Hivi CHADEMA huwa hawahusiki kwenye matukio ya kitaifa?

babu na mjukuu

JF-Expert Member
Jun 23, 2016
2,672
2,000
Muda huu natazama Azam TV wakionesha tukio la kuaga miili ya askari wetu waliopoteza maisha Congo.

Nimekaa nikitafakari kuhusu ushiriki wa CHADEMA kwenye matukio ya kitaifa yasiohusiana na siasa.

Binafsi sikumbuki nilini nimewahi kuwaona hawa makamanda akishiriki kwenye matukio hayo. Iwe ni sherehe za uhuru,ugeni wa kimataifa nk.

Hata kwenye tukio hili, hawapo. Namuona Zitto Kabwe, Lipumba na wengineo. Lakini CHADEMA pamoja na kujiona kwamba wao ni wazalendo kuliko watanzania wote, lakini kwenye matukio ya kutuunganisha wao wanajiyenga. Lakini wakipatwa na tatizo wanakuwa wa kwanza kuomba ushiriki wa wote.

Hivi hata msiba huu kwao wanaona unawahusu CCM tuu?
 

babu na mjukuu

JF-Expert Member
Jun 23, 2016
2,672
2,000
Wangeenda watolewe ili wananchi wafahamu.

Ila kwa cdm wanavyopenda kiki,lazima wangehudhuria watolewe ili wapate kiki yakotokea
 

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,540
2,000
Wangeenda watolewe ili wananchi wafahamu.

Ila kwa cdm wanavyopenda kiki,lazima wangehudhuria watolewe ili wapate kiki yakotokea
Kama wangetolewa ni kwa nini waende?
Na kama basi huwa wanatafuta kiki kwenye matukio kama hayo, hawajaenda sasa nyie mazwazwa mnataka nini?
Na je ccm kama chama cha siasa imewakilishwa na nani, tukiacha viongozi wa kiserikali ambao wamewakilisha serikali??
 

babu na mjukuu

JF-Expert Member
Jun 23, 2016
2,672
2,000
Itifaki inafuatwa, kama hawakupewa mwaliko wa kuhudhuria sasa waende kivipi? Wakifika watakaa kajamba nani? Isitoshe wangejialika wenyewe sasa hivi wangekuwa central polisi kwa kesi ya kuvamia maziko bila mwaliko.. Hii bongo yetu mpya tunaijuwa siku hizi.
Hebu thibitisha kama kuna mualiko uliotolewa kwa viongozi wengine
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,341
2,000
Muda huu natazama Azam TV wakionesha tukio la kuaga miili ya askari wetu waliopoteza maisha Congo.

Nimekaa nikitafakari kuhusu ushiriki wa cdm kwenye matukio yakitaifa yasiohusiana na siasa.

Binafsi sikumbuki nilini nimewahi kuwaona hawa makamanda akishiriki kwenye matukio hayo.
Iwe ni sherehe za uhuru,ugeni wa kimataifa nk.

Hata kwenye tukio hili, hawapo. Namuona Zito Kabwe, Lipumba na wengineo. Lakini CHADEMA pamoja na kujiona kwamba wao ni wazalendo kuliko watanzania wote, lakini kwenye matukio ya kutuunganisha wao wanajiyenga. Lakini wakipatwa na tatizo wanakuwa wakwanza kuomba ushiriki wa wrote.

Hivi hata msiba huu kwao wanaona unawahusu CCM tuu?
Mbona hata Rais hayupo tena yeye ndiye mhusika mkuu Commander in Chief una maana na yeye sio mzalendo.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama hajaenda kuwa salute wanajeshi waliomaliza vita kwa ushindi!

Yuko anafukuzana kukamata dola elfu moja mfukoni mwa msafiri airport!

Unadhani Mbowe angeingia pale na gwanda lake la kikamanda hangepewa kesi ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na sare ya jeshi?

Kusimamia kura zao mliwadakua na kuwasweka lupango sembuse hii inayoweza kuwaweka font fed!!?
 

dindilichuma

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,324
2,000
Mbona hata Rais hayupo tena yeye ndiye mhusika mkuu Commander in Chief una maana na yeye sio mzalendo.
Sioni hoja kwamba kama Rais hajaenda na viongozi wetu wa CHADEMA nao waliwasiliana nae akasema haendi wakasema na sisi hatuendi.
Huu ni msiba wetu ni viongozi wetu, hatuwezi kusubiri kualikwa kwenye msiba sio harusi hiyo wakuu.
Mungu atusaidie kama taifa tuungane pamoja tuwafariji wafiwa nasi sote
 

babu na mjukuu

JF-Expert Member
Jun 23, 2016
2,672
2,000
Kwahiyo thamani ya CDM unataka uione kwenye matukio ya kitaifa tu?

2. Weka Bunge live waonekane.

3. Ruhusu mikutano ili uwaone wakiwasilisha Ujumbe kwa raia.

Wasipohudhuria msibani, uzalendo unakufa mioyoni mwao?
1: Ndio nataka niione thamani ya cdm kwenye matukio ya kitaifa kwani hapo huthibitisha umoja na utaifa wetu.
Mfano wafiwa ndio wapiga kura wetu. Tusiposhirikiana nao,kura watampa alieonesha kuwajali kwenye shida. Zito si mjinga.

2. Bunge live bora limefutwa. Kule walikuwa wanauza sura na kutukana. Hakuna faida yeyote.
Na chama kinachotegemea kujitangaza kwa kufanya vituko bungeni wakiwa live,chama hicho kitakuwa ni muflisi.

3. Mikutano ya hadhara haikuwa na faida. Wala tija yeyote. Mliwafanya vijana washindwe kufanya kazi wawe mateja wa maandamano yenu na mikutano isiyo na faida.
Kama una uthibitisho wa faida ya mikutano hiyo kwa taifa na kuzuiwa kwake kumeleta hasara,tafadhali tuwekee hapa.

Mfano wabunge wanaruhusiwa kufanya kazi na mikutano kwenye majimbo yao. Lakini hawataki hasa upande wa cdm. Kazi yao ni kuchezea ruzuku kidogo wanayopata kustarehe mikoa tofauti kwa kisingizio cha mikutano ya hadhara.
Kwa hili nampongeza JPM.

Mimi mbunge wangu ni Mbowe. Kwakipindi cha miaka 10 ya ubunge wake,hakuna chochote cha kujivunia alichofanya. Zaidi ya matamko uchwara anayoyatoa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom