Hivi CHADEMA haina wataalamu, au viongozi wake ndiyo wasioambilika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi CHADEMA haina wataalamu, au viongozi wake ndiyo wasioambilika?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dabomani, Oct 7, 2010.

 1. D

  Dabomani Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa tunaishi katika kipindi ambacho wataalamu na wanahistoria ya maendeleo ya kitekinolojia katika ulimwengu wanakiita 'information age', yaani kipindi cha 'habari na mawasiliano'. Kwa mujibu wa wataalamu na wanahistoria hawa, kipindi hiki kimeanza mwanzoni mwa miaka ya 1990, na kuchukua nafasi ya kipindi kilichotangulia ambacho wenyewe walikiita 'industrial age', yaani kipindi cha 'mapinduzi ya viwanda'.
  Tofauti na huko nyuma, hiki ni kipindi ambacho taarifa na habari zinatembea kwa kasi kubwa sana na kuwafikia watu wengi zaidi kuliko muda mwingine wowote ule katika historia ya mwanaadamu. Aidha ni kipindi ambacho taarifa na habari mpya zinazoingia na kusambaa ulimwenguni kila siku ni nyingi mno, kiasi kwamba mtu anayetaka kwenda sambamba na wakati, analazimika awe ni mwanafunzi wa kudumu.
  Wataalamu wa tekinolojia ya habari na mawasiliano wanakisia kuwa kila baada ya miezi kumi na nane habari zinazohusu nyanja mbalimbali zinazoingia na kusambaa ulimwenguni zinaongezeka mara dufu!
  Maendeleo katika tekinolojia ya computer yaliyopelekea kuvumbuliwa kwa computer ndogo za mezani na mapajani; uvumbuzi wa mtandao wa kidunia wa internet (world wide web) unaowawezesha wamiliki wa computer duniani kote kujiunga na kisha kupokea, kutuma, kubadilishana, na kupashana habari; na ujio wa mawasiliano ya simu za kiganjani, kwa pamoja ndiyo yaliyozaa kipindi hiki.
  Kipindi hiki kimezaa mabadiliko makubwa sana katika nyanja zote za maisha. Mifano ni mingi sana inayoweza kutumika kulidhihirisha hili.
  Hebu tutazame mifano michache: Kiasili, serikali ni taasisi ambayo ina umbile la piramidi. Juu zaidi kuna raisi, au waziri mkuu, au mfalme, nakadhalika. Chini ya huyu kunaweza kuwa na makamu wa raisi na waziri mkuu, ambao chini yao nao kuna baraza la mawaziri. Mtiririko huu unakwenda mpaka tunampata mtendaji wa mtaa au kijiji, nakadhalika.
  Katika umbile la namna hii tunapata kitu kinachoitwa URASIMU. Jambo zito na lenye uwezekano wa kutikisa Taifa zima linaweza kutokea katika ngazi ya kijiji, lakini hadi raisi apate taarifa za jambo hilo, inaweza kuchukua muda mrefu na pengine asipate taarifa hizo kabisa. Kinachotokea ni kwamba mmoja au baadhi ya viongozi walioko kwenye ngazi za kati, kwa ajili tu ya kulinda maslahi yao, au kwa hofu wanaamua kuacha kuendelea kutoa taarifa katika ngazi zinazofuatia juu yao.
  Hapa nchini miaka ya nyuma kuna maeneo yalikuwa yanakumbwa na njaa hadi baadhi ya Wananchi wanapoteza maisha yao, lakini viongozi wa juu wa serikali wanaishia kupata taarifa hizo kupitia vyombo vya habari. Hali hii ilijitokeza kwa sababu tu viongozi wa ngazi za chini au waliogopa kutoa taarifa, au kuna ambao katika mnyororo huo wa kupeana taarifa walizembea; na mawasiliano na ngazi za juu yakakatika.
  Katika kipindi hiki cha habari na mawasiliano, urasimu wa namna hii unapaswa kuwa historia tu. Pamoja na kwamba umbo la serikali linabaki ni lile lile la piramidi, lakini iwapo kila ofisi ya serikali kuanzia juu hadi chini imeunganishwa kimawasiliano na mtandao wa internet, upashanaji wa habari unabadilika na kuchukua umbo kama la uso wa maji.
  Ukidondosha kijiwe katikati ya uso wa maji yaliyotuama, mawimbi yanasafiri kutoka hapo kijiwe kilipodondokea na kuelekea pande zote juu ya uso huo wa maji, tena kwa wakati huo huo. Kama ilivyo kwa mawimbi katika uso wa maji, barua pepe moja iliyoanzia kwa mtendaji wa kijiji kimoja, mathalani kule Rukwa, inaweza kumfikia katibu tarafa, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, waziri mkuu, na raisi kwa wakati huo huo mmoja. Hii ina maana kwamba kama serikali haikuchukua hatua zinazotakiwa kwa wakati muafaka, tatizo halitakuwa tena ni la urasimu katika kupeana taarifa, ila litakuwa ni kutokana na sababu nyingine, kama uzembe, nakadhalika.
  Hebu sasa tuangalie ulimwengu wa kibiashara. Kwa wafanyabiashara walioridhia kuwekeza muda na kujifunza, kipindi hiki cha habari na mawasiliano ni kipindi ambacho kimezaa fursa zisizo na kifani.
  Kwa mfano: Kama una bidhaa unauza, na hujui soko liko wapi, unachotakiwa kufanya ni kujisajili tu katika moja ya masoko makubwa ya kwenye mtandao, mathalani Alibaba.com, na kuorodhesha bidhaa ulizonazo nazo. Kwa uhakika kabisa, kabla ya masaa ishirini na nne kupita, utaletewa orodha ndefu ya wafanyabiashara duniani kote na anuani zao, ambao wanatafuta bidhaa unazouza.
  Au mathalani, umebuni mradi mzuri lakini kikwazo chako ni mtaji. Kuna mitandao kadhaa ya wawekezaji ambayo ukishajisajili – kuna gharama kidogo unalipia – unaruhusiwa kuwasilisha muhtasari wa business plan yako, yaani muhtasari wa andiko la mradi wako. Wanachama wa mtandao husika watapata fursa ya kupitia muhtasari huo, na wale watakaovutiwa watawasiliana na wasimamizi wa mtandao, ambao nao watakupatia orodha na anuani za wawekezaji hao ili muweze kuwasiliana na kujadiliana. Mwisho wa yote wawekezaji hao watataka walione andiko lote la mradi wako, na kama umeandika kitu cha uhakika, usishangae kukuta unapata watu kutoka Ulaya, Australia, India, Marekani nakadhalika; ambao wako tayari kutoa fedha zao wawekeze kwenye mradi wako kabla hata hamjaonana uso kwa uso!
  Hali iko hivyo hivyo kwa wanaotafuta elimu mbalimbali, mafundi wanaokarabati mashine mbalimbali, madaktari wanaohangaika na magonjwa yanayotatiza, watafiti katika fani mbalimbali, nakadhalika.
  Kwa mfano: Mwanafunzi anayesomea shahada ya uzamifu hapa kwetu Tanzania anaweza akapata tabu sana kufanya utafiti wa maandiko (literature search) juu ya fani husika, iwapo tegemeo lake pekee ni hizi maktaba zetu. Hii inatokana na ukweli kwamba maktaba zetu zina upungufu mkubwa wa vitabu na majarida ya kitaaluma, kutokana na gharama kubwa ya kuagizia vitu hivyo. Hata hivyo tatizo la mwanafunzi huyu linaweza likamalizika ndani ya muda mfupi sana kwa kutumia mtandao. Kuna maktaba nyingi katika mtandao zilizosheheni kila aina ya vitabu na majarida ya kitaalamu; unachotakiwa tu ni kujisajili na kufumba na kufumbua, nyaraka katika fani unayotafiti zitakuwa mbele yako kwa mamilioni.
  Uzuri wa kipindi hiki ni kwamba siyo rahisi tena kudanganya na kuzuia habari kama ilivyokuwa siku za nyuma. Habari inaweza kutokea katika jiji la Mbeya leo asubuhi, na kwa ajili maslahi fulani fulani, ikamuuliwa kwamba taarifa zile zisifikishwe kwa Wananchi kupitia vyombo vya habari vya kawaida yaani Radio, TV na magazeti. Wakati miaka kumi iliyopita uamuzi huu ungekuwa ni wa busara kwa hao wenye kuutoa, leo hii utakuwa ni uamuzi wa kuchekesha. Utaachaje kuwa ni uamuzi wa kuchekesha wakati huenda hata kabla ya kikao kinachotarajiwa kutoa maamuzi ya kuzuia habari husika isitangazwe kuketi, habari hiyo itakuwa tayari imeshasambaa nchi nzima kwa njia ya SMS na barua pepe?
  Hivi sasa tuko katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, 2010. Wagombea mbalimbali wa nafasi za udiwani, ubunge na uraisi wameendelea na kujinadi, na katika kujinadi kwao tumesikia mengi. Uzuri wa kipindi hiki cha habari na mawasiliano ni kwamba, ni rahisi kujua yapi kati ya yanayonadiwa na wagombea yanawezekana; na yapi hayawezekani.
  Naomba nisieleweke vibaya. Kila kinachonadiwa kinawezekana, lakini kuwezekana kwenyewe kunategemea na mazingira ya eneo husika na wakati unaohusika. Kuna mambo mengi ambayo yanawezekana Ulaya, Marekani, Japan, na katika nchi nyingine zilizoendelea lakini hayawezekani katika mazingira ya Tanzania ya leo. Kwa mfano mgombea akijinadi kuwa mkimchagua ataweka treni ya chini ya ardhi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, moja kwa moja unajua kuwa kwa mazingira ya Tanzania ya sasa mgombea huyu ana walakini. Lakini ahadi hiyo hiyo ikitolewa na mgombea aliyeko Ujerumani, Kanada, au nchi nyingine yoyote iliyoendelea, wala watu wa huko hawatapoteza muda wao kujadili; kwa mazingira ya kwao hilo ni jambo la kawaida kabisa; linawezekana.
  Miongoni mwa wagombea uraisi ambao wamekuwa wakitoa ahadi ambazo kwa mtizamo wangu zina walakini mkubwa, ni Dr. Slaa wa CHADEMA. Miongoni mwa ahadi hizo ni ile ya kuweka treni ya masaa matatu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam, na ile ya kushusha bei ya saruji hadi shilingi 5,000.00 kwa mfuko wa saruji wa kilo 50.
  Tuanze kwanza kuangalia hii ahadi ya treni. Umbali kutokaMwanza hadi Dar es Salaam ni kilometa 1,229. Ili kuwa na treni ya kuweza kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa masaa matatu, itailazimu treni hiyo iwe na mwendo kasi wa kilometa 410 kwa saa moja! Hivi sasa treni inayoshikilia rekodi kwa mwendo wa kasi ni ile ya Maglev inayofanya safari zake kati majiji ya Shanghai na Beijing, kule China. Treni hii ina mwendo kasi wa kilometa 431 kwa saa. Treni nyingine maarufu duniani kwa mwendo kasi ni Shinkasen ya Japan, kilometa 260 kwa saa na Eurostar ya Ulaya, kilometa 250 kwa saa!
  Katika Tanzania ya leo ahadi ya Dr. Slaa ni kiini macho kwa sababu nchi hii kwa sasa hata uwezo wa kuwapatia Wananchi wake wote milo mitatu kwa siku haina; achilia mbali ukweli kwamba zaidi ya asilimia 40 ya bajeti ya nchi inategemea zaidi wahisani. Sasa kama hao wanaotufadhili wenyewe bado treni hiyo ya mwendo kasi wa kilometa 410 kwa saa hawajawa nayo, sisi tunategemea treni hiyo tuitoe wapi?
  Tukija kwenye ahadi ya kuuza mfuko wa saruji kwa shilingi 5,000/- tu, hapa napo inabidi tujiulize: Hivi CHADEMA haina wataalamu wa uchumi, au mgombea wao ndiye asiyeambilika? Katika uzalishaji wa saruji, kuna malighafi muhimu inayoitwa CLINKER. Hivi sasa Tanzania ina uwezo mdogo sana wa kutengeneza malighafi hii; na viwanda vyote vya saruji nchini inabidi kuiagiza kutoka nje ya nchi.
  Nchi maarufu kwa uzalishaji na ambayo inaiuza malighafi hii kwa bei rahisi kuliko nchi zote ni China. Katika masoko ya China, kilo 50 ya Clinker inauzwa kiasi cha shilingi 3,902/- kwa sasa. Hii ina maana kuwa pamoja na gharama za usafirishaji hadi katika bandari ya Dar es Salaam, gharama za kuipakua, kuihifadhi, kuitoa, na hatimaye kuisafirisha hadi kiwandani, malighafi hiyo inaweza kufikia gharama ya shilingi 4,500/-; bila hata kulipiwa ushuru wa forodha.
  Malighafi hii ikishafika kiwandani inatakiwa sasa ichanganywe na malighafi nyingine zinazopatikana nchini, mathalani 5% - 8% jasi (gypsum), kabla ya kutiwa kwenye mtambo wa kusagia ili kupata saruji yenye ulaini unaotakiwa. Iwapo kilo 50 ya malighafi hizi inafikia shilingi 500/- tu kwa mfano, hii ina maana kuwa hata kabla ya kuinjikwa kwenye mtambo wa kusagia, tayari saruji ghafi yetu imeshatugharimu shingi 5,000/-.
  Katika gharama hii ongezea gharama ya nishati inayotumiwa katika mtambo, gharama za kuiweka saruji iliyo tayari kwenye vifungio, gharama za upakiaji na usafirishaji hadi kwa mawakala, na gharama za utawala; ambazo kwa mfano tu, tuseme ni shilingi 500/-. Sasa hata kabla kiwanda hakijaweka faida yake na kulipa kodi yoyote ile ya serikali, tunaona kuwa tayari gharama ya mfuko mmoja ishafika shilingi 5,500/-. Ukiweka faida ya kiwanda ambayo ni asilimia kati ya 7 na 9, utagundua kuwa mfuko mmoja wa saruji kwa mahesabu ya chini kabisa ambayo hayajumuishi kodi yoyote ya serikali ni shilingi 5,940/- kwa bei ya kiwanda. Ongeza na bei ya mawakala wasambazaji wa kiwanda na wauzaji wa jumla na rejareja, utagundua kuwa hata bila kulipiwa kodi yoyote ile, haiwezekani saruji ikauzwa chini shilingi 6,500/- kwa mfuko wa kilo hamsini.
  Njia pekee ambayo Dr. Slaa ataweza kutuuzia mfuko wa saruji kwa shilingi 5,000/- ni iwapo tu serikali yake itakuwa inatoa ruzuku kwa wazalishaji wa saruji. Swali linakuja:Ruzuku hiyo itatoka wapi?
  Narudia tena: Hiki ni kipindi cha habari na mawasiliano. Ni kipindi kigumu sana kudanganya, na hasa lengo linapokuwa ni kuudanganya umma. Inawezekana CHADEMA haikuwa na nia ya kutudanganya, lakini wanawezaje wakajitetea kuwa wamekuja na ahadi nzito kiasi hicho bila kufanya utafiti? Tangu kampeni hizi zimeanza chama hiki kimefanya makosa mengi mno ya kiufundi na ya wazi, kiasi kwamba mtu unabaki ukiwa umepigwa na bumbuwazi. Ni vipi chama kichanga kiasi hicho kiwe na matumaini ya kupewa ridhaa ya kuongoza nchi? Ushauri wangu kwa CHADEMA ni kwamba viongozi na wagombea wake wawe wanatoa ahadi baada ya kuzifanyia kazi; vinginevo watagundua kuwa Watanzania wanaowadhania ni wajinga, kumbe ni wajanja kuliko wao.
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Uuuhhh!!! Nitamalizia kusoma hii post baadae, am half-way, tired
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mkuu tafadhali edit, weka paragraphs, ikiwezekana kuza maamdishi kidogo. Wengine humu macho yetu ndio hivyo tena.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Unajua wewe ni pasua kichwa kwa upembuzi wako huu ambao unakataa kutambua mchango wa CCM na hususani JK katika kuturudisha nyuma KIMAENDELEO. Hoja kama hizi nitakazozinukuu ulipaswa uzitafutie chanzo kabla ya kuzitumia kama ni sababu ya sisi kuridhika na umasikini:-

  Usichojua ni kuwa JK na CCM yake wanatoa ruzuku kwa wawekezaji wakubwa lakini mpigakura ng'o hapati kitu. Dr. Slaa anachosema zigo la kuwabeba wakuja sasa mwisho wake umefika na zamu hii mpigakura naye ajinome nchi yake sasa hili linakukera vipi?

  Kwa mwaka JK na CCM yake walivyo wanoko wanatoa misamaha ya kodi ya zaidi ya Tshs 700 bilioni, sasa ukiwa na hili fungu lenye neema kebekebe kwa nini usiwe na kiburi cha kufikiria majibu ya matatizo yetu?

   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante Rutashubanyuma. Hata hiyo article siisomi tena.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Huyo jamaa ni mhuni...
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hii mada haina urafiki na msomaji!
  BTW, Thank you!
   
 8. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duuuuuuh. mkubwa hayo magazijuto uliyoyashusha hapo juu mimi hoi, tuambie unafanya kazi TWIGA CEMENT au kiwanda gani cha Saruji? Au kaka ni mgazijuto hayo yanatokana na utafiti wako juu ya uzalishaji wa saruji?

  ETIIIII DKT SLAA kahaidi Kuhusu kuanzisha treni itakayofanya safari toka mwanza hadi Dar kwa masaa matatu hiyo kali. Kwa uchumii huuu wa BONGO au wa JAPAN? mimi binafsi sijapata kumsikia DKT akitoa ahadi hiyo kama kweli mi simo.

  WanaCHADEMA mpo wengi humu JF embu tujuzeni ni kweli ahadi ya TRENI iendayo kasi imetolewa na DKT.

  DABOMANI embu nifanyie uchambuzi wa kimagazijuto maana wewe ni mtaalam wa namba kwa ahadi za Mgombea DKT (wa heshima) JK kama zinatekelezeka ndani ya miaka 5 au laa maana yeye anaongoza kwa ahadi anafuatia na DKT (waukweli) SLAA na PROF (wa ukweli) LIPUMBA
  1. ujenzi wa reli mpya na ununuzi wa treni yake
  2. ujenzi wa viwanja vya ndege vi 3 vya kimataifa
  3. Ununuzi wa meli kubwa mbili
  4. ujenzi wa hospitali 6 za rufaa
  5. ujenzi wa hosp ya magonjwa ya moyo
  Kwangu ni hayo tu ahadi nyingine achana nazo,

  ktk majibu yako zingatia utendaji wake wa miaka 5. pili muda unaotumika kukamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege songwe mbeya(miaka 10 sasa imepita) na ufisadi uliotamalaki nchini.
   
 9. m

  mozze Senior Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Kwanza lazima ujue kila serekali ina vipaumbele vyake. Dr. Slaa ameshaainisha jinsi atakavyo finance hiyo miradi na ahadi za Chama. JE WEWE UNAKUBALIANA NA MGOMBEA ALIYESEMA ATASAMBAZA LAPTOP KWA WANAFUNZI WOTE? MBONO UKO KIMYA JUU YA HILO.

  Ukumbuke Serekali ina uwezo wa kutoa "SUBSIDY" kupunguzia wananchi makali, pamoja na kupunguza kodi, kupunguza gharama za uzalishaji kama kwenye Nishati na usafirishaji na vitu kama hivyo. Kama unafuatilia tu, kuna nchi kama Korea Kusini, Leo Serekali imeamua kuagiza cabbage (maarufu kwa kutengenezea kitu kinaitwa Kimchi) na kuwauzia wananchi kwa bei ya chini kwa sababu mwaka huu wazalishaji wa ndani hawakufanikiwa. Zaidi nchi kama USA, na EU wanatoa Subsidies kwa wakulima wao kufanya maisha ya wananchi kuwa rahisi. Kwa TZ pia inawezekana, its just a matter of Priorities!

  Kuhusu train, inawezekana mkubwa alikosea tu kusema. Kwenye Ilani hawajasema muda wa train, lakini core point ni kuwa Chadema wanakusudia kuweka treni ya kisasa, badala ya hii ya sasa ambayo CCM wameipokea toka Mjerumani na wameshindwa kuweka usimamizi hadi imekufa.
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Umeshakuwa msemaji wa chadema sasa...! Mbaya zaidi hata huna hakika kama alisema hivyo ama la! Pole
   
 11. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe kibunango sio unatoa support tu bila kutafakari kama umetoka usingizini. Fanya mchanganuo wa mahesabu kuhusiana na AHADI za DKT wa chama cha jembe na nyundo utubainishie kama zinatekelezeka au la na CHADEMA fanyeni mahesabu kuhusiana na ahadi za DKT SLAA je zina tekelezeka au magumashi. Kama vp tumchague fami DOVUTWA wa UPDP atujengee kiwanda cha silaha ili wabongo tufanye biashara ya maana na SOMALIA, CONGO na tuendelee kuyachonganisha mataifa ya maziwa makuu ili tuuze silaha zetu kwa wingi. Maana tusiwe tunatoa ushabiki tu bila kufanya uchambuzi yakinifu kwa wagombea wetu.

  unaandika POST kubwa ndefu kuhusu mgombea wa chama tofauti na chako kuhusu ahadi zake kutotekelezeka je mnatafakali na ahadi za wagombea wenu?

  ACHENI mahaba na kupenda kwa kibwege, mimi naendelea kumkataa DKT wa heshima JK maana aliyoahidi 2005 ajatekeleza yote antulazimisha tukubali kuwa katekeleza yote. mimi sichagui waongo na wanao beba mafisadi hivyo kwa huyu heri nimchague KUGA MZIRAY KULIKO JK. CHADEMA mteteeni DKT SLAA na kutushawishi tumchague teteeni kwa hoja na si jazba
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  madrassa al sul
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Dabomani,

  Mbona hushangai ahadi ya:

  1. Kigoma kuwa Dubai.
  2. Mwanza kuwa Carlifonia??
  3. Uwanja wa ndege Mbeya, Kigoma, na .................. (hebu ongezeeni).
  4. Ongezeko la Mishahara ambalo baadaye wamekana kuwa si kweli.
  5. Kuleta maji Tanga wakati Dar penyewe hayapo.
  6. Barabara za Fly-oveer Dar na ujenzi wa njia za Rapid Bus ambao waliahidi tangu mwaka 2005.
  7. Umeme wa uhakika na tukaishia kupewa RICHIMONDULI.
  8. Wanafunzi wote Tanzania kuwa na Laptop wakati umeme hamna.
  9. Ameahidi BAJAJI 400 kwa akina mama waja wazito. Hebu muone mama na mtumbo kwenye Bajaji.
  10. Katujengea bora shule Tanzania nzima badala ya shule bora. Hii katimiza ahadi.

  Mengine mengi watakuja jamaa wengine waongezee.

  Naona mkuu umekaa sana Majuu na kusahau kuwa Tanzania iko bado vilevile. Unafikiri huku kila mtu ana Internet. Sanasana ni watu kuwa na simu na siyo Internet. Rudi uone RUMBA la Tanzania ndiyo uanze kukosoa. Wengi wanaoshinda humu sidhani hata watapiga kura. Hivyo kama wahutubia basi mbegu zako zimeangukia kwenye Miiba na Magugu.
   
 14. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hili li-article halina urafiki na wasomaji. Weka walau aya basi tuweze kusoma hii post yako. Dah!
   
 15. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ACHA KUKURUPUKA wewe, Swali nimeuliza mimi, wewe unaanza kihere here chako. nimekupa na wewe kazi ya kufanya mahesabu ya AHADI ya chama chako jembe na nyundo utueleze kimahesabu kama zinatekelezeka au la. Pili zipo kwenye ilani yenu ya chama au niza mgombea wenu na si za chama. katika mchanganuo wako usisahau na ahadi ya BAJAJ 400 kama zipo ktk ilani yenu au siku mgombea wenu wakati anautubia aliona BAJAJ inapita mbele akaona ni mtaji hivyo akatoa ahadi
   
 16. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbinu Dabomani aliyokuja nayo ni 'persuasion' nayo kwenye uwanja wa vita inakubalika. Thx though
   
 17. p

  pierre JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa wasomi wanajua mtu anaposema mission and vision.Inasemekana 'Without vision people perish'.Tunapoongelea kuhusu peponi hatujafika but we are on the way.Kusema tunataka tuwe na treni inayokwenda Mwanza kwa lisaa limoja hiyo ni sawa ndiyo vision yenyewe,tunataka tufike mahali mfuko mmoja wa cemenmt uuzwe 5,000/= hiyo ni sawa.Nikuulize swali je ulitaka aseme kuwa atatengeneza treni ya kwenda Mwanza kwa mwezi mmoja?au ulitaka cement iwe Tshs.50,000/= ukiona mtu anayefanya hivyo,huyu anatafuta kifo.We are striving to mkae life better and not to make it worse.
  Tafakari chukua hatua.Piga kura 31.10.Mpe mtu mwenye VISION anayeleta MATUMAINI na siyo KIFO kwa kusema hili HALIWEZEKANI.
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Watu kama huyu dabomani wanaotumia muda mwingi madrassa hawawezi kukuelewa
   
 19. Samawati

  Samawati Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 13
  TOO MUCH OH!.....
  CHADEMA ni chama makini... kina watu wenye uwezekano wa ku turn around this country. Wakipewa nafasi watafanya mengi ila tusisahau kuna majaribio yenye gharama kubwa.CCM na serikali yake wamefaidika na vipindi virefu vya kujaribu, kukosea na kujaribu tena bila kuwekwa kati na kusutwa na wananchi.Nawahurumia sana kama wakishinda huu uchaguzi.
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni chadema na ahadi za kihuni! Hata wafuasi wake wengi ni wahuni na mfano mojawapo ni wewe mwenyewe! Hebu angalia lugha uliyotumia katika posti yako hapo!

  Zaidi nimeona uchambuzi wako yakinifu!
   
Loading...