Hivi dini zingine hawaruhusiwi kuchinja?

Kremme

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
471
494
Mimi nimeishi katika jumuiya ya watu mbalimbali na wa dini zote.

Cha kushangaza inapofika sikukuu au wamenunua jogoo basi watu hutafutwa kwa ajili ya kuchinja, japokuwa wanaume wapo.

Nimekula sana shingo mchuzi hata vibawa kwa kazi hiyo. Ndio nauliza; Je, kuna madhehebu ya wakristo wanakataza kuchinja?
 
Wakristo sio tu kwamba haturuhusiwi kuchinja, tunaweza na tunaruhusiwa kula chochote isipokua nyamafu tu. Tukiamua kuchinja wenyewe hakuna tatizo lolote kwa upande wetu, tatizo jamii zetu zimeingiliana na kuna ukaribu wa hali ya juu sana na ujirani kati ya waumini wa dini hizi mbili, sasa kwa wengine hawaruhusiwi kula kilichochinjwa bila kufuata taratibu zao, kuamua kuchinja wenyewe italeta kuwanyima ushiriki wa hao ndugu na jamaa zetu.

Tunafanya hivyo kwa kuweka maelewano tu na kujumuika, kuchinja tunaweza sana. Kama hatuwezi, mnyama nani hua anachinja?
 
Umejibu kwa hekima sana mkuu. Hongera kwa ilo.
 
Ni vema kufanya hivyo kutokana na ugeni wa uislamu kwa waislamu walio wengi. Ila kiuhalisia waislamu wanaruhusiwa kula kilichochinjwa na wakristu pia mayahudi kwani ktk Qur-ani ipo aya inaruhusu kula vilivyochinjwa na watu walioteremshiwa Taurati na Injili. Ila si halali kula kilichochinjwa na mshirikina hata kama ni muislamu kama wale wanaojitia kutibu kwa kutumia majini na wapiga nyota.
Pia ktk uislamu mwanamke aruhusiwa kuchinja.
 
Ahsante kwa elimu na mchango wa kiungwana mkuu.
 
Ni vema kufanya hivyo kutokana na ugeni wa uislamu kwa waislamu walio wengi. Ila kiuhalisia waislamu wanaruhusiwa kula kilichochinjwa na wakristu pia mayahudi kwani ktk Qur-ani ipo aya inaruhusu kula vilivyochinjwa na watu walioteremshiwa Taurati na Injili. Ila si halali kula kilichochinjwa na mshirikina hata kama ni muislamu kama wale wanaojitia kutibu kwa kutumia majini na wapiga nyota.
Pia ktk uislamu mwanamke aruhusiwa kuchinja.
Unaweza itoa hiyo aya ...... au umenogewa na mada?
 
Ni vema kufanya hivyo kutokana na ugeni wa uislamu kwa waislamu walio wengi. Ila kiuhalisia waislamu wanaruhusiwa kula kilichochinjwa na wakristu pia mayahudi kwani ktk Qur-ani ipo aya inaruhusu kula vilivyochinjwa na watu walioteremshiwa Taurati na Injili. Ila si halali kula kilichochinjwa na mshirikina hata kama ni muislamu kama wale wanaojitia kutibu kwa kutumia majini na wapiga nyota.
Pia ktk uislamu mwanamke aruhusiwa kuchinja.
Leta aya/verse
 
Wakristo sio tu kwamba haturuhusiwi kuchinja, tunaweza na tunaruhusiwa kula chochote isipokua nyamafu tu. Tukiamua kuchinja wenyewe hakuna tatizo lolote kwa upande wetu, tatizo jamii zetu zimeingiliana na kuna ukaribu wa hali ya juu sana na ujirani kati ya waumini wa dini hizi mbili, sasa kwa wengine hawaruhusiwi kula kilichochinjwa bila kufuata taratibu zao, kuamua kuchinja wenyewe italeta kuwanyima ushiriki wa hao ndugu na jamaa zetu.

Tunafanya hivyo kwa kuweka maelewano tu na kujumuika, kuchinja tunaweza sana. Kama hatuwezi, mnyama nani hua anachinja?
Hongera kwa hekima zako
 
Sisi kama watanzania wadini mbalimbali huwa tunapenda kujumuika katika sherehe mbalimbali za kidini na za kitaifa,sasa kama wewe ni muumini wa dini ambayo hana masharti ya kuchinja na unapenda kuwaalika watu wa dini nyingine ili tusherekee pamoja,huna budi kumualika mchinjaji wa kiisilamu au wa kiyahudi.
 
Leta aya/verse
Maa'ida: 5

"This day are (all) things Good and pure made lawful unto you. The food of the People of the Book is lawful unto you and yours is lawful unto them. (Lawful unto you in marriage) are (not only) chaste women who are believers, but chaste women among the People of the Book, revealed before your time, when you give them their due dowers, and desire chastity, not lewdness, nor secret intrigues…"

Kwa ufafanuzi zaidi wa kadhia hiyo rejea: Fatawa Islamiyya, Sheikh Abdel-Aziz Bin Baz, 3/404.
 
Back
Top Bottom