Hivi CHADEMA mkichukua nchi hawa wasanii wetu wataweka sura wapi?

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,436
2,292
Habari wana jamvi,

Hivi kasi walio nayo sasa hivi wasanii kwa kuimba nyimbo za CCM na zote zikiwarushia wapinzani madongo makali na Kuwasifia CCM. Mfano imetokea CHADEMA wakachukua nchi sijui itakuwaje

Kila msanii sasa hivi anatoa ngoma ya CCM. Jana nimeiona ile Magufuli gangs ya kina Sheta aise wamewaua vibaya CHADEMA; kama ile verse ya G. Nako hahahahahah nacheka kama mazuri

CHADEMA mwambie basi hata Sugu na Professor Jay watoe hata mabata madogo madogo yanaogelea yanaenda chadema chadema chadema
 
Hakuna jipya hapo,hata Mwanamuziki Superstar wa Congo enzi hizo Franco wkt wa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 1984 alimuimbia Nyimbo Mobutu ya kumsifia,wimbo huo uitwao Candidat na biso Mobutu” (1984)“ yaani Our candidate is Mobutu”.

So ni mambo ya 'kawaida' tu hayo 'ulimwenguni'.
 
Mkuu tuwasamee kumbuka miezi mitatu walikuwa juu ya mawe!! Mayalla kikwetu ni NJAA , Njaa baba Njaaaaaa!!! Njaa haina Baunsa ,Adui Muombee Njaa atanyoosha mikono juu hata kama alikuwa shujaa.
 
Wasanii na Wanasiasa ni pete na kidole. Hao viumbe huwezi kuwatenganisha.
Isitoshe uchaguzi wa mwaka huu 2020, magufuli hana budi kuwatumia Wasanii wengi kadiri iwezekanavyo ili tu kuwavutia wapiga kura!

Maana hotuba zake zinatabirika! Na zote zimeegemea kwenye ujenzi wa miundombinu tu huku zikiyasahau matumbo ya Wapiga kura. Na kwa bahati mbaya amesahau pia haya mambo huenda kwa pamoja. Hivyo kwa kutumia hao wasanii, walau watu watajitokeza kwa wingi kwenda kuwaona na kuburudika bila kiingilio.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mkuu unakwama wapi. Hata Epikeia kwenye maisha yako umekosa. Hiyo CHadema Ni chama cha Siasa. CCM chama cha Siasa. Hao Ni watanzania Unadhani we unaijua Tz kuliko wewe. Uwe unatumia akili yako. Life is about opportunities. Grab it while you can. Ukitaka kujudge watu vizuri jichunguze. Mfano Hivi CCM ikishinda uchaguzi wao watakuw wapi. Na wewe itakuwaje kwako. Ccm haitawahitaji. Ila chao watakakuwa wamekipata. Very Simple.
 
Wanajua CCM itatawala milele kumbe kwenye maisha kuna miujiza ref Sudan,Libya,Malawi,Ghana,Ghambia nk
 
Nchi ya ahadi au ipi?,au nchi ile ile waliyogomea uchaguzi wa serikali za mitaa?,kipi kimebadilika?,Tume ya uchaguzi ile ile iliyojaa mazonge?...Bongo hakuna uchaguzi,kuna uchafuzi na wapinzani njaa wasio na mipango madhubuti...
 
Uwezekano wa chadema kuchukua nchi mwaka huu ni sawa na barafu kutokea jangwani.

Wasanii wamenusa na kujua hilo. Chadema hawana huwezi wa kuchukua nchi mwaka huu.
 
Back
Top Bottom