Hivi CCM wanasoma alama za nyakati?

Silas A.K

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
807
157
Nimeshitushwa na tamko la CCM kuhusiana na ''walkout'' ya wabunge wetu kupitia chama cha chadema.Ninachelea kusema CCM haina watu makini na wanakurupuka kutoa tamko bila kuliangalia suala hili kwa kina na kuangalia athari au madhara ya hatua yoyote ya kukurupuka kufanya maamuzi kwa taifa hili. kitu kimoja wanasahau ni kwamba bado hali tete na wananchi walio wengi walionyimwa haki yao kwa kuchaguliwa viongozi wasiowapigia kura hawajui next course of action. wananchi hawa ambao walikesha katika vituo vya kutangazia matokeo wakati wa uchaguzi uliopita bado wana vidonda vya kupokwa ushindi wao na hawatakubali tena kuona wabunge wao wakiendelea kunyanyaswa.Nafikiri badala ya kutafuta njia ya mkato katika kutafuta suluhu ya jambo hili serikali ya CCM inapaswa kuona utete wa jambo hili na kulitafutia ufumbuzi wa haraka ili kuendeleza kile wanachoita amani na mshikamano. CCM wanapaswa kuelewa kwamba watanzania wa leo si watanzania wa jana tatizo kubwa ni kwamba CCM kinawazee wengi kwenye vyombo vyao vya maamuzi na hivyo maamuzi yao hayareflect mawazo na matazamio ya watu wengi katika nchi hii. Rai yangu ni kwa CCM kuacha kukurupuka katika hili na kuliangalia katika upeo tofauti ili kuepusha matatizo yasiyo ya lazima.
 
Wanajidanganya nyang'au hawa, jaribio lolote la kuhujumu Chadema litachafua hali ya hewa, wajaribu waone mziki wake.
 
Hii ndio advantage ya kuwa na wabunge wengi vijana kwa chadema,
na hii ndio disadvantage ya kuwa na viongozi wengi wazee kwa ccm.
Hii muvie ni kali sana.
 
Nadhani CCM wanajua wanachokifanya.

Hawana asili ya kukurupuka.

Tusubiri tuone, lakini ninahisi itakula kwa Chadema.
 
Nadhani CCM wanajua wanachokifanya.

Hawana asili ya kukurupuka.

Tusubiri tuone, lakini ninahisi itakula kwa Chadema.
Hata chaedama wanajua wanachokifanya.
Ndi maana nikasema hii movie ni kali sana ila mpaka sasa ccm ameshalazwa sijui kama atasawazisha.
 
nadhani ccm wanajua wanachokifanya.

Hawana asili ya kukurupuka.

Tusubiri tuone, lakini ninahisi itakula kwa chadema.
kishoka tafadhali kaongee na uongozi wako na uwaaambie si kila sehemu matumizi ya pesa yanafanya kazi sometimes watumie vichwa vyao katika kuamua mambo! Mi sijui itakula kwa nani ila sipendi ile kwa mtu nataka haki itendeke! Hakuna mambo ya kulana hapa.
 
A simple question kwa sisiem; Chadema wangechakachua kura na wakashinda, sisiem wangemtambua rais wa Chadema na wakubali kusikiliza hotuba ya Dr. Wakweli?
 
HATA chadena wanajua walifanyalo wameshapitia vifungu vyote vya kanunu za bunge na kuona sio tatizo ku
wasilisha mawazo yako kwa mtindo ule. Chiligati alishindwa kuonyesha ni kifungu kipi cha katiba au kanuni ip
i ya bunge imevunjwa ajenge hoja zake.bado na wenyewe ccm hawana huhakika ni wapi hasa pa kuwabana
chadema mechi bado ngumu mkuu
Nadhani CCM wanajua wanachokifanya.

Hawana asili ya kukurupuka.

Tusubiri tuone, lakini ninahisi itakula kwa Chadema.
 
Tatizo ccm wanategemea alama za nyota za SHEKHE Y.H! watasubiri atabiri kitakachotokea ili nao wafanye uamuzi. By the way shekhe hajasikika tena baada ya utabiri wa kifo cha mgombea maarufu wa urais kutotimia, au aliprovide majini ya kuzuia kifo hicho?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom