Hivi CCM wanaweza kujisifia kuhusu haya yanayofanywa na Magufuli?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Watanzania wenzangu ebu tujiulize maswali haya;

Hivi ni serikali ipi iliyotengeneza hayo majipu yanayotumbuliwa leo?

Ni chama gani kilichokuwa kinatetea kwa nguvu zote kwamba serikali ya awamu ya 4 ni nzuri sana?

Kama kweli serikali ya awamu ya 4 inakusudia kutumbuwa majipu yote kwanini isimkamate yule aliye create hayo majipu?

Hivi kwanini ccm wasitoke hadharani kuwataka radhi watanzania kuwa waliwafanya vibaya kutetea wizi uliokuwa unafanywa na serikali ya kikwete.

Kwani ni dhambi kwa CCM kutoka na kuwasifia wapinzani waliogundua ubadarifu ulikuwa unafanywa na serikali ya awamu 4 pamoja na safari za nje zilizogharimu pesa nyingi za umma ambazo walikuwa watetea kwamba safari hizo zimeleta mafanikio makubwa?
 
Majipu yanaanzia kwa mzee "Ruksa - AHM" na kumea vizuri kwa "Mr Clean - BWM" kisha "mzee wa Msoga - JKM" akayapalilia na kuyatia dawa ya kujivimbia vizuri.

Sasa ngoja tuone kama watatumbuana wao kwa wao. Huu ni usanii tu wa JPM na yeye mwenyewe ni jipu baya lililokwisha iva na linalisubiri kuja kutumbuliwa mwaka 2020!!

Mla ni lazima naye huja kuliwa tu. Na tusisahau kuwa CCM ni ileile na mfumo wake ni uleule!!
 
Back
Top Bottom