Hivi CCM wanatambua kua Lowassa anawonea huruma?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza bwana mmoja kwa kujaribu kujitambua kua anamheshimu sana Mh Lowassa, hivi ndivyo inavyotakiwa na wanatakiwa wajitokeze na wengine kusema wazi kua wanamheshimu mzee wa kazi!

Nirudi kwenye mada;Kwa historia ya Mh Lowassa ndani ya CCM yeye na Mzee Kingunge ndio watu wenye mchango mkubwa katika chama hicho kuliko hata hao waliokua wakiropoka hadharani na kuwapakaa matope bila aibu wada adabu,Lowassa huyu anayekifahama chama cha mapinduzi kwa muundo wake wa ndani na nje aamue sasa anataka kukiua chama cha mapinduzi bado kutakua na chama hapo? Lowassa huyu huyu ambaye baadhi ya makada wa CCM wanatamka wazi wazi kua msaada mkubwa kwa ushindi wa CCM katika chaguzi zilizopita?

CCM wanashindwa kuelewa kua ndani yao bado kuna masalia watiifu kwa Mh Lowassa na wanashiriki vikao vizito vya chama,CCM wanasahau kua ukimya wa Mh Lowassa baada ya uchaguzi kuliwapa uchungu mkubwa wafuasi wake ndani na nje ya chama? CCM wanasahau tu baada ya Lowassa kikatwa pale mjini Dodoma ukumbi ulizizima kulitajataja na kuliimba jina lake tu"Tunaimani na Lowassa"? CCM wanafikiri maswahiba wa Lowassa ndani ya chama chao watasambarika kirahihisi tu? CCM walishawahi kusikia Lowassa akiwaponda waliosalia CCM? Kama sio wanadhani watamchukia swahiba wao kirahisi tu?

Nafikiri hapa ni kama Lowassa amewasamehe na kuwahurumia maana hawajui watendalo, Lowassa ni bingwa wa siasa za Tanzania ila ameamua kutanguliza busara na kuutambua uwepo wa Mungu, Kulithibitisha hilo ni pale ambapo katika kampeni zake hakuwahi kumshambulia wala kumtukana mwanaCCM yeyeote wakati wao wanamsakama kwa matusi.Nina uhakika Lowassa akitamka mdomoni mwake Leo"Nataka kuisambaratisha CCM" kitakua ni kilio cha kusaga meno kwa CCM.
 
Watu wa Lumumba na Ufipa karibuni.Mada imeshachokozwa.Mzee Tupa Tupa unasemaje kwa andiko hili? Yeriko Nyerere sogea kwenye 'keyboard' hapo.
 
Hizi ngonjera za kwamba lowasa akihama ccm itapasuka zimeanza tena??

Sasa naelewa kwa nini Lowasa alisema elimu elimu elimu kumbe alijua anaongoza watu Wenye uelewa Wa kwenda chooni na kupayuka hovyo
 
Tunamshukuru sana kuwaonea huruma CCM, tunaomba aendelee na moyo huo huo
Mtoa mada umesema ukweli kabisa mada bila Lowassa kuhama na kingunge CCM isingeshinda kwani walikuwa wameichafua mno hao wazee kiasi kwamba wapinzani wangepata cha kusema. Ushauri wangu,Lowassa mzee Lowassa tunakuomba baba ukaze kamba uendelee kuionea huruma CCM ili 2020 ugombee tena urais then CCM ipate tena mteremko. Asand mleta mada kwa kutufumbua macho.
 
Lazima CCM imshukuru Lowassa. Kama sio Lowassa CHADEMA bado ingekuwa inaitesa CCM kwa hoja za ufisadi. Ujio wa Lowassa CHADEMA ulineutralise hoja ya ufisadi na kuipa CCM ahueni kubwa.
 
Mtoa mada umesema ukweli kabisa mada bila Lowassa kuhama na kingunge CCM isingeshinda kwani walikuwa wameichafua mno hao wazee kiasi kwamba wapinzani wangepata cha kusema. Ushauri wangu,Lowassa mzee Lowassa tunakuomba baba ukaze kamba uendelee kuionea huruma CCM ili 2020 ugombee tena urais then CCM ipate tena mteremko. Asand mleta mada kwa kutufumbua macho.
Mimi sio mleta mada Mkuu
 
T
Kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza bwana mmoja kwa kujaribu kujitambua kua anamheshimu sana Mh Lowassa, hivi ndivyo inavyotakiwa na wanatakiwa wajitokeze na wengine kusema wazi kua wanamheshimu mzee wa kazi!

Nirudi kwenye mada;Kwa historia ya Mh Lowassa ndani ya CCM yeye na Mzee Kingunge ndio watu wenye mchango mkubwa katika chama hicho kuliko hata hao waliokua wakiropoka hadharani na kuwapakaa matope bila aibu wada adabu,Lowassa huyu anayekifahama chama cha mapinduzi kwa muundo wake wa ndani na nje aamue sasa anataka kukiua chama cha mapinduzi bado kutakua na chama hapo? Lowassa huyu huyu ambaye baadhi ya makada wa CCM wanatamka wazi wazi kua msaada mkubwa kwa ushindi wa CCM katika chaguzi zilizopita?

CCM wanashindwa kuelewa kua ndani yao bado kuna masalia watiifu kwa Mh Lowassa na wanashiriki vikao vizito vya chama,CCM wanasahau kua ukimya wa Mh Lowassa baada ya uchaguzi kuliwapa uchungu mkubwa wafuasi wake ndani na nje ya chama? CCM wanasahau tu baada ya Lowassa kikatwa pale mjini Dodoma ukumbi ulizizima kulitajataja na kuliimba jina lake tu"Tunaimani na Lowassa"? CCM wanafikiri maswahiba wa Lowassa ndani ya chama chao watasambarika kirahihisi tu? CCM walishawahi kusikia Lowassa akiwaponda waliosalia CCM? Kama sio wanadhani watamchukia swahiba wao kirahisi tu?

Nafikiri hapa ni kama Lowassa amewasamehe na kuwahurumia maana hawajui watendalo, Lowassa ni bingwa wa siasa za Tanzania ila ameamua kutanguliza busara na kuutambua uwepo wa Mungu, Kulithibitisha hilo ni pale ambapo katika kampeni zake hakuwahi kumshambulia wala kumtukana mwanaCCM yeyeote wakati wao wanamsakama kwa matusi.Nina uhakika Lowassa akitamka mdomoni mwake Leo"Nataka kuisambaratisha CCM" kitakua ni kilio cha kusaga meno kwa CCM.
Mwenyezi Mungu ni muweza wa yote. Katuwezesha tuishi katika fikara tofauti sana na bado anatupatia mahitaji ya lazima kwa usawa na pengine kuwazidishia zaidi hata wanaomkana. Fikiria mtu anawaweka pamoja lowasa na kingunge na kuwapa sifa zote wakati pengine hakuwahi kumpa sifa hata mmoja wao kabla ya kuhamia upande wa pili. Ni wazi kwamba Lowasa anaupenda na kuutamani sana urais kuliko kitu chochote na alikuwa radhi kufanya lolote ili aupate. Ukiona hakuwa akijibu mapigo ya CCM wakati wa kampeni ni vile alijua alikuwa mchafu zaidi na aliogopa wasije mvua nguo zaidi. Haikuwa kwa sababu aliwahurumia. Hakuwa na lolote na hatakuwa na lolote mbeleni.
 
Kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza bwana mmoja kwa kujaribu kujitambua kua anamheshimu sana Mh Lowassa, hivi ndivyo inavyotakiwa na wanatakiwa wajitokeze na wengine kusema wazi kua wanamheshimu mzee wa kazi!

Nirudi kwenye mada;Kwa historia ya Mh Lowassa ndani ya CCM yeye na Mzee Kingunge ndio watu wenye mchango mkubwa katika chama hicho kuliko hata hao waliokua wakiropoka hadharani na kuwapakaa matope bila aibu wada adabu,Lowassa huyu anayekifahama chama cha mapinduzi kwa muundo wake wa ndani na nje aamue sasa anataka kukiua chama cha mapinduzi bado kutakua na chama hapo? Lowassa huyu huyu ambaye baadhi ya makada wa CCM wanatamka wazi wazi kua msaada mkubwa kwa ushindi wa CCM katika chaguzi zilizopita?

CCM wanashindwa kuelewa kua ndani yao bado kuna masalia watiifu kwa Mh Lowassa na wanashiriki vikao vizito vya chama,CCM wanasahau kua ukimya wa Mh Lowassa baada ya uchaguzi kuliwapa uchungu mkubwa wafuasi wake ndani na nje ya chama? CCM wanasahau tu baada ya Lowassa kikatwa pale mjini Dodoma ukumbi ulizizima kulitajataja na kuliimba jina lake tu"Tunaimani na Lowassa"? CCM wanafikiri maswahiba wa Lowassa ndani ya chama chao watasambarika kirahihisi tu? CCM walishawahi kusikia Lowassa akiwaponda waliosalia CCM? Kama sio wanadhani watamchukia swahiba wao kirahisi tu?

Nafikiri hapa ni kama Lowassa amewasamehe na kuwahurumia maana hawajui watendalo, Lowassa ni bingwa wa siasa za Tanzania ila ameamua kutanguliza busara na kuutambua uwepo wa Mungu, Kulithibitisha hilo ni pale ambapo katika kampeni zake hakuwahi kumshambulia wala kumtukana mwanaCCM yeyeote wakati wao wanamsakama kwa matusi.Nina uhakika Lowassa akitamka mdomoni mwake Leo"Nataka kuisambaratisha CCM" kitakua ni kilio cha kusaga meno kwa CCM.

Nawewe ni mmojawapo kwenye mpango mpya wa Sh.Bilion 3 ili kumjenga Mtandaoni?
 
Back
Top Bottom