G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Yani interchange ya Ubungo ni moja ya interchange mbaya kabisa duniani na najua kuwa ile inapatikana Tanzania pekee.
Sasa niulize, lile daraja la juu la kuunganisha Mwenge na Buguruni yani Sam Nujoma na Mandela road lipo kwa kazi gani? Umeenda kujenga juu halafu barabara ya chini umeua wakati kwa ile ile poor design ungeweza kutanua barabara ya chini ukapata michepuko ya pembeni kutokea barabara ya Mandela kwenda Kimara kupitia ya Morogoro vile vile ungepata straight kutoka Mandela kwenda Sam Nujoma na wanaotokea upande wa Ubungo kwenda Mwenge wangeenda kujengewa round about njia panda ya chuo kikuu.
Kwa kutumia ubunifu huu walau pangeonekana afadhali. Yale madaraja yalivyopishana pale yameonekana kituko cha aina yake.
Yani nashangaa na watanzania wanasambaza video! Tunajidhalilisha sana.
Yani kwa ufupi lile daraja la pili ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Achilia mbali ujenzi wote ni wa hovyo hovyo usiozingatia utaalam hata kidogo.