyooshea Mungu vitabu vitakatifu pamoja na katiba ya nchi. Neema ya Mungu tu iwasaidie kujielewa
 
Hana chuki, anauliza Bajeti ya Ujenzi wa uwanja ilipangwa na Nani? Wao Kama Bunge walipitisha bilioni 2, lakini mpaka Leo imetumika bilioni 36,
Ni Nani aliyepitisha hizo Pesa?

Jibuni swali Acheni kupotosha ukweli,
Akijibu naenda zimbabwe
 
Back
Top Bottom