Hivi CCM inapendwa sana na kuaminiwa au wananchi wenye uzalendo wamekosa chama mbadala?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,725
141,585
Wakati mwingine huwa najiuliza sana kama watanzania wana imani na upendo wa kweli kwa CCM au wanakosa tu chama mbadala kwa kuwa vilivyopo ni vibovu kuliko CCM.

Nimeshuhudia namna Waziri mkuu mh Majaliwa alivyopambana kuibua wizi ufisadi na vitendo vya uzembe uliopindukia huko Morogoro na Iringa.

Kiukweli CCM bado haijabadilika na viongozi wake wanaishi kimazoea.

Haiwezekani mtu anaenda kujenga ukumbi na bar kwenye viwanja vya shule ambayo walimu wake wengi ni wake wa viongozi na makada wa chama na CCM inaangalia tu

Hata kama manispaa iko chini ya Chadema lakini mkurugenzi na watendaji wake wako chini ya CCM na ndio waliouza eneo la shule

Johnthebaptist nimesikitishwa sana lakini ninashukuru kwa kuwa mh Rais Magufuli na mh Waziri mkuu Majaliwa wanaijua Gangilonga tangu wakiwa vijana.......eneo hilo halitaporwa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wakati mwingine huwa najiuliza sana kama watanzania wana imani na upendo wa kweli kwa CCM au wanakosa tu chama mbadala kwa kuwa vilivyopo ni vibovu kuliko CCM.

Nimeshuhudia namna Waziri mkuu mh Majaliwa alivyopambana kuibua wizi ufisadi na vitendo vya uzembe uliopindukia huko Morogoro na Iringa.
Kiukweli CCM bado haijabadilika na viongozi wake wanaishi kimazoea. Haiwezekani mtu anaenda kujenga ukumbi na bar kwenye viwanja vya shule ambayo walimu wake wengi ni wake wa viongozi na makada wa chama na CCM inaangalia tu

Hata kama manispaa iko chini ya Chadema lakini mkurugenzi na watendaji wake wako chini ya CCM na ndio waliouza eneo la shule

Johnthebaptist nimesikitishwa sana lakini ninashukuru kwa kuwa mh Rais Magufuli na mh Waziri mkuu Majaliwa wanaijua Gangilonga tangu wakiwa vijana.......eneo hilo halitaporwa.

Maendeleo hayana vyama!
...vyama mbadala vipo sana ila sisi wana CCM tukijaribu kujiunga navyo au kuviunga mkono, tunakumbana na mizengwe ya kufukuzwa kazi, kudunishwa kimaisha na hata kutishiwa jela au ahera kabisa.

hapo ndipo penye shida!
 
Kwa mfano Chadema hata chaguzi za ndani hawafanyi......je kinaweza kuwa mbadala " halali" wa CCM?!!
 
Hili neno!.
Hata mimi huko nyuma niliwahi kuuliza maswali mengi tuu kuhusu CCM.
Miongoni mwao ni haya

P
 
Huko CCM mwendo ni wa samaki mkubwa kula mdogo. Hata Vodacom ulikuwa mradi wa chama lakini matokeo yake samaki wakubwa wameuza shares South Africa.
 
Hili neno!.
Hata mimi huko nyuma niliwahi kuuliza
P

Unajiuliza jambo ambalo liko wazi? Huoni mfumo wa uchaguzi ukoje, je huoni ukatili na uhayawani wa wazi nyakati za uchaguzi ili ccm iendelee kuwa madarakani, kinyume cha matakwa ya umma? Ni ukweli usio na chembe ya shaka kwamba ccm sio chama cha siasa, bali ni taasisi ya dola iliyojivika koti la chama cha siasa.
 
Hata isipopendwa na Wananchi tutapendwa na TUME ya Uchaguzi pamoja na vyombo vya usalama hawa niwapiga kura tosha kabisa. Kikubwa ni Usalama wa nchi tu ambapo ni wajibu wa CCM kufanya hivyo.. Kama hutaki basi wewe Mbishi tuu.. :p :p
 
Vyama mbadala vipo lakini ni dhaifu mno na viongozi wake hawana mawazo mbadala ya kujenga na wakiwa na mawazo mbadala basi mbadala huo ni wa kutukana viongozi wa serikali na chama tawala
 
Vyama vingi vya upinzani havikuanzishwa kwa nia ya kuongoza nchi au wananchi, vingi vilikuwa ni vya kutafuta ulaji tu. Hatuna sababu ya kuwa na utitiri wa vyama vingi kama nia ni kuongoza nchi na kuleta maendeleo. Vyama viwili au vitatu vinatosha kutatua matatizo ya wananchi na nchi kwa ujumla.
 
hapana, wanadai eti vikao vya ndani vya Chadema havijapewa kibali cha polisi.
wakati mwingine wanasema eti intelijensia yao imewaonyesha viashiria vya uvunjifu wa amani!
yaani chama chetu CCM kinaiogopa mno Chadema na Mbowe hadi sisi wafukurukutwa chama tunapatwa na kinyaa na kichefuchefu kwa kweli!!
 
Back
Top Bottom