Hivi China kuna njaa kali hadi raia zake wako radhi kufa kufika Ulaya/Uingereza

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
6,191
13,614
Vifo vya watu 39 walioswekwa na kusimikwa kwenye trela refregirate vimetingisha vichwa vya habari duniani.

Inasadikika raia hao wanaume 30 na wanawake 9 wengi wao ni wa China na baadhi wa Vietnam walikutwa wamekufa kwenye container lililokuwa linatoka Bulgaria kupitia Ubelgiji hadi Uingereza.

Sasa najiuliza China inasifiwa kuwa nchi tajiri na yenye uchumi mkubwa hata kuzidi Marekani kwanini wananchi wake wanalia njaa na maisha magumu hadi wanahatarisha maisha yao kufika Ulaya?

Ni Taiwan na Hong Kong tu ndio Visa free kuingia Ulaya, Marekani na Australia lakini huko mainland lazima uombe Visa kwa nini ni hivi?

Kingine licha ya utajiri na uchumi mkubwa mbona wazamiaji hawajisumbui kuzamia China licha ya Visa yake kuwa rahisi?
 
Taifa la China ni kweli lina uchumi mkubwa ila sio kwa mtu mmoja mmoja eneo linalopimwa ambalo anamkaribia Mmarekani ni uchumi mpana. Hii imeegemea zaidi kisekta kwa ujumla uchumi wa mtu mmoja mmoja nchi za Asia ujumuishi wake ni mzuri ktk uwiano ila wana ujira mdogo sana usioweza kukidhi mahitaji hasa hasa kwa watu wasiokua na ujuzi ndo maana wengi wao utawaona wanakimbilia mahala pengine kwenda kuganga njaa.
 
Taifa la China ni kweli lina uchumi mkubwa ila sio kwa mtu mmoja mmoja eneo linalopimwa ambalo anamkaribia Mmarekani ni uchumi mpana. Hii imeegemea zaidi kisekta kwa ujumla uchumi wa mtu mmoja mmoja nchi za Asia ujumuishi wake ni mzuri ktk uwiano ila wana ujira mdogo sana usioweza kukidhi mahitaji hasa hasa kwa watu wasiokua na ujuzi ndo maana wengi wao utawaona wanakimbilia mahala pengine kwenda kuganga njaa.
Mbona wajapan, korea kusini, Hong Kong na Taiwanese na Singaporeans hawazamii na wao kwao ni visa free nchi za magharibi??
 
Umekosea kuweka hoja yako .Ungesema mbona China wana ma flyover, ma bullet train,Towers kila mahali ,wana mandege mengi lakini wanakimbia nchi yao? Maana hivi sasa huku bongo hayo ndio tunaambiwa ukiwa na hivyo vitu ndiyo umeendelea .Maendeleo ya watu mifukoni huku danganyika tunaambiwa si maendeleo.
 
Mchizi, Naona wewe umesaidia pia kidogo kumfungua mara nyingi watu wengi huchanganya mambo hata wataalamu wenye hushindwa kuwasilisha vizuri taarifa za mwendo wa uchumi kwa sisi raia wa kawaida . Uchumi mara zote hupimwa kisekta yaani uchumi mpana mara nyingi uchumi huu hautoi taswira halisi ya watu wake.

Kwa mfano nchi nyingi zinazoendelea huwa zinasoma namba kubwa sana ya ukuaji wake wa uchumi kwa ssb huchangiwa na uwekezaji mkubwa sana wa miradi ya kimaendeleo kama ujenzi wa miundombinu kama barabara, reli, madaraja na kadharika, swali la msingi hapa je hizi sekta kama ujenzi mawasiliano teknolojia anga na nyinginezo zinajumisha idadi gani ukilinganisha na raia waliopo nchini kwako ambao wanapaswa kuwepo ktk nguvu kazi?

Mara nyingi nchi zinazoendelea huwa hapa ndo changamoto utaona unafanya miradi mikubwa ila inabeba idadi ndogo sana ya watu ukilinganisha na uhitaji wa wengi na hapa ndo utaona wengine wanajiongeza kwenda kutafuta fursa mahala pengine.
 
Mungu ni Mzungu wanasema, hivyo kila mtu anataka kama sio kuishi basi amsogelee. Naskia Mexico ni Jirani sana na Marekani lakini mnasikia huko Mexco hali ngumu sana, hadi raia wake wana kufa jangwani wakijaribu kukatiza kuingia Marekani.
Usiwashangae wachina Maendeleo hayana chama, anasema Magufuli.
 
Nilipata fursa ya kwenda Quingdao nikakutana na Mr Lee ambaye ni mfanyakazi wa kiwanda cha FAW

Akanikaribisha vema , kwakuwa task ilonipeleka ilitakiwa kusafiri ndani ya China Kwa miezi kadhaa nilishangaa baadhi ya Maeneo china yako zaid ya kawaida na wachina maskin sana
Hahaha ungewaambia waje Tanzania kuna fursa za kufa mtu.

Kuna mchina mmoja anaishi Buguruni, alinichekesha sana, yeye anasema wachina ni kama chawa, ukiona mmoja tu jua wako wengi sana wamejifichaficha humo, ukitaka kumaliza chawa kichwanni unanyoa kipara, na kwenye nguo unazichoma. Alikuwa anasema wachina wakigundua fursa zilizoko huku wanaweza kuhamia kwa maelfu kwa mkupuo.

Yeye huwa anasema walimsahau huku na hatorudi china mpaka waliomleta wamfuate, anasema china alikuwa hana mke lakini Tanzania wanawake wengi, kwake hicho ni faraja sana kuliko kuwa tajiri.
 
MAISHA BORA

Suala la Utajiri kwa China ni kama taifa, ilhali kwa raia ni sio sawa.

Maisha bora hayapimwi kwa Skyscrapers, Electric train's, Airplanes, Fly Over na Industries/Factories ndio maana unayaona hayo.

Mr. Jon tena uzuri upo Scandinavia na unafahamu fika Skyscrapers ni chache lakini taifa na raia wanao uwezo mzuri kufanikisha kuwa na maisha bora.

Maisha Bora, Maisha Bora, Maisha Bora
 
Miongoni mwa 39 waliokufa ndani lahilo container 'metal coffin' ni huyu mdada yani imeniuma sana alimuandikia mama yake sms kwaheri sisi ndio hivyo tena tunakufa taratibu. Kwasababu walisimikwa ndani na ni soundproof. Hiki kitu kimenifanya nilie kabisa. Unakufa hivi hivi unaona Mnajaribu kupiga kelele wapii. Hii chansi ninayo ya kubeba boksi Denmark nitaitukuza milele. Ndio maana kila wakati napochoka na sometimes kukata tamaa nikibeba boksi nakumbuka nilipotoka na nakumbuka malaki wanavyohatarisha maisha kupata fursa kama hiininayo yani sichoki.
20200834-0-image-m-7_1572043771162.jpg
Pham Thi Tra My enzi za uhai wake
 
Umekosea kuweka hoja yako .Ungesema mbona China wana ma flyover, ma bullet train,Towers kila mahali ,wana mandege mengi lakini wanakimbia nchi yao? Maana hivi sasa huku bongo hayo ndio tunaambiwa ukiwa na hivyo vitu ndiyo umeendelea .Maendeleo ya watu mifukoni huku danganyika tunaambiwa si maendeleo.
Mmekatazwa kuuliza maswali magumu, mkiuliza mnaonekana mnamuombea jamaa afe
 
Back
Top Bottom