HoneyBee
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 912
- 860
Asanteni sana kwa point zenu. Nakubaliana nanyi kutokana na niliyoyaona kupitia wazazi wangu pia. Baba ana masters, mama ni std 7 lakini baba alikuwa anamuogopa na haelewani na mama sababu hata kama hakuweza kujiendeleza kimasomo, alikuwa na akili za kujituma hata kama baba alikuwa hampi support. Nawapenda wazazi wangu wote, lakini ingekuwa sio mama nisingesoma ingawa baba alikuwa analipia kiasi fulani ada, ikija kwenye pango na pesa ya chakula anachelewesha au anaweza kukuambia pesa hakuna. Lakini ndugu zake wakiita pesa zinapatikana. Mama alifanya juu chini kuhakikisha pesa zinapatikana on time ili nisipoteze chumba wakati nipo chuo.
Hata mimi najiuliza mama angekuwaje kama angeenda mpaka from 6 au hata chuo. Her potential is fantastic and she is the strongest person I know. She is my role model.
My point is, elimu ni ukombozi wa mwanamke. Anaesema wanawake wenye elimu wana jeuri ni wale wanaume wasiopenda kuhojiwa na wake au wapenzi wao. Wewe kama mwanamme huwezi ukasema hutamsomesha mtoto wako wa kikei ili awe mke bora kwa atakaemuoa.
Hata mimi najiuliza mama angekuwaje kama angeenda mpaka from 6 au hata chuo. Her potential is fantastic and she is the strongest person I know. She is my role model.
My point is, elimu ni ukombozi wa mwanamke. Anaesema wanawake wenye elimu wana jeuri ni wale wanaume wasiopenda kuhojiwa na wake au wapenzi wao. Wewe kama mwanamme huwezi ukasema hutamsomesha mtoto wako wa kikei ili awe mke bora kwa atakaemuoa.
Tatizo sio elimu wala wanawake wasomi, tatizo ni wanaume waliosoma bado hawajaelimika. Wanaume wasomi wanataka wanawake wasiosoma kwa kuwa wanakubali kukanadimizwa. Wanaume hawataki mawazo mbadala toka kwa wake zao. Wanataka wafanye watakavyo bila kuhojiwa na mke wake. Mke aliyeelimika ni lazima atataka ufafanuzi kwa kila jambo linalofanyika ndani ya familia. Iwapo majibu hayataridhisha hata kubali, hapo ndiyo mwanzo wa migogoro.
Elimu humfanya mwenye kuelimika kujiamini zaidi katika maisha, pia kipato pia mfanya mtu kuwa huru na kujiamini. Wanaume wanataka mtu anayemtegemea kwa pesa na amwawazo ili waendeleze mfumo dume. Wanaume wengi ni madikiteta. Wakiweza wanataka wadikteti hata watoto wazaliwe wangapi na kwa nafasi gani.
Kama mambo kama haya hawawezi kuyapata kwa wasomi, basi wakoradhi kuoa hata asiyesoma kabisa. Ukiangalia Maprofesa wengi wameoa wasiofikia kiwango chao cha elimu ikiwezekana anaoa asiyesoma kabisa ambaye atamsujudia kama mume, chanzo cha uchumi, mweneye mawazo pevu na msomi kuliko wote kwenye familia. Hawezi kuulizwa lolote.
Siyo elimu peke yake lakini pia wanaume wanaogopa kuoa mke mwenye kipato kikubwa kuliko yeye. Sababu ni ileile kwamba anakuwa amepunguza utegemezi kwa mume. kutomtegemea mume kunatafsiriwa kama kujivuna. Kuwa tegemezi kunakunyima uhuru. Angalia nchi maskini kama Tanzania, zinazotegemea nchi tajiri hazina ubavu wa kukataa lolote linalosemwa na mtoa misaada. Malawi kwa mfano: ilikataa ndoa za jinsia moja hadi ikawafunga wanaume wawili waliooana, lakini Uingereza ilipinga uamuzi wa mahakama ya Malawi. Kwa kuchelea kunyimwa misaada serikali ya Malawi iliwaachia huru.
Hali kadhalika mwanamke asiyemtegemea mume kwa kila kitu anaonekana tishio kwa mume dikteta
aise haya mambo yana umuhimu wake kama watu wenyewe walivyoelewana. Kwa kizazi cha leo maisha ni tofauti na zamani. Ngoja nikwambie, dingi yangu alikuwa mtumishi na mama akawa mkulima. Dingi alikuwa mkware sana kwani pesa yake nyingi alitumia kunywa na wanawake. Alifika hatua hata kutusomesha hataki. Aise nilipata shida sana lakini chakula kilikuwepo cha kutosha familia. Kuna wakati nililaumu kutosoma kwa mama japo kutuwezesha kwa ada. Ilinibidi nifanye vibarua ili kukidhi ada, na mahitaji mengine thanks God i was clever shule haikunisumbua. Niliapa kwamba sitaweza kuassociate na mtu ambaye hana mwanga na maisha ya sasa. Sisemi kwamba hawafai lakini tafuta mtu ambaye chemistry itakaa vizuri. Ko always nimekuwa sijihusishi na wasichana ninaoona hatutaendana. Onyo: usivamie wasomi kama chemistry haiendani.