Hivi chadema haiwezi kuendeshwa bila maandamano na fujo?

nimefikilia sana na nimejiuliza why kila siku ni CHADEMA , CHADEMA....... mgomo wa madaktari CHADEMA , mgomo wa walimu CHADEMA ,ulimboka CHADEMA , kifo cha muuza magazeti CHADEMA , kifo cha mwandishi wa habari CHADEMA .kukataa kutii amri halali za nchi (POLISI) CHADEMA.

hivi huwezi kudai hiyo madai au haki yeyote bila kuwa na vurugu? huwezi kufungua tawi bila vurugu au maandamano isitoshe umeambiwa usubiri ili kupisha sensa hutaki.... sasa mnataka nini..... au kama ndio chama cha upinzani kwani kipo CHADEMA peke yake ????? au ndio kama alivyoahidi baada ya kushindwa kuupata uraisi huyo dokta SLAA kuwa nchi hii haitatawalika . (na mwisho najiuliza hivi je MWANDISHI wa HABARI tena wa PART TIME ...... anayo ruhusa ya kupinga amri halali ya jeshi la POLISI)[/QUOTE]

Nina hofu nawe!
 
Maandamano, mikusnyiko haikwepeki kwenye siasa. Hivi Unaweza kufungua tawi bila watu???? Unataka CDM iwe kama vyama vingine vya upinzani ambavyo hukaa tu kusubiri uchaguzi kisha kushindwa na kusubiri mwingine? Hilo si lengo la chama cha siasa. Kwa nini vibali viwe songombingo kwa CDM? Hivi ile ziara ya kusini Lindi Mtwara ambako vibali havikuwa na zengwe ulipata kusikia shida? Lengo la serikali ni kuleta matatizo kama hayo kwa kuwa wanajua wapo watu wengi wasioweza kuchambua mambo kama mtoa mada na hivyo kuichukia CDM. Its a strategy na inaelekea kufanikiwa kwa Kupe and Yaser
 
YASER PLUUS KUPE I CAN SEE NOW "MASABURI YENU YAPO KAZINI" THINKIN HARD AS HELL.... poleni sana na mnaloooooooo mpaka tutie maguu plot # 1 block # 1 ....i guess you know wara mini....PEOPLEEEEZZZ PAWAAAAAAAA...M4C mpaka kieleweke.

mpaka kieleweke sawa ila msipige kelele nyie si makamanda.mnapiga kelele za nn humu.au hii ni chadema forum na sio jamii forum?
 
mpaka kieleweke sawa ila msipige kelele nyie si makamanda.mnapiga kelele za nn humu.au hii ni chadema forum na sio jamii forum?

wengine tutaendelea kupiga kelele kwa kuangalia maslahi ya Tanzania na Watanzania. tutaipigia kelele CCM sasa,tutawapigia kelele wengine watakao tawala baada ya CCM,lengo ni kuimarisha demokrasia na hali bora zaidi kwa Watanzania. kama kwa akili yako ndogo unadhani inachukiwa CCM basi jaribu kubadilika na kuwa Great Thinker!
 
wengine tutaendelea kupiga kelele kwa kuangalia maslahi ya Tanzania na Watanzania. tutaipigia kelele CCM sasa,tutawapigia kelele wengine watakao tawala baada ya CCM,lengo ni kuimarisha demokrasia na hali bora zaidi kwa Watanzania. kama kwa akili yako ndogo unadhani inachukiwa CCM basi jaribu kubadilika na kuwa Great Thinker!

ishu n kwamba wafuasi wa chadema wamekua co wabunifu wa fikra hata pale viongoz wao wanapunja sheria wao bado wanatetea tu.kwa namna hii hatuwez kujenga nchi.honestly cpend kabisa ccm, chadema walianza kunivuta ila the way wanavyoendesha haya mambo yao now days napata wakat mgumu sana kuona mwangaza huko mbeleni.kwan wamegeuka chama cha waasi?serikali iliyoko madarakan japo hatuipendi ila kuna wakat lazima tuitii kwa namna flan.wamekataza maandamano yann kulazimisha.athari yke ndio hivi watu wanakufa na viongoz wa cdm ndio wanapata pa kusimamaia,hii co ishu kiukweli.hebu tujifunze kwa wenzetu wa kenya walipomtoa moi madarakan cdhan km walitumia hizi njia ambazo cdm wanatumia.mi nawasihi waingie tu chimbo warudi na mbinu mbadala.
 
hivi ule mkutano wa pili uliofanyaika Arusha Unga ltd ambao hata polisi hawakuja kutoa ulinzi palitokea fujo yeyote au mauaji ?
Kuna haja ya kuomba kufanya mikutano miwili bila ya police maana police wanaleta vurugu ili cdm ndio ionekane machoni mwa wengi kuwa wao ndio wanafanya vurugu sasa ndio yanawatokea puani maana wanaenda raia hata wasiohusika ndani ya chama.
 
Kama ukisoma historia ya chama cha NSDP cha ujerumani miaka ya 1920 utagundua modus operandi zinashabihiana kweli na Chadema
 
tunadanganyana nini kwani hujui kuwa ni mbinu za c.c.m kutumia polisi kuua raia kwenye mikutano ya chedema ili chadema ionekane chama cha vurugu na tendwa akifute. kabla ya hpo hukumsikia wasira, ndugu zangu mnafuatila mambo ya siasa ya nchi hii kweli? soma tanzania daima la leo utaelewa kwamba ni mkakati wa c.c.m na jk. daktari kweli umesoma wewe au mzushi tu, huna uelewa wowote wa mambo ya siasa ni bora uachane nayo kwani unajidhalilisha.
 
ishu n kwamba wafuasi wa chadema wamekua co wabunifu wa fikra hata pale viongoz wao wanapunja sheria wao bado wanatetea tu.kwa namna hii hatuwez kujenga nchi.honestly cpend kabisa ccm, chadema walianza kunivuta ila the way wanavyoendesha haya mambo yao now days napata wakat mgumu sana kuona mwangaza huko mbeleni.kwan wamegeuka chama cha waasi?serikali iliyoko madarakan japo hatuipendi ila kuna wakat lazima tuitii kwa namna flan.wamekataza maandamano yann kulazimisha.athari yke ndio hivi watu wanakufa na viongoz wa cdm ndio wanapata pa kusimamaia,hii co ishu kiukweli.hebu tujifunze kwa wenzetu wa kenya walipomtoa moi madarakan cdhan km walitumia hizi njia ambazo cdm wanatumia.mi nawasihi waingie tu chimbo warudi na mbinu mbadala.

mdogo wangu,mfano wako wa Kenya sijui kama unaelewa historia ya ukombozi wa pili wa Kenya ulivyopatikana mpaka Moi akasalimu amri kwa kuitisha uchaguzi huru! ningekuelewa kama ungeshauri watawala wa sasa wangeiga mfano wa Moi ambaye baada ya kugundua upepo wa mageuzi ulikua unavuma dhidi yake na KANU aliamua kuondoka kabla ya shari kamili. licha ya madhila makubwa aliyowafanyia Wakenya,lakini mpaka sasa anaishi kwa amani ktk nchi yake.
 
ngoja nijaribu kukujibu japo naona kabisa kichwa chako ni kizito. sema serikali iliyopo madarakani itangaze kuwa haitaki tena vyama vingi. au serikali/chama tawala itangaze kuwa kama chama pinzani kinataka kiendelee ku-exist shurti wafanye kama kitakavyo chama tawala. kinyume na hayo kupe, usitegemee jibu.
raia wamekipenda chama cha cdm sana, wakisikia chochote wanamiminika-wengi, ni kama mfano wa enzi zile Yesu akisikika yuko wahali, walimiminika watu wengi, wakamsikilize, walipenda mafundisho yake. sasa kwa tanzania watu wamekata tamaa na chama tawala kiasi kwamba wakisikia cdm ina event 'yoyote' wanajaa.
kwa hilo ccm linawakera mno, wanaamua kutumia kila mbinu kudhibiti hiyo kitu, lakini sio rahisi sana, kwa hiyo wanaamua lolote na liwe- ndio maana unaona watu wanauwawa. cdm ni kisingizio cha kulazimisha tu, na watu wanaona na kuelewa. umeelewa kupe?
 
Chama chakavu CCM, 50yrs old hawana majibu ya shida za wananchi, wanaamini kuua raia kwa kutumia polisi na kuipakazia chadema kutawakubalisha kwa umma wa watanzania...Nasubiri waikataze TBC kuonesha vikao vya bunge ili kujificha na aibu ya kuambiwa watekeleze ahadi zao na bw mdogo chadema mwenye miaka 17
 
Hauitendei haki elimu yako kabisa! Inasikitisha sana unapoleta ushabiki wa vyama kwenye mambo ambayo hayana uhusiano na siasa. Madaktari walipogoma hawakuwa na uhusiano na siasa kama utabisha ntakuacha kabisa kwa sababu hauwezi kuelewa kwanini nakuambia hivyo and i will not waste my time trying to convince you! Kwa hili la kufa mwandishi halina connection kabisa na siasa. U have to know bila waandishi wa habari usingejua huyo mwandishi ameuwawa, usingejua kitu gani kinatakea around the world my friend. Waandishi wa habari wanalindwa na sheria za nchi zote kutafuta na kupata habari, but only cruel people hawaelewi wanaua, wana kidnapp na kutesa waandishi wa habari. Let us call Dog a dog and Monkey a monkey.

Jibu hoja bwana mdogo. umeulizwa why CHADEMA? hujaulizwa umuhimu wa waandishi wa habari. Understand?
 
Tatizo hakuna aliyejibu hoja as mnavyojiita great thinker. Nimeuliza hivi huwezi kufungua tawi la chama chako bila maandamano, mkusanyiko au vurugu? Sheria inakutaka uombe kibali unapotaka kufanya maandamano au mkusanyiko . Wewe hujaomba na unafanya mkusanyiko wako bila kibali. Sasa hapo si umevunja sheria. Polisi inakuonya hutaki. Inakufukuza pia hutaki. Sasa unataka wafanyaje? Au basi tuamue kitu kimoja tuwe hatuna jeshi la polisi wala serikali tuwe kama somalia? Kuna wengine wanapenda maandamano na wengine hawapendi. Kwenye mkusanyiko lolote linaweza kutokea kuna kuibiana , kuvunjika kwa amani, vifo etc. Na madhara yeyote yakitokea wa kwanza kulaumiwa ni polisi. Sasa kwanini tusitii amri ya polisi?

You are extremely right brother
 
tatizo letu hapa ni ushabiki unaoletwa bila kupambanua pumba na mchele. Ukweli ni kwamba CHADEMA lazima wafanye fujo ili wasije wakaulizwa mambo ya msingi ya kitaifa kwani hawana majibu. Ndio maana mikutano yao imejaa 'blames' lakini haina 'solutions' kwa matatizo ya wananchi. Nina uhakika hata hao washabiki wao hawawezi kusimama na kusema mwelekeo wa CHADEMA ni huu. Badala yake wanaelekeza mawazo yao katika kuchukua utawala. Swali: wakishachukua utawala wana stratejia gani katika kurekebisha mambo hapo hawana njia wala jibu wala mtizamo. kwa kifupi sera za CHADEMA ni kuchukua nchi; so what. Inapofikia hapo ndipo wanapolazimisha kufanya mambo nje ya sheria ili watu wenye akili wasipate nafasi ya kuwahoji. Si mnakumbuka Slaa alivyoshindwa kujibu swali rahisi kutoka kwa Mmachinga wa Mpwapwa kwenye kampeni za urais 2010? Sasa wana nini zaidi ya fujo tu?
 
Mimi shida yangu ni jinsi FFU wanavyodhibiti ghasia. Utakuta polisi 6 wamemzibiti raia mmoJa, hana silaha wala hafurukuti lakini cha ajabu hawa jamaa watampiga vibaya hadi hata kumvunja. Hii ndio nini hasa
 
hivi ule mkutano wa pili uliofanyaika Arusha Unga ltd ambao hata polisi hawakuja kutoa ulinzi palitokea fujo yeyote au mauaji ?

Walipata habari za kiintelejisia kwamba hakutakuwa na vurugu au kuvunjika amani.
 
Back
Top Bottom