Hivi Dr.Mpango anafanya kazi yake kitaalamu bila kuingiliwa?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,682
149,886
Huyu Dr.hivi tangu akabidhiwe hiyo Wizara ya Fedha,kazi zake mfano hii ya kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Bajeti ya serikali anaifanya kwa kuzingatia utaalamu wake au anaifanya kwa maelekezo ya wanasiasa?

Mimi napata shida sana kuhusu huyu waziri tena ambae ni msomi wa kiwango cha PhD.

Tukiendelea nae huyu kwa muda wote uliobaki,tutakuja kuona matokeo yake.

Hebu tutafakari huu mfano mdogo tu.

Mabasi na malori yanayojaza lita za mafuta kuanzia lita mia moja na kuendelea na kila siku yako barabarabani kwa tozo ya shiling 40 kwa lita yatalipa kodi kiasi gani kwa mwaka kupitia huu utaratibu mpya wa kulipa hiyo Road License?

Hii kodi atalipa mwenye basi au mwananchi?

Hivi kwa wenye magari ya abiria hii kodi inawagusaje zaidi ya wao kuongeza nauli ili ilipwe na mwananchi wa kawaida?
 
Huyu Dr.hivi tangu akabidhiwe hiyo Wizara ya Fedha,kazi zake mfano hii ya kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Bajeti ya serikali anaifanya kwa kuzingatia utaalamu wake au anaifanya kwa maelekezo ya wanasiasa?

Mimi napata shida sana kuhusu huyu waziri tena ambae ni msomi wa kiwango cha PhD.

Tukiendelea nae huyu kwa muda wote uliobaki,tutakuja kuona matokeo yake.
Tutupie takwimu zenye mushkeli kwani hitimisho lako halina uhusiano na tuhuma za kuingiliwa kwenye majukumu yake
 
Back
Top Bottom