Hivi CCM wana ujasiri gani kampeni za uchaguzi wakiwa na ESCROW?

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,480
907
Hili sakata la ufisadi na ujambazi wa ESCROW uliofanywa na vigogo wa CCM, je bado wana ujasiri wa kufanya campaign?
 
ccm wamefika mahala pabaya sana ebu fikiria mtuhumiwa wa escrow anatoa ushauri wake nini kifanywe kuhusu suala la escrow can you imagine judge amuulize mtuhumiwa nini cha kufanya kuhusu kesi yake? ccm hawana aibu tena kilichobakia wananchi wawafundishe adabu tu hakuna kingine
 
Zamani walikuwa wakivaa magwanda ya kijani ,siku hizi ni aibu kumukuta mtu amevaa magwanda ya ccm akitembea mujini ,wanajificha ile mbaya ,zaidi utakuta kwenye vijimikutano vyao wamevaa,ajabu zote mpya ,wakiashiria zimegaiwa siku ya kuamkia mkutano ,kumbe mkutano ukimaliza wanaambiwa wazirudishe.
 
Kwasababu. Wanajua watanzania wanaakili kama za kuku. Kuku unawatupia maindi alafu wanakufuata. Kisha unamchukua mmoja wao na kumchinja mbele yao na kumla. Chaajabu hata baadae ukiendelea kuwarushia maindi kuku wataendelea kuja.
 
Hili sakata la ufisadi na ujambazi wa ESCROW uliofanywa na vigogo wa CCM, je bado wana ujasiri wa kufanya campaign?

Ujasiri upo mkubwa sana kwa kuwa tayari wana noti za ESCROW zinatosha kuwalaghai Wadanganyika
 
Kwasababu. Wanajua watanzania wanaakili kama za kuku. Kuku unawatupia maindi alafu wanakufuata. Kisha unamchukua mmoja wao na kumchinja mbele yao na kumla. Chaajabu hata baadae ukiendelea kuwarushia maindi kuku wataendelea kuja.

Diku hizi tumekuwa njiwa, chinja njiwa mbele ya wenzake uone.
 
sisi kina gogo la shamba tunaendelea kuesabu siku,leo hii ni siku ya nane tangu maazimio ya bunge kuhusu suala la Escrow
 
sisi kina gogo la shamba tunaendelea kuesabu siku,leo ni siku ya nane tangu maazimio ya suala la Escrow
 
CCM wana ujasiri kwa kuwa wanajua kuwa watanzania wengi ni mataahira! Wakihongwa tu chumvi, kanga na vikofia vya kijani, kura zote kwa CCM. Aliyesema kuwa mtaji wa CCM ni ujinga wa watanzania alipatia sana.
 
Back
Top Bottom