Hivi duniani kote viongozi wa juu wa nchi wakimaliza muda wa uongozi wanalishwa na pesa za nchi?

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,946
2,929
Saalam!

Nimekuwa nikijiuliza Sana juu ya gharama watanzania Kama taifa kugharimia viongozi wa juu wanapomaliza muda wao wa kuliongoza taifa.

Ni gharama kubwa Sana, ukizingatia siyo wachache na watazidi kuongezeka.

Wajuzi wa mambo nisaidieni, huu ni utaratibu wa dunia nzima, na Kama siyo kwanini tusiubadiri ili kutupunguzia mzigo wa kuwalea watu ambao

1. Walikuwa watumishi wa umma Kama wengine Kama haitoshi walikuwa na kipato kuliko wengine

2. Wanakuwa wanajilimbikizia Mali kuliko wengine.

3. Wanakiiunua mgongo kikubwa kuliko wengine.

Nimekuwa nikisoma mijadala mbalimbali humu hasa ya wale wanaosema Tanzania ni nchi huru haiwezi kuingiliwa na mataifa mengine kimaamuzi.

Ni vema kama huu utaratibu ni wa kidunia, kama taifa huru na masikini kwanini tusiamue kuufuta na mabilioni hayo yakaelekezwa kwenye matumizi ya serikali?

Wapewe ulinzi tu, mambo mengine wastruggle wenyewe kama wastahafu wengine.

Alipoingia Magufuli nilitazamia Angeliona hili na kulifanyia marekebisho kwakuwa alisema anauchungu na pesa za wanyonge.

Na hili alijipambanua alipokataa kwenda nje ya nchi kwa kuokoa pesa za wanyonge, lakini ninashanga kuona zikitungwa na Sheria za kuwalinda wakiondoka madarkani, kama haitoshi, misafara ya ndani tu inalighairimu taifa mamilioni ya shilingi.

Maana kila uzinduzi serikali yote inahamia hapo.

Nadhani Kuna haja ya kuyaangalia Mambo mengi kwa jicho pevu na angavu.

Karibuni
 
Unawezekana huo utaratibu upo, ila kwa Bara la Afrika, nadhani tutakuwa tumeongeza na udambwi dambwi wetu wa Kiafrika.

Kama Tanzania ndiyo usiseme kabisa! Yaani ukiwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, nk. Ukistaafu unakula mshahara wa 80% wa yule aliyeko madarakani!

Hatari sana.
 
Omba Mungu mzee ukipata shavu kama hilo ndio umetoboa yani unaserereka tu.

Kinachoua watu mapema mara nying ni umaskini uzeeni.
 
Unawezekana huo utaratibu upo, ila kwa Bara la Afrika, nadhani tutakuwa tumeongeza na udambwi dambwi wetu wa Kiafrika.

Kama Tanzania ndiyo usiseme kabisa! Yaani ukiwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, nk. Ukistaafu unakula mshahara wa 80% wa yule aliyeko madarakani!

Hatari sana.
Hii ni dhuluma kubwa sana kwa watanzania masikini, sijui nani alipitisha hizi sheria za namna hii.
 
Iko hivyo karibia kila nchi.

Na kila nchi ina sheria kwa ajili ya maslahi ya viongozi wastaafu.

Mambo mengine ukubali tu kama binadamu huwezi kuyapata.

Ndio tunaita kuridhika.

Ridhika na ulichonacho mkuu na ukitumie vyema.
 
Vishawishi vya vipi?

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Kikwete alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10 na baadae amiri jeshi na mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa miaka 10. Kwa mambo anayoyajua, ule ni mgodi unaotembea, lazima atunzwe na asiwe na wasiwasi na maisha yake.

Marekani hawakuwa na huu utaratibu mpaka Harry Truman alipoondoka madarakani na akawa na hali mbaya ya kifedha wakatunga sheria ya mshahara, ulinzi na mambo mengine
 
Huwa mnakataa kuwaiga mabeberu Leo ni wazuri kwenye eneo hili!?
 
Kikwete alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10 na baadae amiri jeshi na mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa miaka 10. Kwa mambo anayoyajua, ule ni mgodi unaotembea, lazima atunzwe na asiwe na wasiwasi na maisha yake.

Marekani hawakuwa na huu utaratibu mpaka Harry Truman alipoondoka madarakani na akawa na hali mbaya ya kifedha wakatunga sheria ya mshahara, ulinzi na mambo mengine
Apewe ulinzi tu
 
Back
Top Bottom