Hivi CCM wana uhalali gani wa kusema eti wanatumbua majipu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,682
149,885
Hivi ni serikali ya chama gani iliyotufikisha hapa tulipo?

Kabla ya kuanza kutumbua hayo majibu,wao wenyewe wanawajibika vipi?

Chama kilichokuwa kinasimamia serikali na bado wizi umetokea huku taifa likiingia hasara,wana uhalali gani wa kuendelea kupokea ruzuku wakati kazi imewashinda?

Unamwajibisha Mkurugenzi wa shirika au Taasisi fulani,aliekuwa anamsimamia unamuachaje?

Hivi tunapaswa kupongeza au kusikitika?

Hivi tunajitambua?

Hii nchi na watu wake kuna siri tusioijua!!!
 
Si tupo hapa JF. Huyu anayetumbua majipu ilhali naye jipu yani ni sarakasi ya aina yake.
 
Mkuu watanzania wanafiki,vyombo vya habar ni wanafik pia,haya uliyosema ingekuwa waandishi wa habar wa kenya,wangeuchambua utawala uliopita wa ccm na wa sasa tungepata jibu sahihi.Utawala wa ccm unatakiwa kushitakiwa kwa kututia umaskin namna hii.
 
Wako humu Jf wanahangaika na Chadema. Kila kukicha wao ni Chadema. Agenda yao ni Chadema! Na kazi nyngne walionayo ni kumtetea mkwere kwa kila post inayoletwa humu. Ndo maana wamekataza hata mikutano ya vyama vya siasa!!
Yaani wanajitumbua wao wenyewe ndo maana wanaweweseka na hawana agenda maalum.
 
Tangu zoezi la utubuaji majipu lianze ili kuboresha huduma za jamii, majipu mengi ukifatilia utabaini yanatoka CCM.

Kwa kitendo hiki yawezekana waliojitoa CCM walikuwa majipu yaliyokimbia kutumbuliwa!
 
taratibu mkianza kuguswa msianze kulalamika kuwa magu ana visasi na watu wa upinzani maana kuna vilaza waliokuwa wameanza kulalamika
 
Hivi ni serikali ya chama gani iliyotufikisha hapa tulipo?

Kabla ya kuanza kutumbua hayo majibu,wao wenyewe wanawajibika vipi?

Chama kilichokuwa kinasimamia serikali na bado wizi umetokea huku taifa likiingia hasara,wana uhalali gani wa kuendelea kupokea ruzuku wakati kazi imewashinda?

Unamwajibisha Mkurugenzi wa shirika au Taasisi fulani,aliekuwa anamsimamia unamuachaje?

Hivi tunapaswa kupongeza au kusikitika?

Hivi tunajitambua?

Hii nchi na watu wake kuna siri tusioijua!!!
Kijana hivi hujui huyo Edward mliyemfuata ni moja ya watu waliotuumiza sana,wewe si ulikuwa naye huku kabla ya kujiunga chadema?..wacha kujidhalilisha!
 
Back
Top Bottom