Bramo
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 13,160
- 10,007
Wakuu
IGP Amemtuma ACP Chagonja kwenda kuchunguza kiini cha machafuko ya Songea.
Namnukuu ACP Chagonja kama ifuatavyo Kutoka Mwananchi
Akaenda mbali zaid
Akaongeza
Atoa angalizo kwa Media
Source: Mwananchi - 24/2/2012
My Take
Chagonja Tayar jibu analo, so kwenda kwake huko ni Ubadhirifu wa Fedha zetu walipa kodi na kimsingi ni ka aina flan ka ufisadi.
IGP Amemtuma ACP Chagonja kwenda kuchunguza kiini cha machafuko ya Songea.
Namnukuu ACP Chagonja kama ifuatavyo Kutoka Mwananchi
" Chagonja akizungumza na Mwananchi jana alisema maandamano hayo hayakuwa ya amani bali ya kihuni kwani yalilenga kuvamia ofisi za serikali ikiwemo Ikulu ndogo na Ofisi ya Mkuu wa mkoa. Chagonja alikuwa akijibu swali lililotaka aeleze endapo haoni kama polisi imetumia nguvu kubwa kutawanya raia waliokuwa wakiandamana kwa amani.
Akaenda mbali zaid
"Maandamano ya amani watu wanavamia Ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi ya mkuu wa mkoa?"
"Sijafika huko ndo naelekea lakini, yale si maandamano ya amani. Yaani wahuni wanataka kuivuruga nchi waachiwe? Kuweni wazalendo, msiwe kama labda ninyi ni waandishi wa BBC kutoka Uingereza, hii ni nchi yenu."
Akaongeza
Atetea Polisi (Wauaji)Alifafanua kwamba, maandamano ya amani yanafahamika kwani watu hulazimika kuomba kibali na kuweka wazi ajenda ya maandamano "Lakini siyo maandamano yale, watu hayakuwa na kibali chochote, wahuni wamejiingiza wanataka kuvuruga nchi tu.".
Mkuu huyo wa operesheni alitetea polisi akisema,"Usifikirie polisi hawana akili. Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue hovyo risasi za moto kwa raia. Hakuna askari anapenda kuua raia..., lakini watu wanavamia Ikulu, ofisi ya mkuu wa mkoa, magari ya polisi hapo kuna amani kweli?".
Atoa angalizo kwa Media
Alitoa angalizo kwamba ni lazima hata vyombo vya habari, viache ushabiki badala yake viangalie maslahi ya taifa kwani nchi ikivurugika wao pia hawatasalimika na kusisitiza, "Kuweni wazalendo bwana, msifikirie kulishutumu jeshi la polisi tu.".
Source: Mwananchi - 24/2/2012
My Take
Chagonja Tayar jibu analo, so kwenda kwake huko ni Ubadhirifu wa Fedha zetu walipa kodi na kimsingi ni ka aina flan ka ufisadi.