Nimeshitushwa na tamko la CCM kuhusiana na ''walkout'' ya wabunge wetu kupitia chama cha chadema.Ninachelea kusema CCM haina watu makini na wanakurupuka kutoa tamko bila kuliangalia suala hili kwa kina na kuangalia athari au madhara ya hatua yoyote ya kukurupuka kufanya maamuzi kwa taifa hili. kitu kimoja wanasahau ni kwamba bado hali tete na wananchi walio wengi walionyimwa haki yao kwa kuchaguliwa viongozi wasiowapigia kura hawajui next course of action. wananchi hawa ambao walikesha katika vituo vya kutangazia matokeo wakati wa uchaguzi uliopita bado wana vidonda vya kupokwa ushindi wao na hawatakubali tena kuona wabunge wao wakiendelea kunyanyaswa.Nafikiri badala ya kutafuta njia ya mkato katika kutafuta suluhu ya jambo hili serikali ya CCM inapaswa kuona utete wa jambo hili na kulitafutia ufumbuzi wa haraka ili kuendeleza kile wanachoita amani na mshikamano. CCM wanapaswa kuelewa kwamba watanzania wa leo si watanzania wa jana tatizo kubwa ni kwamba CCM kinawazee wengi kwenye vyombo vyao vya maamuzi na hivyo maamuzi yao hayareflect mawazo na matazamio ya watu wengi katika nchi hii. Rai yangu ni kwa CCM kuacha kukurupuka katika hili na kuliangalia katika upeo tofauti ili kuepusha matatizo yasiyo ya lazima.