Hivi Dr Slaa alipitishwa lini na mkutano mkuu kugombea urais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Dr Slaa alipitishwa lini na mkutano mkuu kugombea urais?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Akili Kichwani, Aug 9, 2010.

 1. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  nimesikia habari kuwa dr slaa leo anachukua fomu za urais toka NEC!!

  nimefuatilia nimeona kama ifuatavyo....


  7.7.10 Kazi za Mkutano Mkuu wa Taifa ni:-
  (a) .............
  (b) ........
  (c) Kuteua mgombea wa Uraisi na mgombea wenza wake kwa Jamhuri ya Muungano
  wa Tanzania na mgombea Urais wa Zanzibar.


  7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
  (a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
  wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika
  mkutano mkuu kwa uamuzi.

  7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
  (a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisha
  ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.  1. hiv ni lini mkutano mkuu wa chadema ulimpitisha kugombea urais wa JMT kupitia chadema?
  2. kama hakupitishwa na mkutano mkuu, katiba ya chadema inaruhusu hili?
  3. kama katiba inaruhusu, nini hatima ya demokrasia ndani ya chama hiki?

  msaada tafadhari, manake mi sikuusikia mkutano mkuu wa chadema!!!
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Ndugu,
  Kwa kukusaidia si vyama vyote vina mfumo kama CCM....alipitishwa kwa mujibu wa CHADEMA
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kama TBC hawataki kuonesha live huwezi kuona, umafya unaofanywa na ccm kwa chadema inacheza na karata yenye shibe,


  Slaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mujibu wa chadema unasemaje?
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Kamati kuu.......
   
 6. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwisho utauuliza kuwa Hadija kopa wa chadema ni nani?
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Sio wote wenye pesa za kujitangaza kifisadi kama ccm

  Kama umesikia hivyo ndo imetoka, ulitaka wafanye kama CCM kurusha live tv zote??
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Hawa nao mkutano mkuu ulifanyika lini
  1. LIPUMBA
  2. MUTAGWAYA
   
 9. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  naomba kipengele cha katiba ya chadema kinachohusika nifuatilie, manake mwaka 2005 niliona mbowe alipitshwa kwa utaratibu tofauti na wa mwaka huu uliompitisha dr slaa!!1
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  3.'dr' hashim rungwe
   
 11. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  jamani mbona mnazunguka mbuyu?
  nimeuliza nieleweshwe. nisaidieni utaratibu wa chadema unasemaje na kama ulifuatwa sawasawa? basi sitaki zaidi.
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Huu sio mwaka 2005 ndugu....mwaka 1980 CCM walifanyaje kumteua mwalimu?...mkutano mkuu pia?
   
 13. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kama wangemudu gharama ingekuwa vizuri sana, kwani ni sehemu ya promotion na labda hata swali hili nililouliza lisingenisumbua!!! heri yangu nina mahali pa kuulizia, imagine wako wangapi wanaojiuliza swali kama hili kimyakimya???
   
 14. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  soma post # 11
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Katiba ya ccm na chadema ni sawa???

  Chadema sio Mafisadi kama wewe
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Soma post nambari tano....
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kuna kitu hakijakaa sawa kwenye uteuzi huu wa mpendwa wetu Dr Slaa. CHADEMA kirekebisheni msije mkawapa ahueni CCM kwa kuweka pingamizi wao au kuwatumia watu wa aina ya Mrema, Mziray wa APPT Maendeleo, Mtikila wa DP,.....
   
 18. kajukeg

  kajukeg Member

  #18
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Umeshajibiwa alipitishwa kwa mujibu wa chadema,unataka nini tena? we cha kuuliza ATACHUKUWA SAA NGAPI HIZO FORM NEC? sio kuhoji kama utaratibu ulifuatwa,we yanakuhusu nini? SUBIRI UONE KAMA NEC WAKIGOMA KUMPA FORM NDO UHOJI KAMA UTARATIBU ULIFUATWA AMA LA....!
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Anachohoji Akili Kichwani kimo kwenye Katiba yao kwenye vifungu vifuatavyo:
  7.7.10(c) na 7.7.13(a)
   
 20. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  nakushukuru sana mzee anagalau wewe umeona kitu.... najua ukipenda sana hata chongo utaona kengeza, ni makosa makubwa sana kuruhusu vidosari vidogovidogo hata kama hakuna pingamizi ndani ya chama, lakini vinaweza kutumiwa na wapinzani wa chadema kwenye kampeni, kumbuka chama hiki kinazongwa na uzushi wa aina nyingi kama ukabila, sasa udini na tena mnataka kuongeza udikteta wa kamatikuu!!

  jamani siasa zina mbinu nyingi..... bado sijaridhika na majibu, ina maana pamoja na chadema kushabikiwa sana hapa jamvini, hakuna mtu anayejua utaratibu wa kumteua mgombea uais ndani ya chama unasemaje? ni ajabu na kweli!!

  bado nasubiri anayejua utaratibu ukoje anisaidie....
   
Loading...